Ukipata muda nenda katembelee makaburi ya wazazi au ndugu zako

Ukipata muda nenda katembelee makaburi ya wazazi au ndugu zako

Kuna baraka nyingi unavyokuwa unatembelea makaburi wazazi au ndugu zako ambao uliwaona kwa macho yako mwenyewe walikuwa wanafanya mema hapa duniani.

Jitahidi kutembelea mara kwa mara ata kusafisha kaburi endelea kumuombea marehemu kwa Mungu wa mbinguni kuna baraka nyingi.
Kweli eeh!!

Na vipi kuhusu kitu alichokuwa anakipenda sana marehem ukienda nacho ukakiweka juu ya kaburi Ina uhusiano gani?
 
Ngoja lokolez & sabaths waje kukuuliza maswali hadi usahau uliliweka wapi jembe la kupalilia kaburi.🤔
Mimi ni mtu nisiyeamini kuwa omba wafu. Na ni matumaini yangu kuwa mtoa mada haongelei suala la ibada makaburini. Ila hili la kwenda na kupalilia, kutengeneza mazingira kuhakikisha kumbukumbu hazifutiki hasa kwa waliolala katika haki na matendo mema Nina ushuhuda.
Kuna jamaa alikuja town kutafuta spare za gari lake la biashara (kubeba abiria). Alipozipata akanishurutisha twende kuona kaburi la dada yangu ( alikufa katika Bwana) kufika tulilitafuta muda mrefu maana kilikuwa na pori tayari Mungu saidia tukalipata na kulifanyia usafi. Jamaa alipiga kazi si mchezo tukatoka jamaa kajaa vumbi hatari. Tulivyofika home akajifuta tu akaaga akasepa japo nilimshurutisha aoge akagoma.
Baada ya wiki Moja kupita alipata ajali iliyohusisha gari mbili yake ikiwemo na yeye akiwa dreva na abiria. Takribani Watu kumi na nane walipoteza maisha papo hapo akiwemo dreva WA gari jirani jamaa alipotolewa anasimulia aliona Watu wanalia wakiwa wametapakaa damu pale pale akachukua boda akasepa kizuri yeye NDIYE alikuwa konda na driver hivyo alikuwa na nauli zote mfukoni akatokomea kusikojulikana. Nikarejea jinsi alivyonilazimisha twende kupalilia kaburi la sister nikasema wafu walimgomea asife na Mungu akamtendea.
Huko mbele ndio alianza kusikia maumivu ya kifua na kujitibisha. Tokea hapo hajawahi Rudi kwenye huo mji akahamisha na familia yake jumla. Naunga mkono hoja ila tu ibada za makaburini ni dhambi kwa Mungu hasa kuwaomba wafu.
 
Eti Yesu kafa kwa mapambano na shetani na kamfunga kuzimu lakini mtu akiua wanasema kazi y’a shetani 😹😹😹

Shetani si alifungwa na funguo kapokonywa?!! 🥹
Hahahaha , tunawazoom tu walokole wa buza🤣🤣
 
Miongo balaa..
Kwanza watuambie watoto wa Adamu kina kaini waliwaoa kina nani? Ikiwa wao ndio uzao wa kwanza halafu madume 😹😹😹
Lamo jembe langu ,unaenda mbali waulize maswali ya kijinga tu hawa ni wale wafuasi wa yule nabii wa buza 🤣🤣
 
Sambamba na kutembelea sehemu walipo lazwa wapendwa wetu tutembelee pia wagonjwa hospital wazee yatima na wote wenye kuhitaji, wao wanahitaji kutembelewa zaidi kuliko walio lala, baraka zipatikazo unaweza kuzielekeza ziwe faida kwao walio tangulia au ziwe faida kwa walio waacha hapa duniani
 
Back
Top Bottom