Ukisoma Degree ya Political Science (Sayansi ya siasa) unategemea kuajiriwa wapi bongo?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Hawa watu wanaosoma degree ya Political Science katika vyuo vya hapa Tanzania huwa wanaajiriwa wapi? Ni kazi gani mahususi ambazo zinahataji waliosomea political science tu?

Hii degree naona imekaa kimtego sana na kama haina mashiko kabisa kwa nchi kama ya Tanzania.
 
TANZANIA imeharibu maana ya university degree, imelazimisha degree kuwa too specific wakati degree ni general. Leo kuwa bank teller unahitajika kuwa na taaluma ya uhasibu ama mambo ya namna hiyo wakati ilitakiwa wote waliosoma social science na general science waifanye.

Kwenye suala lako kulingana na upeo mdogo wa watanzania hasa Hawa wanaojiita secretariat ya utumishi wa Umma huna Cha kufanya labda uwe political analyst ama political monger lakini kwenye Dunia inayoelewa maana ya degree hiyo unafanya kazi zote za social sciences ikiwemo sociology, ualimu, diplomasia, uongozi, utafiti wa mambo ya siasa, na taaluma zote za humanity.
 
Ndio wale unaosikia wanaitwa Chawa, kidding 🤣
 
Ni kweli.

Nilishangaa kumkuta jamaa yangu US anafanya kazi kwenye investment bank moja ila ana degree ya Geography. Na sio kitengo maalum, no mtu wa sales kabisa.
 
Abdul Nondo, kasoma political science
 
Hiyo degree uliyoitaja haipo bali kuna political science and Public administration.
Kabla haijawa kama membe ya msimu,walikuwa wanaajiriwa kwenye utawala,makatibu kata,tarafa nk
 
POLITICAL consultant, Political Analyst, Public Administration
 
Ni kweli.

Nilishangaa kumkuta jamaa yangu US anafanya kazi kwenye investment bank moja ila ana degree ya Geography. Na sio kitengo maalum, no mtu wa sales kabisa.
Marekani unaweza kukuta hata mtu wa political science, history, philosophy anafanya kazi ya bank. Mark Zuckerberg wa Facebook chuoni alikuwa anasoma Computer Science and Psychology.
 
Kwanza Siasa si sayansi - hii ni kuidhalilisha sayansi niliyoisosea.

Hiyo inatakiwa iitwe Degree ni Arts with (in) Politics.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…