Uchaguzi 2020 Ukiondoa Wana - CHADEMA na wafuasi wake mwenyewe, Tundu Lissu atapata kura nyingine nyingi kutoka kwa hawa

Uchaguzi 2020 Ukiondoa Wana - CHADEMA na wafuasi wake mwenyewe, Tundu Lissu atapata kura nyingine nyingi kutoka kwa hawa

Tangu mh Tundu Lissu arejee nchini mwezi Agosti, amekuwa akitoa matamko mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa yameweza ku reshape approach ya serekali ya awamu ya 5 katika utekelezaji wa mambo yake kadhaa.

Hii imepelekea makundi mbalimbali katika jamii ya Watanzania kunufaika kwa namna moja ama nyingine. Tafsiri ya hili ni kwamba bila ya intervention ya Lissu serekali isingeweza kuchukua hatua stahiki kwa manufaa ya makundi haya.

Makundi haya lazima yatakuwa yameshatambua mchango wa Lissu katika ufanikishwaji wa yale waliyokuwa wanayahitaji kutoka serekalini bila mafanikio kwa miaka yote 5 iliyopita.

Nina uhakika akilini mwao watakuwa wanajiuliza "Kama Tundu Lissu amewezesha haya ilihali hayuko madarakani, je haitakuwa zaidi pale atakapokuwa madarakani? Kwa nini tusimpe nchi kabisa tunufaike pakubwa zaidi?"

1. Walimu 13'000 ambao serekali imetangaza kuwapa ajira mpya - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

2. Wafanyabiashara waliopewa msaada wa sh milioni 100 - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

3. Wananchi walioahidiwa kujengewa barabara ya km 46 (Sengerema - Nyehunge) - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu.

4. Wananchi wa Itigi walioahdiwa kujengewa barabara ya km 16 - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

5. Wamachinga ambao Magufuli kawaambia si lazima tena kulipia elfu 20 kupata kitambulisho - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu.

6. Askofu Niwemugizi aliyerejeshewa passport yake baada ya Lissu kupiga spana - huyu pamoja na waumini wake na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

7. Kuanzia mwezi huu mshahara kima cha chini serekalini umepanda kutoka 170,000 hadi 270,000 - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

8. Kwa mara ya kwanza (baada ya kuwa anawafokea tu kwa miaka 5) Watanzania wamemwona mgombea urais wa CCM akiongea nao kwa kuwabembeleza - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu.

9. Ni makundi hayo tu kwa uchache, lakini yapo mengi unaweza kuongeza mengine.
10 waislamu wa kweli ambao mashekh na maimamu zao wapo jela bila kupelekwa mahakamani
Lissu hakusema wataachiwa ila amesema watapelekwa mahakamani shauri Lao lisikilizwe
Kwa hili
Takbirr
Allah Akbar
Kura zote za waumini zipo kwako
Kura zote za wanafikiri wa BAKWATA zipo kwa jiwe
Kwa muda mrefu watanzania tulikua tunasema
We can't breathe
Sasa jiwe linasema
I can't breathe
 
Endapo kweli hao wote watampigia kama ulivyosema.

Amesogea,Atapata 15% ya kura za wananchi wa kitanzania.

He already loosed this Game.
 
Back
Top Bottom