Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Yaani kama ulitoka nje ukashuka airport Dar miaka 8 iliyopita, ukashuka miaka mitano iliyopita na ukashuka leo, unakutana na barabara ni lami siyo lami, vumbi tupu, makorongo matupu, mitaro ya waziwazi iliyojaa maji machafu, yaani kanchi kamechoka kamechoka kwelikweli. Hivi nyie watawala mnaoshinda kwenye ndege kila kukicha mnnaenda kwenye nchi za watu huwa hamuoni huko kwa wenzenu kukoje?

Yaani just imagine, barabara ya mwanzo ambayo wageni wanapita kabla hawajaenda popote nchini wanakutana na kituko cha barabara ile. First impression inayopatikana hapo ni ya kanchi masikini ka watu masikini, ka viongozi hopeless!

Yaani hako kabarabara kako hivyohivyo miaka nenda rudi pachovu choka mbaya, yaani vagalanti hovyohovyo.

Nyie watawala mnatutia aibu, mnajionaje fahari kuwa viongozi msioweza kudeal na issues ndogo namna hiyo kama hiyo ya kuipa nchi "reception" ya maana?

Kwa kweli aibu naona mimi.

Miviongozi kazi kujilimbikizia mali, kutwa kucha kwenye ndege, misafara ya mamia ya magari, lakini barabara tu ya airport wanayopita daily kwenda huko nje ya nchi kuuza sura imewashinda!. Sijui hii mijitu ikoje?

Kila siku ukipita maendo hayo unakutana na miradi uchwara as if wanajenga, lakini miaka yote huo ujenzi huwa hauishi, ni magumashi, hakuna lolote la maana linaloonekana!. Yaani choka mbaya choka mbaya, hovyo hovyo kabisa!.

Nyie viongozi wa nchi hii badilikeni. Incompentency yenu ndo inatufanya sisi huko duniani tuonekane kama nyani tu. Nchi zina marasilimali kibao halafu unakutana na kinchi kimechokaaa. Hii inakuwaje.

Yaani unapita barabarabani pembeni unakutana na mamitaro makubwaaa hayajafunikwa ambayo kwanza ukifuatilia vizuri hayana exit ya mitoni wala sewage system yoyote ya maana, yaani yapo ceremonial tu.

Mamitaro makubwa hayajafunikiwa na yamekaa kama mahandaki ya vita kuu ya kwanza ya dunia. Hivi hawa wenye dhamana ya utawala wakienda huko kwa wenzetu wanajifunza chochote kweli?.

Achilia mbali hilo. Ukishuka airport njiani unakutana na wabongo wamechoka mbaya, hali ngumu, wamekonda, wameweka vimizigo vyao barabarani masikini wanahustle. Hii iko hivyo miaka nenda rudi. Wakati huo kuna watu wanaitafuna nchi hii kwa kula na kusaza. Ni lini wansnchi wataanza kula matunda na mema ya nchi?. Watawala wanawaza siasa tu, siasa tu.


Pia soma
- Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Kituko kipo Dodoma kuelekea ikulu

Kama umetembelea nchi za wenzetu ukaona ikulu zao zilivyozungukwa na mitaa safi majengo mazuri, na barabara za kiwango cha juu kabisa alafu ukaja Tanzania Dodoma uende uelekeo wa Ikulu unaweza dhani uko karne ya 18 huko.

Ikulu yetu imezungukwa na vijumba vya hovyo, havijajengwa vizuri, kuna maeneo hadi kuna vinyumba vya udongo, vumbi la kufa mtu hadi unaweza sema sie ni wanyama sio binadamu.
 
Halafu sasa ukifika airport jinsi maafisa usalama walivyojazana ktk nguo za kiraia, yaani wapowapo tu wamezagaa zagaa utadhani bado tupo enzi zile za ushushushu wa mwaka 47
 
Back
Top Bottom