Ukisikia kua uyaone ndo haya sasa: Bhufakale dawa ya kuchelewa kufariki (kufa)

Ukisikia kua uyaone ndo haya sasa: Bhufakale dawa ya kuchelewa kufariki (kufa)

Bahati mbaya Bible siijui..kwa hiyo sina jibu
Uchawi upo mkuu na hili nililo lishuhudia lipo.

Mtu alikaa zaidi siku14 bila kula muda huo baadhi ya mwili wake umeanza haribika.

Kitendo Cha kutolewa kwake na kuhamishiwq pengine na akapata mwanga wa jua na kufa Bado nisiamini ni kwelii?

Maandiko yanashuhudia kuwa Musa alipotupa fimbo yake na kugeuka kuwa nyoka na wachawi wa misri walifanya hivo hivo.

Ndipo yule nyoka wa Musa akawla nyoka wote wa wa wachawi.


Hapo tunaona utofauti ulikuja kuzidiana nguvu tu lkn Kwa upande wa miujiza Ngoma ilikuwa droo sio Musa sio wachawi.

Naishia hapa
 
Hoja ni hii Kwa wastani binadamu asipo kula Wala kunywa anaweza ku survive Kwa muda Gani Hadi umauti kumkuta?
Kwahiyo hii dawa inachelewesha kufa kwa njaa tu? Na kwa muda gani?

Au hata ukipata ajali ukakatika kichwa utachelewa kufa pia?
 
Hilo jua ni la kwenye nyumba ya nyasi tu? Siku nyingine hapigwi na jua?
 
Hayo siyajui mkuu ninachojua ndo nilicho share na ninyi hapa.

Kilichobaki ni kuamini au kukut it's your own choice
Kwahiyo hii dawa inachelewesha kufa kwa njaa tu? Na kwa muda gani?

Au hata ukipata ajali ukakatika kichwa utachelewa kufa pia?
 
Alikuwa mgonjwa sana. Alikuwa hatoki Nje huduma zote alikuwa anapewa akiwa kitandan.

Nadhani masharti ya dawa ndo yalivo.

Kuna Babu yetu mdogo aliyebakia umri wanakadiria 94+

Pamoja na kumjengea nyumba kubwa ya kisasa m south hajawahi lala humo Huwa analala kwenye nyumba yake ya miti na nyasi mpaka Leo. Huwa tukimuuliza anasema nyumba za bati Zina kelele hasa mvua ikiwa inanyesha.

Sijui kama anasababu nyingine ya msingi kama hiyo.
Hilo jua ni la kwenye nyumba ya nyasi tu? Siku nyingine hapigwi na jua?
 
Kuna bibi mmoja alikua anaogopeka sana kijijini kwa uchawi, alipofikia hali hiyo ikabidi wajukuu zake waanze kumletea waganga wakumuua, maana waliezua nyasi akapigwa jua mpaka na mvua ikamnyeshea hafi tu.

Mganga wa kwanza alipoingia tu ndani, tukaanza kusikia analia ile kuja kutoka ameloa jasho mwili mzima hakusema kilichomtokea zaidi ya kubeba mizigo yake na kusepa.

Wapili na wa tatu nae hivyo hivyo, mpaka alivyo kuja wa nne ndiyo akafanikiwa, nae nafikiri alisaidiwa na style yake ya kuingia kinyunyume kama mchizi mox.
 
Pita kushuto huku unachechemea mkuu
Simple logic kuna haja gani ya kutokufa huku ukiishi ukiwa mzee kibogoyo, umejichokea , huna kumbukumbu na mali nyingi wakati wangetengeneza na ya kuzuia uzee kabisa ili uishi kwa starehe ukiwa kijana milele , hii ina prove uongo uongo mwingi na UJINGA ULIOKITHIRI
 
Nenda kamuhoji marehem mimi Sina majibu.😂😂

Ukute hapo ndo una miaka22+ yaani hata wewe hujijui umekulia mjini na unaishi mjini. Hizi code ni zetu waafrica halisi
Simple logic kuna haja gani ya kutokufa huku ukiishi ukiwa mzee kibogoyo, umejichokea , huna kumbukumbu na mali nyingi wakati wangetengeneza na ya kuzuia uzee kabisa ili uishi kwa starehe ukiwa kijana milele , hii ina prove uongo uongo mwingi na UJINGA ULIOKITHIRI
 
Sumple tu muingizeni ndani kisha mkokee moto kwa jiko la mkaa kisha fungeni milango na madirisha muacheni Babu wawatu apate joto kidogo kesho yake mfungulieni mtakuja kunishukuru mtakuta keshapona mda sana..
 
Habari za Leo mabibi na mabwana.

Mnamo 14/05/2024 tulimzika mzee mmoja kijijini kwetu jina (..)

Mzee yule alikuwa amemuoa shangazi yangu Mimi. Chanzo Cha kifo chake ni ugonjwa wa kisukari uliodumu Kwa muda mrefu.

Baada ya kuzunguka huku na huko na hospital mbalimbali kutafuta matibbu ya ugonjwa huu na kudanganywa na Kila aina ya wanatiba asilia kuwa wanaponesha.

Hatimae mzee huyu alizirudia tiba za hospital (vidonge).

Ikumbukwe mzee huyu kaugua kisukari zamani kidogo ni zaidi ya miaka 10 ana kisukari.

Hadi mwishoni mwa mwaka 2023 Hali yake ilizorota sana na kuandamwa na magonjwa mbalimbali.

Mapema mwezi wa kwanza mwaka huu walimpeleka sengerema mission na kupewa rufaa Hadi bungando.

Na walipofika pale wakakutana na bro yangu yupo hapo (Dr)

Baada ya vipimo kufanyika waliambiwa in,Figo nk havifanyi kazi Tena hivyo wakaambiwa warudi wasubiri lolote(kama mnavyojua kauli hii humanisha kifo)

Yule kaka akawaambia mlichoambiwa ni sahihi kuliko kusafirisha maiti ni Bora msafirisheni ingali Bado Yu hai.

Nifupishe kisa hiki

Mwezi wa pili baada kwenda kijijn nikaona ni Vyema na haki Nami nikamuone huyu mgonjwa.

Nikafika nikamkuta mgongwa anakula Kwa mrija ametibolewa hivyo uji unapita Kwa mrija na kukojoa pia anakojoa Kwa mirija.

Kwakweli Hali yake haikuwa nzuri Wala hakuna matumaini kabisa.

Daima ndg wa karibu walikuwa wanakaa hapo nyumbani wakisubiri Kila anaye Toka ndani awaambie lolote.

Niliondoka nikiwa najua kabisa Kwa Hali hii mzee wetu huyu siku3 hatoboi.

Mwezi wa 1 ukakata wa pili ukakata watatu na wanne pia ukaisha Ngoma bila bila.

Madaktari wenyewe walikuwa wanashangaa sana. Kila wanapokuja.

Ilifikia kipindi hata kula Hali Wala kunywa maji hanywi.

Lakini kufa hafi. Hadi tarehe 9/5/2024 Watoto wakakaa kikao wakasema jambo hili sio sawa jamani hii haiwezekani Wala hatujawahi ona.

Ndipo wakasema aitwe mmoja wa baba zao wakubwa kwenye ukoo wao nae ni mzee sana kwenye miaka 87+ Hivi.

Baada tu ya kufika pale wakamueleza Hali ILIVYO ndipo akawapa Siri hii..... ....

Akawaambia walichanjwa dawa inayoitwa "BHUFAKALE" Hii ni Kwa kisukuma tafsiri yake kufa zamani.

Ndipo wakaambiwa kuwa nendeni mkamtoe kwenye nyumba ya bati mwekeni kwenye nyumba ya nyasi mlazeni humo halafu mbomoeni (waezue zile nyasi juu ya paa)

Iwapo atapata mwanga wa jua tu(kivuli Cha jua) atakufa muda huohuo hatachukua muda na kama Hana hiyo dawa basi mtamrejesha kwenye nyumba ya bati.

Kweli baada ya kutoka huko hawakuchukua muda wakamtoa na kumuingiza jikoni maana ndo nyumba ya nyasi pekee ilikuwa imebakia pale.

Ilipofika saa 3 asubuhi ya tarehe 12 mzee akafariki ni baada tu ya kupata huo mwanga wa jua.

Hii ni ngumu kidogo kuamini wale wa Kwa mwamposa, Baraka, mzee wa upako, Malisa l, kiboko wa wachawi nk.

Mzee alikuwa mfugaji mkubwa sana.

Siku ya mazishi 14/5/2024

Nikabahatika kuonana na mzee mmoja wa makamo nikaanza ulizia hii imekaaje na Nini faida yake?

Aliniambia mengi lakini Kwa kifupi tu alisema kuwa

Wazee wa zamani walikuwa na Imani ya kwamba akiwa na hiyo dawa kwanza inaendana na Baraka na laana

Akikubariki amekubariki na utafanikiwa pia akikulaani wewe umelaanika yamkini hata ungeoga mafuta ya mwamposa Bado laana yake isingekutoka.

Pili akasema waliamini akichelewa kufa manake atakula mali yake vizuri Hadi anakufa kashabakiza kidogo tu.

Maana yeye anakuwa anajua kabisa kuwa huenda ugonjwa huu ndo utaniondoa ila Kwa sababu ya dawa hii niliyochanjiwa Wacha Nile Mali zangu.

Je ulikuwa unalijua hili mwana JF?

MWISHO.
Hii naijua hata Babu yangu walifanya hvo.
 
Back
Top Bottom