Nilishasema yote maisha tu.
Najifikiria na mimi nisingezaliwa familia fulani kwa bahati tu chances are ningekuwa na maisha tofauti sana na yasiyo na relative privileges nyingi sana nilizo nazo.
Imagine unaishi kwenye hizo nyumba za mabati chakavu, halafu kuna mijamaa iko Marekani inasema maneno kama haijawahi kukaa Tanzania.
Yani ushapigwa na maisha, halafu unaona unazodolewa na wabongo wenzako waliokimbikia dunia ambayo huna hata nafasi ya kufika.
Kuna siku nilikuwa nasema Watanzania hawapendi kusoma, nikasema mimi nilijenga utamaduni wa kusoma nika ji challenge kusoma mambo mengi sana, nikapitia Tambaza Library, Tanganyika Library, USIS Library (Peugeot House), British Council, mpaka Goethe Institute na Alliance Francaise. Watu wengi hawasomi.
Jamaa mmoja akaniambia hata kuzijua hizo sehemu ni privilege, hata kupenda kusoma mara nyingi kwenu kutakuwa na msingi wa kupenda kusoma, wazazi waliosoma na wenye maktaba ya nyumbani wana nafasi kubwa ya kuwapa msingi mzuri watoto wao kupenda kusoma.
Kwamba maisha yetu mara nyingi yanafuata mkondo fulani ambao umewekwa kwa bahati, si kwa juhudi, ingawa sehemu ya juhudi oia ipo.
Kwa hivyo, tunaposema habari za mapungufu ya nyumbani, tuwe waangalifu kutowakwaza wenzetu ambao hawajapata nafasi ya kutoka, bila kusahau kuweka msisitizo kwenye kufanya mazungumzo ya kubadilisha mambo yawe mazuri zaidi.