Ukiondoa Ukakasi wa Kauli za RC Chalamila Mnyonge Mnyongeni Ila Haki Yake Mpeni, Waafrika Tunapenda Kulelewa Mpaka Imekuwa Ulemavu

Ukiondoa Ukakasi wa Kauli za RC Chalamila Mnyonge Mnyongeni Ila Haki Yake Mpeni, Waafrika Tunapenda Kulelewa Mpaka Imekuwa Ulemavu

Ninaunga mkono hoja ya mpagani Kiranga. Serikali na wananchi kwa pamoja wana makosa. Makosa ya serikali ni kutumia pesa nyingi kwenye baadhi ya vitu visivyo vya lazima kama vile kuwabadilishia viongozi magari. Upande wa wananchi ni kama ulivyoelezea.
Kwani ulikuwa huwezi kuweka hoja yako bila kuniita mimi mpagani?

Kwanza mimi si mpagani na kuniita mpagani kunaonesha huelewi mpagani ni nani.
 
Huduma bora za afya ni haki ya kila mtu lakini linapokuja swala la huduma ya afya za bure hapo ni lazima tuwe makini.
Chalamila siyo mnafiki, viongozi wengine wengi watuaminisha kuwa mama mjamzito anatakiwa kutokuchangia chochote lakini ukweli hauopo hivyo.
Ni kweli tunalipa kodi, lakini matatizo ya mfumo wa nchi yetu yamesababisha kushindwa kutolewa kwa huduma za bure kwa wananchi.
Kwa mantiki hiyo ukitaka kupata huduma iliyobora iwe ya afya, elimu na mambo mengineyo ni vyema kujipanga na kwenda kwa watoa huduma binafsi, kule utapata huduma bora na yenye kukidhi.
 
Rc Chalamila hajakosea kitu chochote.
Mke wako unampa mimba, anakuwa mja mzito since day one ujue umeingia kwenye majukumu.
Ukienda Clinic siku ya kwanza wanakuhasa kufanya maandalizi pamoja na kuweka hakiba.
Sasa inakuwaje inafika hadi miezi tisa bado mtu analialia eti ameombwa 50000 ya gloves?
Sisi watanzania tunapenda vitu vya bure na kudanganywa danganywa na watawala.
Hakuna kitu cha bure katika mfumo wa ubepari.
Tumeambiwa elimu bure lakini sasa kwa kuwa ni bure amka asubuhi umpeleke mwanao shuleni kawambie amekuja kusoma tu bila vitu vya msingi uone kama utatoboa.
Sisi kama wananchi tufike wakati tuwe na fikra huru, mtu akikwambia hiki ni bure uwaze mara mbili na ujiongeze.
Mimba na mtoto atakayezaliwa ni wako wala siyo wa RC Chalamila.
Kama kakosea ni katika ile hali ya kushindwa kujenga hoja lakini alitaka kuwambia kuwa there's no free lunch.
Basi tukuite

Menyewe ipo kundi gani?
 
NCHI INAZAMA KWA KUKUMBATIA UJINGA

Je, umewahi kujiuliza kwa nini nchi hii haipigi hatua licha ya kuwa na rasilimali, amani, na nafasi za kujikwamua? Sababu iko wazi: tunakumbatia ujinga na kusambaza mzigo wa maamuzi yetu mabaya kwa wengine.

Mtu anataka kondomu afadhiliwe, akishindwa kuitumia na kupata VVU, anataka dawa za kufubaza ugonjwa zitolewe bure. Akimpa mwanamke mimba, anataka mtoto azaliwe kwa ufadhili wa serikali. Watu hawa ndio wale wale ambao wakifika hospitali kujifungua, hawana hata shilingi 5,000 ya kununua glovu za daktari, lakini wanaamini ni haki yao kupata kila kitu bure. Kwa nini? Kwa sababu wameshawishika kuwa serikali inapaswa kuwajibika kwa kila uamuzi wao mbovu maishani.

Hili suala linafanana kabisa na chuki dhidi ya kauli za RC Chalamila. Yaani mtu amebeba ujauzito bila kuwa na uhakika wa hata shilingi elfu tano ya vifaa vya kujifungulia, halafu anakuja hospitali akiamini kila kitu kitaangukia bure kutoka kwa serikali. Hebu fikiria—ikiwa hata hela ya kondomu siku hiyo haikuwepo, serikali ndiyo ije kubeba mzigo wa mtoto wako? Na kama kweli huna uwezo hata wa kununua glovu, unadhani kweli utakuwa na uwezo wa kumlea huyo mtoto?

Ni mentality hii hii tunayoiona kwa ARV. Mtu anaamua kufanya zinaa bila kinga, akipata UKIMWI anataka matibabu yatolewe bure. Ndio maana mpaka misaada ya Wamarekani inahitajika kulisha taifa linalozaliana bila mpango. Watu milioni 60, lakini wanaochangia mfuko wa bima hawafiki hata milioni 5. Hao wachache ndio wanapaswa kubeba mzigo wa wengine wote? Na bado tunajiita taifa huru!

Tuache unafiki. Hii siyo tena hoja ya CCM au CHADEMA. Ukifukuza CCM na kuleta upinzani, hakuna miujiza itakayofanyika. Historia imetufundisha kuwa mabadiliko hayaji kwa kubadilisha majina ya viongozi, bali kwa kubadili tabia na mtazamo wa jamii. Tanzania ina watu milioni 60, lakini wenye mchango wa moja kwa moja kwenye pato la taifa hawazidi milioni 10. Unadhani nchi yoyote inaweza kuendelea ikiwa idadi kubwa ya watu wake ni mizigo?

Tazama tofauti kati ya Kenya na Switzerland. Miaka ya 1960, nchi hizi zilikuwa na idadi sawa ya watu, lakini leo Kenya ina watu zaidi ya milioni 50, wengi wao wakiishi kwenye umasikini, huku Switzerland ikiwa na milioni 7 wanaoishi maisha mazuri. Unadhani ni kwa bahati mbaya? Hapana. Ni kwa sababu kule watu walitumia akili, huku kwetu wengi wanaamini "Mungu atajalia" huku wakizaliana bila mpango na kutegemea serikali iwahudumie.

Kama hatutabadilika, tusitarajie maendeleo. Tusipokuwa wakweli kwa nafsi zetu, tutaendelea kulalamika huku tukizidi kuzama kwenye lindi la umasikini wa kujitakia.
Nchi yetu yenyewe inategemea misaada. Like father like son bro acha kukaza hilo fuvu
 
Nyepesi kwa Ghana kwasababu ina idadi ya Watu wachache zaidi yetu (50% less) na pato la taifa kwa kila mtu (GDP per Capita) ni mara mbili yetu
Kodi mnazokusanya mnauliza zinaenda kufanya nini? Madeni ya mikopo ya kimataifa hayajilipi yenyewe; wote milioni 66 tunahitaji barabara, maji, hospitali, shule, umeme, ajira na kadhalika ila tunachozalisha kwa mkupuo kujustify matumizi hayo yote hakiakisi uhalisia yaani hata tukiondoa ufisadi katika mahesabu bado changamoto bado kubwa sana
Mimi naamini yote hii inatokana na kuwa na uongozi na serikali mbovu na hili siyo tatizo la Tanzania pekee, ni Africa kwa ujumla.

Serikali inahitajika kuweka vipaumbele vizuri na kusimamia rasilimali kwa ufanisi. Ikiwa watu wanapaswa kulipia vitu vya msingi kama vile gloves, inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa katika sekta ya afya ambayo inahitaji utatuzi wa haraka.

Serikali inapaswa kupunguza matumizi yake ili kuwekeza nguvu na fedha katika sekta hii nyeti ya afya:

1. Kupambana na rushwa na usimamizi mbaya wa rasilimali: Moja ya mambo yanayochangia kupoteza rasilimali ni rushwa na matumizi yasiyofaa ya fedha za umma. Kuimarisha mifumo ya uwazi na uwajibikaji kunaweza kuzuia matumizi ya kifedha yasiyo ya lazima.

2. Kupunguza matumizi
yasiyo ya lazima: Serikali hutumia kiasi kikubwa cha fedha katika miradi ambayo haina manufaa ya muda mrefu kwa wananchi. Kupunguza matumizi haya na kuelekeza fedha katika sekta ya afya kunaweza kusaidia. Mfano, kupunguza matumizi ya magari ya kifahari, sherehe za kifahari za serikali, n.k.

3. Maboresho ya ukusanyaji Kodi: Kuongeza fedha kupitia sera za kodi za haki kunaweza kusaidia kufadhili huduma za afya. Hii inaweza kujumuisha kodi juu ya bidhaa. Yalifanyika mabadiliko ya ukusanyaji kodi zikaja tozo za miamala, ni pesa nyingi zinakusanywa lakini zinaelekezwa kwenye miradi isiyokuwa na tija kwa kila mwananchi.

Serikali yetu inakusanya kodi za kutosha tu ila kwenye usimamizi na matumizi ya mapato kumejaa wizi. Haiwezekani kama taifa tena linaloongozwa na mwanamke tunaona ni sawa kumuweka hatarini mama na mtoto huku fedha nyingi zikitumika kununua magari mapya ya wabunge, wakuu wa mikoa kwenda kutembelea miradi hewa wakati wagonjwa wakikosa dawa na vifaa tiba, kuchangia "goli la mama" inawezekana lakini kuchangia mama mjamzito kupata huduma muhimu bure ni anasa kwasababu inaonekana kama kupata ujauzito ilikuwa ni starehe yake.
 
Kodi zinazolipwa bado hazijafikia kiwango cha kutosha cha kutoa kila huduma bure.
Taifa lisiloweza kutoa huduma za msingi kama afya na elimu bure au kwa gharama nafuu tayari ni taifa lililofeli.
 
Mimi naamini yote hii inatokana na kuwa na uongozi na serikali mbovu na hili siyo tatizo la Tanzania pekee, ni Africa kwa ujumla.

Serikali inahitajika kuweka vipaumbele vizuri na kusimamia rasilimali kwa ufanisi. Ikiwa watu wanapaswa kulipia vitu vya msingi kama vile gloves, inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa katika sekta wa afya ambayo inahitaji utatuzi wa haraka.

Serikali inapaswa kupunguza matumizi yake ili kuwekeza nguvu na fedha katika sekta hii nyeti ya afya:

1. Kupambana na Rushwa na Usimamizi Mbaya wa rasilimali: Moja ya mambo yanayochangia kupoteza rasilimali ni rushwa na matumizi yasiyofaa ya fedha za umma. Kuimarisha mifumo ya uwazi na uwajibikaji kunaweza kuzuia matumizi ya kifedha yasiyo ya lazima.

2. Kupunguza matumizi Y
yasiyo ya lazima: Serikali hutumia kiasi kikubwa cha fedha katika miradi ambayo haina manufaa ya muda mrefu kwa wananchi. Kupunguza matumizi haya na kuelekeza fedha katika sekta ya afya kunaweza kusaidia. Mfano, kupunguza matumizi ya magari ya kifahari, sherehe za kifahari za serikali, n.k.

3. Maboresho ya ukusanyaji Kodi: Kuongeza fedha kupitia sera za kodi za haki kunaweza kusaidia kufadhili huduma za afya. Hii inaweza kujumuisha kodi juu ya bidhaa. Yalifanyika mabadiliko ya ukusanyaji kodi zikaja tozo za miamala, ni pesa nyingi zinakusanya lakini zinaelekezwa kwenye miradi isiyokuwa na tija kwa kila mwananchi.

Serikali yetu inakusanya kodi za kutosha tu ila kwenye usimamizi na matumizi ya mapato kumejaa wizi. Haiwezekani kama taifa tena linaloongozwa na mwanamke tunaona ni sawa kumuweka hatarini mama na mtoto huku fedha nyingi zikitumika kununua magari mapya ya wabunge, wakuu wa mikoa kwenda kutembelea miradi hewa wakati wagonjwa wakikosa dawa na vifaa tiba, kuchangia "goli la mama" itawezekana lakini kuchangia mama mjamzito kupata huduma muhimu bure ni anasa kwasababu inaonekana kama kupata ujauzito ilikuwa ni starehe yake.
Naunga mkono hoja
 
Amechanganya na atheist
Watu hawajui tofauti ya atheist na mpagani, wanajionesha utupu wao.

Anatutoa nje ya reli.

Back to Chalamila.

Chalamila kafeli zaidi ya presentation, kafeli uongozi.

Na wananchi wa Tanzania wengi bado wanaishi kijamaa, hata kijima.
 
Wananchi na viongozi wote ni tatizo, kiongozi ni wajibu wake kuhakikisha anatupatia huduma bora za afya, si anakusanya kodi zetu??

Wananchi wengi wao wavivu wanawaza kujifungia ndani kuzalisha mitoto mingi ambayo wanashindwa kuimudu..!!
Ukiwaambia wapange uzazi ni wabishi haswaa watu wa kanda ya ziwa 😹🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️
 
Nimesoma paragraphs 3 tu. Umeandika US3NGE, samahani.

Kodi tunazolipa zina msaada gani? Kuna nchi hapahapa Africa zina free healthcare. Ghana tu wana free maternal healthcare.
So long as tunafanya kazi na kulipa kodi, we deserve health care benefits, mbona wengine wanafanya, au kodi zetu zinaenda wapi?
Hivi vitu bila kufanya Mahesabu kila siku mtakua ni watu wa kulalamika,

Bajeti ya Afya 2023 ilikua ni Trilioni 1.2 kwa Nchi ambayo ina watu zaidi ya milioni 60 hio ni kama 20,000 kwa mwaka kwa kila mtu. Unaweza nipigia mahesabu 20,000 inatoaje huduma za Afya mwaka mzima bure? Kwa Pato la Taifa letu hata tukisema tunatumia 50% ya pato la Taifa kwenye Afya tu bado haitoshi kutoa Huduma bure, bado hapo mtu anataka Atibiwe bure, Elimu bure, ajengewe barabara etc.
 
Wale waandishi wa 'New Life in Kyerefaso' na 'My Newest Bride' walikuwa na lengo la kuwastua viongozi wa Africa miaka ile ya uhuru lakini poor Africans are still dancing todate.
 
Hivi vitu bila kufanya Mahesabu kila siku mtakua ni watu wa kulalamika,

Bajeti ya Afya 2023 ilikua ni Trilioni 1.2 kwa Nchi ambayo ina watu zaidi ya milioni 60 hio ni kama 20,000 kwa mwaka kwa kila mtu. Unaweza nipigia mahesabu 20,000 inatoaje huduma za Afya mwaka mzima bure? Kwa Pato la Taifa letu hata tukisema tunatumia 50% ya pato la Taifa kwenye Afya tu bado haitoshi kutoa Huduma bure, bado hapo mtu anataka Atibiwe bure, Elimu bure, ajengewe barabara etc.
Waache kufanya mambo ya starehe, wawekeze kwa mambo ya msingi hapo tutawaelewa. Watu wapo bitter kwa sababu serikali imewekeza kwenye luxuries na kusahau mambo ya msingi.
 
Tanzania bila kuweka sheria Kali ya kuzuia hii kasi ya kuzaliana ....tutalaumiana sana. Serikali haiwezi kukidhi mahitaji ya familia kubwa inayokua kwa kasi ya mwanga kwa rasilimali hizi hizi.
Iwekwe sheria ya kuzaa watoto wawili tu hadi idadi isimame kwenye million 65. Anayezingatia vigezo na kutii apewe ruzuku au zawadi.
 
Waache kufanya mambo ya starehe, wawekeze kwa mambo ya msingi hapo tutawaelewa. Watu wapo bitter kwa sababu serikali imewekeza kwenye luxuries na kusahau mambo ya msingi.
Sisemi kwamba wanunue ma V8 na kufanya Ubadhirifu, ila hata wakiacha kununua Still haitoshi, bado nchi yetu inakusanya kidogo, Trilioni 10-20 ni ndogo sana kwa Nchi ambayo ina watu milioni 60,
 
Back
Top Bottom