Ukipita Ubungo Flyover lazima umkumbuke Hayati Magufuli

Wajinga ndio mliwao.
Ujinga ni kutoelewa. Ubungo Flyover ilifadhiliwa na World Bank wakati wa Kikwete, na design ya ujenzi wake wakati wa Kikwete.
Magufuli alikuta kila kitu kimetayarishwa.
Kwanini Kikwete hakuitekeleza muhula wake wa Kwanza au wapili .
 
Mawazo ya watanzania wengi ni kujipeg kimaendeleo na kiongozi fulani tu.
Uongozi wa Rais nii bipindi viwili vya miaka mitano mitano.
Rais na serikali yake hailali kipindi cha pili cha uongozi na inaendelea na mipango endelevu ya miaka 25.
We should not restrict our thinking kwa kiongozi mmoja.
 
Jina la John Pombe Magufuli limejikita katika historia ya Tanzania kama kiongozi mwenye maono na utendaji wa kasi. Moja ya alama kubwa za uongozi wake ni Ubungo Flyover, daraja ambalo limebadilisha mandhari na mtiririko wa usafiri katika jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya ujenzi wa daraja hili, eneo la Ubungo lilikuwa maarufu kwa msongamano wa magari. Safari za kwenda na kutoka katikati ya jiji zilichukua muda mrefu, na hali hii iliathiri sana shughuli za kiuchumi na kijamii. Watu walikuwa wakipoteza muda mwingi barabarani, hali ambayo ilisababisha hasara kubwa ya kiuchumi.

Magufuli, akiwa rais wa Tanzania, aliona umuhimu wa kuboresha miundombinu kama sehemu ya mkakati wake wa kukuza uchumi. Ndipo alipoanzisha mradi wa ujenzi wa Ubungo Flyover. Ujenzi wa daraja hili haukuwa rahisi. Kulikuwa na changamoto nyingi, ikiwemo uhamishaji wa makazi na biashara zilizokuwa kandokando ya barabara. Lakini kwa maono yake thabiti na ufuatiliaji wa karibu, daraja lilijengwa kwa wakati na kwa viwango vya hali ya juu.

Sasa, unapopita Ubungo Flyover, unakutana na mtiririko mzuri wa magari, mabasi na malori. Muda wa safari umepungua kwa kiasi kikubwa, na watu wanaweza kusafiri kwa urahisi zaidi. Hali hii imechangia kupunguza msongo wa akili kwa watumiaji wa barabara na kuongeza ufanisi katika biashara na shughuli za kila siku.

Kila mara unapopita Ubungo Flyover, ni vigumu kutopata mawazo ya John Pombe Magufuli. Uthubutu wake, maono yake, na kazi yake ya bidii vimeacha alama isiyofutika katika historia ya Tanzania. Daraja hili sio tu njia ya kupita magari, bali pia ni kumbukumbu ya kiongozi ambaye alifanya kazi kwa bidii kuboresha maisha ya Watanzania. Ni ushuhuda wa jinsi kiongozi mmoja anaweza kubadilisha nchi kwa maono na utendaji wa dhati.
Hata NISIPOPITA darajani namkumbuka Magufuli tu.
Kwani Iddi Amini na Mobutu hawakumbukwi? Au Adolph Hitler na Benito Mussolini hawakumbukwi?

Suala unakumbukwa kwa kitu gani. Mimi nitamkumbuka Magufuli kwa kujenga Airport kijijini kwake na sasa imebaki useless kama Gbadolite ya Mobutu. Nitamkumbuka pia kwa kutuma kikosi cha Makonda kwenda kumshambulia Tundu Lissu.

Na nyie wajinga mna yenu ya kumkumbuka shujaa wenu
 
Bwawa la Umeme la Nyerere, SGR, Kuhamisha serikali kwenda Dodoma, Daraja la Busisi urefu wa karibu kilometer 4, Ikulu ya Dodoma. Hivi vitu VYENYE MASHIKO vitamfanya akumbukukwe milele!
Ameacha wizi wa Tsh 2.4 Trilion, chuki dhidi ya upinzani, ubaguzi wa maendeleo kwa kupendelea Chato, umalaya kwa akina Jokate na Kairuki, matusi kwenye majukwaa, kuropoka, ubishi wa Corona mpaka imemuua, uuaji wa akina Ben Saanane na Azory Gwanda, utekaji wa akina MoDewji, maonezi kwa akina Eric Kabendera na Tito Magoti na dharau kwa wanawake tu.

Atakumbukwa kwa UDIKTETA, kukandamiza Demokrasia, Wizi wa uchaguzi Serikali za Mitaa 2019, wizi wa kura uchaguzi Mkuu 2020, kuvunja Katiba, kudhibiti Bunge na kuitishia Mahakama. Vilevile kuminya uhuru wa kujieleza na kuitishia vyombo vya habari.

Nani atanikamata leo nikisema Magufuli alikuwa muuaji? Hakuna kwa vile Rais SSH anakubali kukosolewa kwa misingi ya Sheria.
 
Tutakukumbuka daima milele🙏🙏
1693938687100.jpg
 
Mawazo ya watanzania wengi ni kujipeg kimaendeleo na kiongozi fulani tu.
Uongozi wa Rais nii bipindi viwili vya miaka mitano mitano.
Rais na serikali yake hailali kipindi cha pili cha uongozi na inaendelea na mipango endelevu ya miaka 25.
We should not restrict our thinking kwa kiongozi mmoja.
Kuna Msemo siku njema huonekana Asubuhi sio usiku wa kiza ndio mtazamo wangu, ingekuwa kama wengine mihula 2 na hatujaona kitu Hadi usiku, sijui ingekuaje Kwa Magufuli wa muhula moja.
 
Bwawa la Umeme la Nyerere, SGR, Kuhamisha serikali kwenda Dodoma, Daraja la Busisi urefu wa karibu kilometer 4, Ikulu ya Dodoma. Hivi vitu VYENYE MASHIKO vitamfanya akumbukukwe milele!
Kuna suala zima la gharama za kuhamia Dodoma kutowekwa wazi, matumizi ya leo kazi inafanyika Dar kesho inahamia Dodoma ni makubwa na hayawekwi wazi.
 
Jina la John Pombe Magufuli limejikita katika historia ya Tanzania kama kiongozi mwenye maono na utendaji wa kasi. Moja ya alama kubwa za uongozi wake ni Ubungo Flyover, daraja ambalo limebadilisha mandhari na mtiririko wa usafiri katika jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya ujenzi wa daraja hili, eneo la Ubungo lilikuwa maarufu kwa msongamano wa magari. Safari za kwenda na kutoka katikati ya jiji zilichukua muda mrefu, na hali hii iliathiri sana shughuli za kiuchumi na kijamii. Watu walikuwa wakipoteza muda mwingi barabarani, hali ambayo ilisababisha hasara kubwa ya kiuchumi.

Magufuli, akiwa rais wa Tanzania, aliona umuhimu wa kuboresha miundombinu kama sehemu ya mkakati wake wa kukuza uchumi. Ndipo alipoanzisha mradi wa ujenzi wa Ubungo Flyover. Ujenzi wa daraja hili haukuwa rahisi. Kulikuwa na changamoto nyingi, ikiwemo uhamishaji wa makazi na biashara zilizokuwa kandokando ya barabara. Lakini kwa maono yake thabiti na ufuatiliaji wa karibu, daraja lilijengwa kwa wakati na kwa viwango vya hali ya juu.

Sasa, unapopita Ubungo Flyover, unakutana na mtiririko mzuri wa magari, mabasi na malori. Muda wa safari umepungua kwa kiasi kikubwa, na watu wanaweza kusafiri kwa urahisi zaidi. Hali hii imechangia kupunguza msongo wa akili kwa watumiaji wa barabara na kuongeza ufanisi katika biashara na shughuli za kila siku.

Kila mara unapopita Ubungo Flyover, ni vigumu kutopata mawazo ya John Pombe Magufuli. Uthubutu wake, maono yake, na kazi yake ya bidii vimeacha alama isiyofutika katika historia ya Tanzania. Daraja hili sio tu njia ya kupita magari, bali pia ni kumbukumbu ya kiongozi ambaye alifanya kazi kwa bidii kuboresha maisha ya Watanzania. Ni ushuhuda wa jinsi kiongozi mmoja anaweza kubadilisha nchi kwa maono na utendaji wa dhati.
Labda wewe ndio unamkumbuka sio wote
 
Magufuli, akiwa rais wa Tanzania, aliona umuhimu wa kuboresha miundombinu kama sehemu ya mkakati wake wa kukuza uchumi. Ndipo alipoanzisha mradi wa ujenzi wa Ubungo Flyover. Ujenzi wa daraja hili haukuwa rahisi. Kulikuwa na changamoto nyingi, ikiwemo uhamishaji wa makazi na biashara zilizokuwa kandokando ya barabara. Lakini kwa maono yake thabiti na ufuatiliaji wa karibu, daraja lilijengwa kwa wakati na kwa viwango vya hali ya juu.
Mkuu wewe ni mtu makini sana so nimeshangaa kidogo unaposema JPM ALIANZISHA..... mie nachojua DMDP enzi za JK ndio ilishachora ramani kwenye kipengele cha "decongestion dar es salaam". Humo ndani kulikua na barabara za mwendokasi, flyovers, stendi mpya n.k so labda ungesema JPM aliendeleza ramani za DMDP ambazo tayari zilishaanzwa telekezwa na JK kwa kujengwa mwendokasi na mabasi kuletwa.
 
Sawa, hongera kwake.

Nikiwa sjna hata chembe ya wivu na unafiki na uzandiki; binafsi napeleka kongole nyingi tu pia kwa jk na timu yake maana ndo waasisi wa hivyo vitu. Upimaji wa sehemu nyingi pale dar ulifanyika nikiwa naona hivi kwa macho yangu.
Waliasisi afu wakafanya Nini? Jk had 10 years on his name!!! Siasa za ahadi hatutaki tunataka Kuona matokeo, hapo ndo jpm alipowapiga gap hao watoto wa mjini, haya wanasema mama kafungua nchi, wakati tunashindwa kuagiza hata vitu vya Dola 10000 tu nje, hakuna Dola, kupata dola ishakua kama Moja ya majukumu yetu ya kila siku
 
Unataka kuagiza nini nje cja Dolla 10,000 tukupe ushauri?
 
Back
Top Bottom