Ukiondoa Ukakasi wa Kauli za RC Chalamila Mnyonge Mnyongeni Ila Haki Yake Mpeni, Waafrika Tunapenda Kulelewa Mpaka Imekuwa Ulemavu

Ninaunga mkono hoja ya mpagani Kiranga. Serikali na wananchi kwa pamoja wana makosa. Makosa ya serikali ni kutumia pesa nyingi kwenye baadhi ya vitu visivyo vya lazima kama vile kuwabadilishia viongozi magari. Upande wa wananchi ni kama ulivyoelezea.
Kwani ulikuwa huwezi kuweka hoja yako bila kuniita mimi mpagani?

Kwanza mimi si mpagani na kuniita mpagani kunaonesha huelewi mpagani ni nani.
 
Huduma bora za afya ni haki ya kila mtu lakini linapokuja swala la huduma ya afya za bure hapo ni lazima tuwe makini.
Chalamila siyo mnafiki, viongozi wengine wengi watuaminisha kuwa mama mjamzito anatakiwa kutokuchangia chochote lakini ukweli hauopo hivyo.
Ni kweli tunalipa kodi, lakini matatizo ya mfumo wa nchi yetu yamesababisha kushindwa kutolewa kwa huduma za bure kwa wananchi.
Kwa mantiki hiyo ukitaka kupata huduma iliyobora iwe ya afya, elimu na mambo mengineyo ni vyema kujipanga na kwenda kwa watoa huduma binafsi, kule utapata huduma bora na yenye kukidhi.
 
Basi tukuite
Menyewe ipo kundi gani?
 
Nchi yetu yenyewe inategemea misaada. Like father like son bro acha kukaza hilo fuvu
 
Mimi naamini yote hii inatokana na kuwa na uongozi na serikali mbovu na hili siyo tatizo la Tanzania pekee, ni Africa kwa ujumla.

Serikali inahitajika kuweka vipaumbele vizuri na kusimamia rasilimali kwa ufanisi. Ikiwa watu wanapaswa kulipia vitu vya msingi kama vile gloves, inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa katika sekta ya afya ambayo inahitaji utatuzi wa haraka.

Serikali inapaswa kupunguza matumizi yake ili kuwekeza nguvu na fedha katika sekta hii nyeti ya afya:

1. Kupambana na rushwa na usimamizi mbaya wa rasilimali: Moja ya mambo yanayochangia kupoteza rasilimali ni rushwa na matumizi yasiyofaa ya fedha za umma. Kuimarisha mifumo ya uwazi na uwajibikaji kunaweza kuzuia matumizi ya kifedha yasiyo ya lazima.

2. Kupunguza matumizi
yasiyo ya lazima: Serikali hutumia kiasi kikubwa cha fedha katika miradi ambayo haina manufaa ya muda mrefu kwa wananchi. Kupunguza matumizi haya na kuelekeza fedha katika sekta ya afya kunaweza kusaidia. Mfano, kupunguza matumizi ya magari ya kifahari, sherehe za kifahari za serikali, n.k.

3. Maboresho ya ukusanyaji Kodi: Kuongeza fedha kupitia sera za kodi za haki kunaweza kusaidia kufadhili huduma za afya. Hii inaweza kujumuisha kodi juu ya bidhaa. Yalifanyika mabadiliko ya ukusanyaji kodi zikaja tozo za miamala, ni pesa nyingi zinakusanywa lakini zinaelekezwa kwenye miradi isiyokuwa na tija kwa kila mwananchi.

Serikali yetu inakusanya kodi za kutosha tu ila kwenye usimamizi na matumizi ya mapato kumejaa wizi. Haiwezekani kama taifa tena linaloongozwa na mwanamke tunaona ni sawa kumuweka hatarini mama na mtoto huku fedha nyingi zikitumika kununua magari mapya ya wabunge, wakuu wa mikoa kwenda kutembelea miradi hewa wakati wagonjwa wakikosa dawa na vifaa tiba, kuchangia "goli la mama" inawezekana lakini kuchangia mama mjamzito kupata huduma muhimu bure ni anasa kwasababu inaonekana kama kupata ujauzito ilikuwa ni starehe yake.
 
Kodi zinazolipwa bado hazijafikia kiwango cha kutosha cha kutoa kila huduma bure.
Taifa lisiloweza kutoa huduma za msingi kama afya na elimu bure au kwa gharama nafuu tayari ni taifa lililofeli.
 
Naunga mkono hoja
 
Amechanganya na atheist
Watu hawajui tofauti ya atheist na mpagani, wanajionesha utupu wao.

Anatutoa nje ya reli.

Back to Chalamila.

Chalamila kafeli zaidi ya presentation, kafeli uongozi.

Na wananchi wa Tanzania wengi bado wanaishi kijamaa, hata kijima.
 
Wananchi na viongozi wote ni tatizo, kiongozi ni wajibu wake kuhakikisha anatupatia huduma bora za afya, si anakusanya kodi zetu??

Wananchi wengi wao wavivu wanawaza kujifungia ndani kuzalisha mitoto mingi ambayo wanashindwa kuimudu..!!
Ukiwaambia wapange uzazi ni wabishi haswaa watu wa kanda ya ziwa πŸ˜ΉπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
 
Nimesoma paragraphs 3 tu. Umeandika US3NGE, samahani.

Kodi tunazolipa zina msaada gani? Kuna nchi hapahapa Africa zina free healthcare. Ghana tu wana free maternal healthcare.
So long as tunafanya kazi na kulipa kodi, we deserve health care benefits, mbona wengine wanafanya, au kodi zetu zinaenda wapi?
Hivi vitu bila kufanya Mahesabu kila siku mtakua ni watu wa kulalamika,

Bajeti ya Afya 2023 ilikua ni Trilioni 1.2 kwa Nchi ambayo ina watu zaidi ya milioni 60 hio ni kama 20,000 kwa mwaka kwa kila mtu. Unaweza nipigia mahesabu 20,000 inatoaje huduma za Afya mwaka mzima bure? Kwa Pato la Taifa letu hata tukisema tunatumia 50% ya pato la Taifa kwenye Afya tu bado haitoshi kutoa Huduma bure, bado hapo mtu anataka Atibiwe bure, Elimu bure, ajengewe barabara etc.
 
Wale waandishi wa 'New Life in Kyerefaso' na 'My Newest Bride' walikuwa na lengo la kuwastua viongozi wa Africa miaka ile ya uhuru lakini poor Africans are still dancing todate.
 
Waache kufanya mambo ya starehe, wawekeze kwa mambo ya msingi hapo tutawaelewa. Watu wapo bitter kwa sababu serikali imewekeza kwenye luxuries na kusahau mambo ya msingi.
 
Tanzania bila kuweka sheria Kali ya kuzuia hii kasi ya kuzaliana ....tutalaumiana sana. Serikali haiwezi kukidhi mahitaji ya familia kubwa inayokua kwa kasi ya mwanga kwa rasilimali hizi hizi.
Iwekwe sheria ya kuzaa watoto wawili tu hadi idadi isimame kwenye million 65. Anayezingatia vigezo na kutii apewe ruzuku au zawadi.
 
Waache kufanya mambo ya starehe, wawekeze kwa mambo ya msingi hapo tutawaelewa. Watu wapo bitter kwa sababu serikali imewekeza kwenye luxuries na kusahau mambo ya msingi.
Sisemi kwamba wanunue ma V8 na kufanya Ubadhirifu, ila hata wakiacha kununua Still haitoshi, bado nchi yetu inakusanya kidogo, Trilioni 10-20 ni ndogo sana kwa Nchi ambayo ina watu milioni 60,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…