Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Barabara ya kwenda Julius Nyerere airport (kakipande kadogo) sijui ina miaka mingapi haiishi. Na ile ndio reception ya nchi yetu. Wageni wote wakitua tu wanapita hapo. Viongozi wote wa nchi including Rais anapita hapo mara kwa mara. Sijui kile kipande kinashindikana nini?! Kwa kweli tunatia aibu!
Sahihi hiyo barabara huwa inajengwa tu miaka yote, Itakuwa kuna namna mkandarasi na watu wake wanafaidika na huo ucheleweshwaji,
 
Huu uzi ungekua unaambatana na picha ingependeza zaidi,
Huenda wahusika wangeona na kuchukua hatua kwa baadhi ya issue.
 
Ningesema mimi baadhi ya watu wangeona nina madharau! Nafurahi kuona si mimi tu ninayekereka na hiyo hali!

IMG_1115.jpeg


IMG_1117.jpeg
 
Yaani kama ulitoka nje ukashuka airport Dar miaka 8 iliyopita, ukashuka miaka mitano iliyopita na ukashuka leo, unakutana na barabara ni lami siyo lami, vumbi tupu, makorongo matupu, mitaro ya waziwazi iliyojaa maji machafu, yaani kanchi kamechoka kamechoka kwelikweli. Hivi nyie watawala mnaoshinda kwenye ndege kila kukicha u.

Pia soma
- Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Ndio hali yenyewe laana inaisumbua nchi.
 
Kanchi kamechoka Mbaya.

Sijui watawala wanajisikiaje wanavyotumbua mikodi ya wabongo huku Kanchi kakiwa hoi
Kule Arusha kitovu cha utalii wageni na wenyeji wanasongamana kwenye barabara inayopita soko la Kilombero.
Pananuka harufu ya vinyesi na siku ukiwa na bahati unaviona live kwenye mitaro kushoto na kulia!
Dar harufu ya uozo na vinyesi kwenye mitaro iliyoziba ni kawaida maeneo mengi! Sasa ongezea hilo joto na mijasho ya watu.. .. Unapigwa uvundo mmoja matata ukirudi room unaugua!

Aibu sana!
 
Mimi hayo mabati yenye kutu tu!

Dar es salaam ingekuwa na nyumba za maghorofa ya ghorofa 4 mpaka 5 kwa sehemu kubwa, ingechukua sehemu kama robo ya mji wa sasa.
Yes, they are eyesores.

But, what are people to do? Hali ya uchumi ni mbaya siku zote halafu inakuwa compounded na jamii kwa ujumla kutokupenda vitu vizuri.

Kuna mambo mengi tu ambayo hayahitaji hela nyingi lakini utashangaa kwa nini hayafanyiki!
 
Back
Top Bottom