Mimi nilisha achana na habari za kuzingatia ndoto.
Japo nyingi za hizo kuna mazingira yanakuja kutokea halisi.
Mwaka ule wa 2019 niliota Magufuli amekuja kwenye chumba changu kama anakimbia jambo fulani na sehemu salama ya kujificha ni kwenye kile chumba changu!
Hii ilititokea baada ya kutoka kwenye kikundi cha maombi huko kanisani kwetu,na maombi maalumu yalikua kwa rais na nchi kwa kipindi kile corona ina anza .
Mwana maombi mmoja alitoa hoja ya kuona nchi na rais ipo kwenye mashambulizi makali hivyo tuombe, vile tuliomba sijawahi ona, na nakumbuka niliomba toka vilivyo, baada ya maombi kurudi nyumbani ndio naota magu kaja kujificha kwangu!
Ndoto bwana ni ule mzunguko wako wa kawaida wa kila siku unajirudia kwenye akili.