Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Yaani huhitaji kujua kuwa hii nchi haina uongozi. Just shuka na ndege tu pita barabara kuu , kisha utaona haka ka nchi kalivyofanywa useless hopeless kabisa kwa uongozi mbovu usiojua unatakiwa kufanya nini.

Hivi ukiwa kiongozi halafu unaongoza kanchi kachafu, kamechoka namna hii, kana watu wamekondakonda halafu dhaifu dhaifu, unajiona ufahari gani kwa mfano?
Tuna matatizo mengi sana lakini kubwa NJ kukosa mipango sahihi,watu sahihi wa kutekeza na jamii kukubaliana kwenda kwa.njia hiyo thus why hatutoi nafasi Kwa watu wenye akili kushika hatamu.

Hii jamii yetu imelelewa vibaya ndio matokeo yake hayo Sasa.
 
Sometimes unajiuliza kuna maana gani ya wewe kua na jumba kubwa la ghorofa mithiri ya ikulu ya chamwino na ukitoka nje tu ya geti lako unakutana na barabara ya vumbu imejaa viraka na mashimo kila kona kisa tu wewe umeamua kubinafsisha hela za mradi?

Hospitali poor
Shule poor


Kila kitu poor, lakini wewe uko na hela umeficha uswis sijui UAE, ina kua na maana gani?

Haya yote ni matokeo ya siasa za kifedhuri za Tanzania. Mfumo wetu haujulikani ni ubepari, ubeberu au umwinyi.
 
Niliona Kwenye tv mayor wa mji Mdogo wa California analia machozi Kwasababu tu nyumba na mali za raia wake anaowaongoza zimewaka moto nikagundua Siri ya mafanikio ya nchi za ngozi nyeupe ni uzalendo !
Sijui uzalendo Huwa unapatikanaje lakini pia kati ya matatizo mengi ya jamii yetu ni ubinafsi , yaani jambo la kunufaisha Umma sio kipaombele kushinda jambo binafsi.
 
Huko mbali, ukishuka tu DSM pale pale airport unakutana na harufu moja ya ajabu. Mji mzima unanuka.

Miviongozi inaona fahari kuendesha msafara wa v8 kwenye mashimo badala ya kurekebisha barabara. Inaenda nje kupiga picha tu na kushangaa haijifunzi chochote kile.
Nilienda Mwanza Airport Road yaani Jiji Zima linanuka.shombo ya Samaki 😆😆😆😆
 
Eti Kanchi kamechoka😁
Nyiee
Hii Nchi inatia aibu,yaani Halmayzimwshindwa kuajiri kampuni za usafi ili Kusafisha mitaro ,Barabara nk.

Lakini pia ilitakiwa kuweka na sheria kwamba Kila mtu ahakikishe mbele ya nyumba au duka lake kiwanja au mtaro unakuwa safi na hatua Kali zichukuliwe mbona pangekuwa safi ila Kwa kuwa hatuna utaratibu wa kujali na kuthamini ndio maana tunaona Bora liende.
 
Lucas ndio mwenye dhamana ya kujenga hii Nchi na nyie mnakuwa mnafanya nini?

Kwanza mipango ya Nchi hii Huwa haiko coercive yaani ni Bora liende.Mfano unakuta mtu anajua hii ni Barabara anatakiwa asimike Bomba za maji ila hafuati usahihi unatakiwa ndio maana unakuta mradi ukianzanaanza kuingia gharama zingine za kuhamishwa miundombinu ambayo ilitakiwa kuwa imewekwa sehemu inapostahili ila hawakufanya hivyo.
Wakati huyo mtu anafanya mipango ya kujenga, anaweka tofali, anachimba msingi, anaanza ujenzi..serikali ya mtaa/kijiji inakuwa wapi?

Hata hivyo, kwa nini kila.mara serikali inasubiri watu waanzishe shughuli za kiuchumi ndipo nayo ijiingize?

Hii nchi nadhani ina ombwe la uongozi, viongozi ni taswira tu ya vile sisi tulivyo, hakuna wa kumlaumu mwenzake coz hata mimi/wewe tukipewa nafasi ya kuongoza tutafanya same same...we're indifferent.
 
Michael Jackson alikuja Dar akawa anajishika pua, tukaona huyu anaringa tu.

Kumbe ike harufu tulikuwa tumeizoea tu.
Nakumbuka niko kituo cha Palm Beach nasubiri chai maharage “Kabibii” niende home mara huyo Michael Jackson anapita katoa kichwa kwenye open roof amevaa mask yake na bado kaziba mdomo na mkono 😀
 
Wewe jamaa unazingua kwaiyo kweli mtu akitoka AIRPORT anakutana na vumbi your just wale watu waliotokea familia za kimaskini halafu wakapata ela MWALIMU NYERERE AIRPORT iko vizuri acha ujinga na upuuzi wako
 
Barabara ya kwenda Julius Nyerere airport (kakipande kadogo) sijui ina miaka mingapi haiishi. Na ile ndio reception ya nchi yetu. Wageni wote wakitua tu wanapita hapo. Viongozi wote wa nchi including Rais anapita hapo mara kwa mara. Sijui kile kipande kinashindikana nini?! Kwa kweli tunatia aibu!
 
Tanzania hii ni Nchi ya shaghalabaghala ambayo jamii yake haijali,haithamini Wala haijitambui.

Swala sio viongozi Baki aina ya jamii ambayo haiana Ustaarabu ndio matokeo yake haya sasa.

Athari za ujamaa na uswahili zitatutafuna sana.

Nilisikitika kuona Jamaa mmja wa Burundi anajenga apartments nzuri sana kule Bujumbura nikalinganisha na vile vijumba vya Iyumbu Dom nikajua tuna Nchi ya hovyo sana.
Hilo suala la jamii watu wengi hawalioni au wanalifumbia macho.

Watu watalaumu viongozi, watalaumu katiba, lakini ni wachache sana watakubali kwamba viongozi wanatoka kwenye jamii na katiba (ambayo hata hii ya sasa mazuri yake mengi hatuyafuati) imeandikwa na watu.
 
1722378184711.png
 
Wewe jamaa unazingua kwaiyo kweli mtu akitoka AIRPORT anakutana na vumbi your just wale watu waliotokea familia za kimaskini halafu wakapata ela MWALIMU NYERERE AIRPORT iko vizuri acha ujinga na upuuzi wako
Mkuu,

Kuna tofauti kubwa sana. Kuna jamaa mmoja alirudi kutoka New York akatukuta maskani alikuwa anatuambia hizi habari

Alikuwa anasema akishuka kutoka New York anakutana na jua kali, majumba yamepauka, barabara zenye mashimo kibao, nyuso za watu zenye maumivu makubwa.

Sisi tulikuwa tunaona huyu jamaa anatuletea shobo zake za Marekani tu.

Tulipokua wakubwa na kuanza vyuo Marekani na sisi tukaelewa alikuwa anaongelea nini.
 
Back
Top Bottom