Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 878
- 2,014
NCHI INAZAMA KWA KUKUMBATIA UJINGA
Je, umewahi kujiuliza kwa nini nchi hii haipigi hatua licha ya kuwa na rasilimali, amani, na nafasi za kujikwamua? Sababu iko wazi: tunakumbatia ujinga na kusambaza mzigo wa maamuzi yetu mabaya kwa wengine.
Mtu anataka kondomu afadhiliwe, akishindwa kuitumia na kupata VVU, anataka dawa za kufubaza ugonjwa zitolewe bure. Akimpa mwanamke mimba, anataka mtoto azaliwe kwa ufadhili wa serikali. Watu hawa ndio wale wale ambao wakifika hospitali kujifungua, hawana hata shilingi 5,000 ya kununua glovu za daktari, lakini wanaamini ni haki yao kupata kila kitu bure. Kwa nini? Kwa sababu wameshawishika kuwa serikali inapaswa kuwajibika kwa kila uamuzi wao mbovu maishani.
Hili suala linafanana kabisa na chuki dhidi ya kauli za RC Chalamila. Yaani mtu amebeba ujauzito bila kuwa na uhakika wa hata shilingi elfu tano ya vifaa vya kujifungulia, halafu anakuja hospitali akiamini kila kitu kitaangukia bure kutoka kwa serikali. Hebu fikiria—ikiwa hata hela ya kondomu siku hiyo haikuwepo, serikali ndiyo ije kubeba mzigo wa mtoto wako? Na kama kweli huna uwezo hata wa kununua glovu, unadhani kweli utakuwa na uwezo wa kumlea huyo mtoto?
Ni mentality hii hii tunayoiona kwa ARV. Mtu anaamua kufanya zinaa bila kinga, akipata UKIMWI anataka matibabu yatolewe bure. Ndio maana mpaka misaada ya Wamarekani inahitajika kulisha taifa linalozaliana bila mpango. Watu milioni 60, lakini wanaochangia mfuko wa bima hawafiki hata milioni 5. Hao wachache ndio wanapaswa kubeba mzigo wa wengine wote? Na bado tunajiita taifa huru!
Tuache unafiki. Hii siyo tena hoja ya CCM au CHADEMA. Ukifukuza CCM na kuleta upinzani, hakuna miujiza itakayofanyika. Historia imetufundisha kuwa mabadiliko hayaji kwa kubadilisha majina ya viongozi, bali kwa kubadili tabia na mtazamo wa jamii. Tanzania ina watu milioni 60, lakini wenye mchango wa moja kwa moja kwenye pato la taifa hawazidi milioni 10. Unadhani nchi yoyote inaweza kuendelea ikiwa idadi kubwa ya watu wake ni mizigo?
Tazama tofauti kati ya Kenya na Switzerland. Miaka ya 1960, nchi hizi zilikuwa na idadi sawa ya watu, lakini leo Kenya ina watu zaidi ya milioni 50, wengi wao wakiishi kwenye umasikini, huku Switzerland ikiwa na milioni 7 wanaoishi maisha mazuri. Unadhani ni kwa bahati mbaya? Hapana. Ni kwa sababu kule watu walitumia akili, huku kwetu wengi wanaamini "Mungu atajalia" huku wakizaliana bila mpango na kutegemea serikali iwahudumie.
Kama hatutabadilika, tusitarajie maendeleo. Tusipokuwa wakweli kwa nafsi zetu, tutaendelea kulalamika huku tukizidi kuzama kwenye lindi la umasikini wa kujitakia.