Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Jiji la Dar es salaam linajengwa kila siku bila mpangilio, hapa leo panajengwa hivi kesho panabomolewa panajengwa vile.

Wakati linajengwa lile Daraja pale Tazara hawakujua kuna mwendo kasi kuelekea airport.
Unajenga mwendo kasi unaacha barabara za magari nyembamba, kesho ukihitaji express train unajikuta huna eneo, baada yakujenga express electric train kutoka airport to city center ili umalize kabisa unaanza na mwendo kasi ili miaka kumi baadaye urudi tena kwenye electric train.

Ile barabara ya kimara ilijengwa mwendokasi utafikiri hatukuwaza kama tunahitaji six lane muda sio mfupi, tukavunja.

Vuruguvurugu tu.
 
Yule jamaa watu wengi hatumpendi kwa sababu hakuona haya kuusema ukweli, miaka sitini ya uhuru tumefanya Nini Cha maana.....!
Ni kweli kabisa, Rais Pieter Botha Kamwe hakuwa mtu mnafiki katika kusema ukweli mchungu, hususani kuhusiana na Watu Weusi. Kamwe alikuwa hatafuni maneno linapokuja suala la kuwasema Watu Weusi na Mapungufu yao makubwa.
 
Yaani kama ulitoka nje ukashuka airport Dar miaka 8 iliyopita, ukashuka miaka mitano iliyopita na ukashuka leo, unakutana na barabara ni lami siyo lami, vumbi tupu, makorongo matupu, mitaro ya waziwazi iliyojaa maji machafu, yaani kanchi kamechoka kamechoka kwelikweli. Hivi nyie watawala mnaoshinda kwenye ndege kila kukicha mnnaenda kwenye nchi za watu huwa hamuoni huko kwa wenzenu kukoje?

Yaani just imagine, barabara ya mwanzo ambayo wageni wanapita kabla hawajaenda popote nchini wanakutana na kituko cha barabara ile. First impression inayopatikana hapo ni ya kanchi masikini ka watu masikini, ka viongozi hopeless!

Yaani hako kabarabara kako hivyohivyo miaka nenda rudi pachovu choka mbaya, yaani vagalanti hovyohovyo.

Nyie watawala mnatutia aibu, mnajionaje fahari kuwa viongozi msioweza kudeal na issues ndogo namna hiyo kama hiyo ya kuipa nchi "reception" ya maana?

Kwa kweli aibu naona mimi.

Miviongozi kazi kujilimbikizia mali, kutwa kucha kwenye ndege, misafara ya mamia ya magari, lakini barabara tu ya airport wanayopita daily kwenda huko nje ya nchi kuuza sura imewashinda!. Sijui hii mijitu ikoje?

Kila siku ukipita maendo hayo unakutana na miradi uchwara as if wanajenga, lakini miaka yote huo ujenzi huwa hauishi, ni magumashi, hakuna lolote la maana linaloonekana!. Yaani choka mbaya choka mbaya, hovyo hovyo kabisa!.

Nyie viongozi wa nchi hii badilikeni. Incompentency yenu ndo inatufanya sisi huko duniani tuonekane kama nyani tu. Nchi zina marasilimali kibao halafu unakutana na kinchi kimechokaaa. Hii inakuwaje.

Yaani unapita barabarabani pembeni unakutana na mamitaro makubwaaa hayajafunikwa ambayo kwanza ukifuatilia vizuri hayana exit ya mitoni wala sewage system yoyote ya maana, yaani yapo ceremonial tu.

Mamitaro makubwa hayajafunikiwa na yamekaa kama mahandaki ya vita kuu ya kwanza ya dunia. Hivi hawa wenye dhamana ya utawala wakienda huko kwa wenzetu wanajifunza chochote kweli?.

Achilia mbali hilo. Ukishuka airport njiani unakutana na wabongo wamechoka mbaya, hali ngumu, wamekonda, wameweka vimizigo vyao barabarani masikini wanahustle. Hii iko hivyo miaka nenda rudi. Wakati huo kuna watu wanaitafuna nchi hii kwa kula na kusaza. Ni lini wansnchi wataanza kula matunda na mema ya nchi?. Watawala wanawaza siasa tu, siasa tu.

Pia soma
- Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Wengine ni Hawa hapa ambao mnawajengea Sgr 😂😂👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C-GXyjftLsB/?igsh=MWszb3czdjNzM2dmcw==
 
Yes, they are eyesores.

But, what are people to do? Hali ya uchumi ni mbaya siku zote halafu inakuwa compounded na jamii kwa ujumla kutokupenda vitu vizuri.

Kuna mambo mengi tu ambayo hayahitaji hela nyingi lakini utashangaa kwa nini hayafanyiki!
Nilishasema yote maisha tu.

Najifikiria na mimi nisingezaliwa familia fulani kwa bahati tu chances are ningekuwa na maisha tofauti sana na yasiyo na relative privileges nyingi sana nilizo nazo.

Imagine unaishi kwenye hizo nyumba za mabati chakavu, halafu kuna mijamaa iko Marekani inasema maneno kama haijawahi kukaa Tanzania.

Yani ushapigwa na maisha, halafu unaona unazodolewa na wabongo wenzako waliokimbikia dunia ambayo huna hata nafasi ya kufika.

Kuna siku nilikuwa nasema Watanzania hawapendi kusoma, nikasema mimi nilijenga utamaduni wa kusoma nika ji challenge kusoma mambo mengi sana, nikapitia Tambaza Library, Tanganyika Library, USIS Library (Peugeot House), British Council, mpaka Goethe Institute na Alliance Francaise. Watu wengi hawasomi.

Jamaa mmoja akaniambia hata kuzijua hizo sehemu ni privilege, hata kupenda kusoma mara nyingi kwenu kutakuwa na msingi wa kupenda kusoma, wazazi waliosoma na wenye maktaba ya nyumbani wana nafasi kubwa ya kuwapa msingi mzuri watoto wao kupenda kusoma.

Kwamba maisha yetu mara nyingi yanafuata mkondo fulani ambao umewekwa kwa bahati, si kwa juhudi, ingawa sehemu ya juhudi oia ipo.

Kwa hivyo, tunaposema habari za mapungufu ya nyumbani, tuwe waangalifu kutowakwaza wenzetu ambao hawajapata nafasi ya kutoka, bila kusahau kuweka msisitizo kwenye kufanya mazungumzo ya kubadilisha mambo yawe mazuri zaidi.
 
Yaani kama ulitoka nje ukashuka airport Dar miaka 8 iliyopita, ukashuka miaka mitano iliyopita na ukashuka leo, unakutana na barabara ni lami siyo lami, vumbi tupu, makorongo matupu, mitaro ya waziwazi iliyojaa maji machafu, yaani kanchi kamechoka kamechoka kwelikweli. Hivi nyie watawala mnaoshinda kwenye ndege kila kukicha mnnaenda kwenye nchi za watu huwa hamuoni huko kwa wenzenu kukoje?

Yaani just imagine, barabara ya mwanzo ambayo wageni wanapita kabla hawajaenda popote nchini wanakutana na kituko cha barabara ile. First impression inayopatikana hapo ni ya kanchi masikini ka watu masikini, ka viongozi hopeless!

Yaani hako kabarabara kako hivyohivyo miaka nenda rudi pachovu choka mbaya, yaani vagalanti hovyohovyo.

Nyie watawala mnatutia aibu, mnajionaje fahari kuwa viongozi msioweza kudeal na issues ndogo namna hiyo kama hiyo ya kuipa nchi "reception" ya maana?

Kwa kweli aibu naona mimi.

Miviongozi kazi kujilimbikizia mali, kutwa kucha kwenye ndege, misafara ya mamia ya magari, lakini barabara tu ya airport wanayopita daily kwenda huko nje ya nchi kuuza sura imewashinda!. Sijui hii mijitu ikoje?

Kila siku ukipita maendo hayo unakutana na miradi uchwara as if wanajenga, lakini miaka yote huo ujenzi huwa hauishi, ni magumashi, hakuna lolote la maana linaloonekana!. Yaani choka mbaya choka mbaya, hovyo hovyo kabisa!.

Nyie viongozi wa nchi hii badilikeni. Incompentency yenu ndo inatufanya sisi huko duniani tuonekane kama nyani tu. Nchi zina marasilimali kibao halafu unakutana na kinchi kimechokaaa. Hii inakuwaje.

Yaani unapita barabarabani pembeni unakutana na mamitaro makubwaaa hayajafunikwa ambayo kwanza ukifuatilia vizuri hayana exit ya mitoni wala sewage system yoyote ya maana, yaani yapo ceremonial tu.

Mamitaro makubwa hayajafunikiwa na yamekaa kama mahandaki ya vita kuu ya kwanza ya dunia. Hivi hawa wenye dhamana ya utawala wakienda huko kwa wenzetu wanajifunza chochote kweli?.

Achilia mbali hilo. Ukishuka airport njiani unakutana na wabongo wamechoka mbaya, hali ngumu, wamekonda, wameweka vimizigo vyao barabarani masikini wanahustle. Hii iko hivyo miaka nenda rudi. Wakati huo kuna watu wanaitafuna nchi hii kwa kula na kusaza. Ni lini wansnchi wataanza kula matunda na mema ya nchi?. Watawala wanawaza siasa tu, siasa tu.

Pia soma
- Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Maendeleo hayaji mara moja na ni utekelezaji wa vipaumbele vinavyowekwa kwenye ilani za uchaguzi.

Haiwezekani kwa mara moja tu tukawa tumeshatoka katika mabati yenye kutu, yapo mengi sana yenye kuhitaji kutekelezwa na pesa siku zote huwa hazitoshi kwa kuzilinganisha na wingi wa matumizi.
 
Jiji la Dar es salaam linajengwa kila siku bila mpangilio, hapa leo panajengwa hivi kesho panabomolewa panajengwa vile.

Wakati linajengwa lile Daraja pale Tazara hawakujua kuna mwendo kasi kuelekea airport.
Unajenga mwendo kasi unaacha barabara za magari nyembamba, kesho ukihitaji express train unajikuta huna eneo, baada yakujenga express electric train kutoka airport to city center ili umalize kabisa unaanza na mwendo kasi ili miaka kumi baadaye urudi tena kwenye electric train.

Ile barabara ya kimara ilijengwa mwendokasi utafikiri hatukuwaza kama tunahitaji six lane muda sio mfupi, tukavunja.

Vuruguvurugu tu.
Hii inakupa picha viongozi wetu wana akili fupi sana na miradi mingi ni ya upigaji
 
Nilishasema yote maisha tu.

Najifikiria na mimi nisingezaliwa familia fulani kwa bahati tu chances are ningekuwa na maisha tofauti sana na yasiyo na relative privileges nyingi sana nilizo nazo.

Imagine unaishi kwenye hizo nyumba za mabati chakavu, halafu kuna mijamaa iko Marekani inasema maneno kama haijawahi kukaa Tanzania.

Yani ushapigwa na maisha, halafu unaona unazodolewa na wabongo wenzako waliokimbikia dunia ambayo huna hata nafasi ya kufika.

Kuna siku nilikuwa nasema Watanzania hawapendi kusoma, nikasema mimi nilijenga utamaduni wa kusoma nika ji challenge kusoma mambo mengi sana, nikapitia Tambaza Library, Tanganyika Library, USIS Library (Peugeot House), British Council, mpaka Goethe Institute na Alliance Francaise. Watu wengi hawasomi.

Jamaa mmoja akaniambia hata kuzijua hizo sehemu ni privilege, hata kupenda kusoma mara nyingi kwenu kutakuwa na msingi wa kupenda kusoma, wazazi waliosoma na wenye maktaba ya nyumbani wana nafasi kubwa ya kuwapa msingi mzuri watoto wao kupenda kusoma.

Kwamba maisha yetu mara nyingi yanafuata mkondo fulani ambao umewekwa kwa bahati, si kwa juhudi, ingawa sehemu ya juhudi oia ipo.

Kwa hivyo, tunaposema habari za mapungufu ya nyumbani, tuwe waangalifu kutowakwaza wenzetu ambao hawajapata nafasi ya kutoka, bila kusahau kuweka msisitizo kwenye kufanya mazungumzo ya kubadilisha mambo yawe mazuri zaidi.
Hata huko US wanaopiga picha wanajali uzalendo. Nadra sana kuziona mitandaoni picha za watu wanaolala nje pembeni ya njia za watembea kwa miguu. Na wapo wengi sana wanaolala kwenye maboksi.

Zikija picha huku kwetu ni zile za maghorofa marefu ya miji mikubwa, Disney Land na sehemu nzuri nzuri.

Yapo mabadiliko mengi ya mandhari katika majiji yetu lakini kwa kutojipenda kwetu na kukosa uzalendo tunakuwa na wepesi wa kutafuta picha mbaya ambazo zinachangia katika kuwapa watu picha mbaya ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom