KERO Ukipoteza au ukitaka kurekebisha cheti chako cha Chuo cha Stella Maris (Tawi la SAUT - Mtwara) ni ngumu kufanikiwa

KERO Ukipoteza au ukitaka kurekebisha cheti chako cha Chuo cha Stella Maris (Tawi la SAUT - Mtwara) ni ngumu kufanikiwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Huku kwetu Mtwara, kuna changamoto inayowakuta Wanafunzi wa Chuo cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) Tawi la Mtwara linalojulikana kwa jina la Stella Maris Mtwara University College (STEMMUCO) kutopewa vyeti vyao tena kama vilipotea au inapotokea vina marekebisho.

Baadhi ya wahitimu wengine hawapati cheti kabisa ila wanaonekana wamemaliza, shida hii inasababisha vijana wengi kukosa ajira kwa kushindwa kuambatanisha vyeti vyao.

Hili swala ni la muda mrefu kila siku ukienda kufuatilia wanasema vyeti vinaandaliwa Main Campus Mwanza, unaandikishwa barua ila kila mwaka ukienda kuulizia wanasema wamevisahau Mwanza jambo ambalo lina utata.

Mtu haudaiwi hata mia na una uhakika ulihitimu lakini changamoto ni wao kukupa cheti.

Kinachouma zaidi ni kuwa ikitokea umehitimu lakini ukawa unadaiwa hata kama ni buku, hupati cheti, mimi ni mmoja kati ya waathirika wa tabia waliyonayo ya kuzungusha wahitimu.
 
Back
Top Bottom