Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kuna kauli za kipuuzi zimetolewa na baadhi ya watu eti mtu akipiga kura aondoke, asishuhudie hatua nyingine, eti aende nyumbani asubirie kuambiwa nani ameshinda uchaguzi! Wengine wakathubutu hata kusema eti baada ya kupiga kura, wananchi wasipoteze muda, waende wakafanye kazi! Yaani leo ndiyo tuone kuwa mpiga kura kushiriki na kushuhudia hatua zote za upigaji kura ni kupoteza muda, wakati hatujawahi kuumizwa na muda unaopotea kusubiria misafara mirefu ya watawala mabarabarani wanapopita? Kuna wakati watu wanasimamishwa hata masaa 4!! Mbona hatuumizwi na muda tunaopoteza kusikiliza hotuba, tena kwa kusomba watu kwa maelfu kwenda kuwashangilia watawala, watu huwa wanasombwa mkoa mzima, na mara nyingine mpaka mikoa ya jirani. Hawa hawapotezi masaa bali ni idadi siku kuanzia 2 hadi 3.
Kanuni ya efficieny and productivity ni kuwa ukifanya tendo lolote lile lazima ufuatilie mpaka mwisho, na hatimaye ushuhudie matokeo ili ujue kama umefanikiwa au umeshindwa, na uone wapi panahitaji marekebisho.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa kiongozi wa timu ya waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi wa Nigeria, aliporudi alisifua sana namna uchaguzi ule ulivyofanyika kule Nigeria, kwa uwazi na weledi. Na moja ya mambo aliyoyasifia ni kuwa baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika, zoezi la kuhesabu kura lilifanyika hadharani. Kura inanyanyuliwa juu inaoneshwa kwa wananchi na mawakala, kisha inawekwa kwenye kapu la mgombea husika.
Sasa hawa wanaotoa kauli kuwa kusubiria zoezi la kuhesabu kura ni kupoteza muda, ina maana haya mataifa yanayohamasisha wapiga kura kuwepo kushuhudia zoezi la upigaji kura toka mwanzo hadi mwisho, wote wanapoteza muda? Hawa wanaotoa kauli hizi za hovyo, ambazo bila shaka zina dhamira chafu, kuna siku nadhani watawaambia wananchi wasiende kupiga kura, kwa sababu kwa kufanya hivyo, wanapoteza muda, na hivyo kuna watu wamewateua watafanya hiyo kazi badala yao!
Tusikubali kutengeneza mazingira ya kutiliana mashaka. Wacha wananchi washuhudie matukio yote, hatua zote, mpaka kutangaza matokeo ya upigaji kura. Ni haki yao. Hiyo inaleta uwazi, inaondoa malalamiko, inatengeneza mazingira ya amani.
Anayefukuza au kutaka watu wasishuhudie hatua yoyote katika zoezi la upigaji kura, huyo ni wa kupuuzwa, hana maana wala msaada kwa Taifa, ana dhamira chafu. Hawa wachafu wenye dhamira chafu, tusiwape nafasi.