Ukiota ndotoni upo na Mheshimiwa Rais - hii ina maana gani?

Huwezi ukaota ndoto halafu ukayakumbuka maswali yote sita ya ndotoni. Haiwezekani
Ukishituka unawai kuandika...Mimi kipindi flani Nilitamani niwe msanii wa rap/ hip hop so Kuna muda unapata idea ya wimbo ndotoni ukishituka unawai kuchukua counter book na kuandika mistari chap chap...

Ukisema sijui uzembee unasahau chap.. ukishituka ndotoni then chap una andika

So inawezekana jamaa kafanya ivyo..
 
Nimeota Mh. Rais Samia Suluhu Hassan (Rais wa JMT) ameniona nimeketi kwenye umati wa wanafunzi wa Chuo Kikuu, tena niliketi mwisho kabisa (back bencher), sifahamu ni chuo gani, akaniita kwa ishara ya kuninyooshea kidole. Niliinuka nikamfuata kwa heshima na hofu, aliniamuru niwasaidie vijana wake wawili waliokuwa wamebeba mizigo midogo (mifuko miwili ya salfreti).

Mimi haraka sana niliwafuata wale vijana nikawapokea hiyo mizigo kisha nikaipeleka kwa mheshimwa Rais pale alipokuwa amesimama yeye. Lakini Mh. Rais akaniamuru nibebe hiyo mizigo kisha nimfuate. Tukaanza safari ya kwenda nyumbani kwake (Ikulu) sifahamu ni Ikulu gani lakini ni Ikulu huku tukitembea kwa miguu, niliongozana nae mimi na yeye (bila kuwepo mtu mwingine) huku nikiwa nimebeba mizigo yake miwili.

Wakati tukiwa njiani tunatembea kwa miguu, yeye yuko mbele mimi nipo nyuma, akaniuliza maswali kadhaa yafuatayo.

1. Swali la kwanza aliniuliza;
"Pale chuo ulipokuwa umeketi kwenye umati wa wanafunzi ulikuwa unafanya nini?"
Nikamjibu; "Nimekuja kwenye mahafali ya chuo, mimi ni mhitimu".

2. Swali la pili akaniuliza;
"Umehitimu ngazi gani ya elimu?"
Nikamtajia ngazi ya elimu niliyohitimu.

3. Kisha akaniuliza tena swali la tatu,
"Wewe ni mfanyakazi au ni nani?"
Nikamjibu; "Ndio, mimi ni mfanyakazi (nikamtajia na kazi ninayofanya).

Baada ya kumtajia kazi ninayofanya alinigeukia na kunitazama. Alinitazama usoni akawa anafurahi huku tukiwa tunatembea (kwasababu yeye alikuwa mbele mimi niko kwa nyuma).

4. Akaniuliza tena swali la nne,
"Unaishi wapi?"
Nikamjibu (nikamtajia eneo ninapoishi ambalo ni mbali kidogo na pale chuo aliponikuta).

5. Swali la tano aliniuliza;
"Nilikuona uliegesha pikipiki yako mahali fulani, kwahiyo huwa unasafiri na pikipiki yako kutoka huko uliko hadi huku?"
Nikamjibu; "Hapana, ile pikipiki ni kwa matumizi ya kuzunguka huku huku mjini, huwa nikitaka kurudi nyumbani naifungia pikipiki kwenye chumba cha huku chuo, kisha napanda gari, kwasababu naogopa sana ajali za pikipiki".
Nilipomjibu hivyo alicheka. Kisha akanigeukia tena akanitazama na kuniuliza;

6. Swali la sita aliloniuliza;
"Mbona unaonekana ni mdogo kiumri halafu elimu uliyohitimu ni kubwa?"
Nikacheka bila kumjibu chochote.

Tukaendelea na safari ya kutembea. Wakati tunaendelea na kutembea nikamdokeza jambo kwa kumwambia;
"Hata hivyo leo nimekuja kuchukua cheti changu nakwenda kukipeleka kwenye chuo kingine kwasababu tayari nishafanya application ya chuo ngazi inayofuata ya elimu hivyo walihitaji cheti".
Mheshimiwa Rais alisimama na kunigeukia, alionyesha kushangaa mno kisha akajibu kwa ufupi "He! Kumbe!".

Tuliendelea na safari huku nikiwa nimebeba mizigo yake. Tulifika nyumbani kwake (Ikulu), nilikuta watoto watatu wenye umri kati ya miaka 8 - 15 lakini siwafahamu wakiwa wanacheza, nilijitua ile mizigo yake nikaiweka chini. Wakati nataka kumuaga kwa maneno akawa anaongea na simu, kwahiyo nilimuaga kwa ishara ya mkono (bye) kisha nikaondoka. Sikufika mbali nikasikia ananiita.

Haraka sana nilikimbia kwenda kumsikiliza. Nilipofika karibu yake alitoa noti ya shilingi elfu tano akanipa kama asante ya kumbebea mizigo yake huku akisema; "Hii hela ni nauli yako nadhani inakutosha kwasababu una mishahara yako, uliniambia una kazi".
Nilitabasamu kisha nikamjibu; "Asante sana mheshimiwa, inatosha".
Kisha niliondoka.

Wakati narudi nipo njiani natembea kwa miguu nikawa nawaza yale yote niliyoulizwa na majibu niliyompa mheshimiwa Rais, ghafla nikashtuka usingizini. (MWISHO WA NDOTO).

Nimeshika simu yangu sasa hivi ni saa kumi na dakika thelasini na sita usiku (4:36 AM), Jumapili ya tarehe 12.01.2025

Mnaojua kutafsiri ndoto, hii ndoto ina maana gani?.
Haina maana zaidi ya hiyo maana.
 
Waweza opoa msa*a*i
 
Jiandae utapata kazi kwa gabachori
Na elimu yako kubwa atakua anakutuma viroba

Shabaaaniii peleka hiii staki onaaa
 
Mnaojua kutafsiri ndoto, hii ndoto ina maana gani?.
Jieleze vizuri mkuu tujue ulifanya naye nini, je ulijamiiana naye, ulipiga story naye au mlifanyeje.

Nasema hivi kwa sababu ukiitoa cheo rais ni mtu kama watu wengine unakuta nao kwenye ndoto.
 
Inafuatana,alikua ni kasongo au chura kiziwi?
 
Last year niliota NDOTO nipo nafanya mtihani wa chemistry Mimi na mdogo wangu wa toka ni toke mtiani ulikua mgumu nikawa nimeomba msaada wa majibu kwa mdogo wangu akanipa nikawa imebaki nususaa na maswali mengi sikua nimeyajibu..dogo akawa ananipa majibu mpaka nikamaliza pepa under pressure...

Asubuh ndoto ilinifikirisha Sanaa....siku simulia Ila siku iyo jioni nilipata ajari ya kugongea na gari na kuvunjika mguu wa kushoto...niliwasimulia watu NDOTO then two weeks later dogo akapata na yeye ajar akavunjika mkono..

In short NDOTO za kurudi shule huwa sio nzurii
Mkuu hii kwangu ni tofauti kabisa hakuna ndoto naipenda kama nipo shule nina ndoto kubwa sana ya kupata elimu kubwa hivyo ndoto nikiwa shule ni ndoto ambazo nazitafsili kama ktk ulimwengu roho ndoto yangu ya kupata elimu bado inatambulika na bado inaishi napata faraja kubwa sana kuwa siku inakuja na itakuwa na hakuna lolote baya na kila kitu kipo sawa. So mimi sitaki kuamini hilo kbs acheni kukili/kutii jambo jema kulivika ubaya hakika litkuja kama ulivyolipokea unapohisi ndoto yako si njema destroy it! Au hauna jins postpone yote yanawezekana usikubali ndoto mbaya itokee ile umeamka ikatae na uiuwe kabs hakuna kitakachotokea kila kitu kina mlango wa kutokea
 
Mimi mwaka jana wakati mwaka 2024 unaelekea mwishoni, niliota ndoto eti nilikuwa niko mahali fulani na rais Samia, pia walikuwepo watu wengine. Miongoni mwa hao watu wengine mmoja alikuwa ni mbaya wangu. Sasa Rais Samia akaniosha miguu na wale watu wengine walikuwa wanaangalia. Alipomaliza kuniosha miguu na ndoto ile ikaishia hapo.

Nilipoamka asubuhi nikawa naitafakari ndoto hiyo ina maana gani. Ikabidi nifunue Biblia nitafute kujua Biblia inasemaje kuhusu kuoshwa miguu. Nikasoma Yohane 13 yote na kuna ufunuo mwingine ambao nilipewa kuhusiana na ndoto ile lakini haumo kwenye Biblia na wala sitauanika hapa.

Lakini mimi katika kuipindisha ndoto ile , ikapelekea nikakomenti kwenye uzi fulani humu jamiiforums , comment yenyewe niliyocomment inasema " Mwakani ndo mtaelewa ni kwa nini Yesu Kristo aliwaosha miguu wanafunzi wake wakati wa chakula cha jioni." Ilikuwa ni wiki za mwishoni mwa mwaka 2024.
 
Back
Top Bottom