Aisee haya Mambo ni magumu sana. Kuna mtumishi mwenzetu aliachana na mke wake miaka kadhaa nyuma(aliniambia mwenyewe) na akamuachia Kila kitu kuanzia nyumba, mashamba, mifugo na miradi yote aliyokuwa nayo kipindi wapo wote.
Akaamua kuanza maisha upya lakini wakati huu akiwa na stress Sana. Baada ya muda akakutana na mama flani ana watoto wawili akajiweka. Mama akajibebisha vya kutosha dingi wa watu akaona dunia si ndio hii Sasa akawekeza akaili yake yote kwa huyo mama. Akajenga, akaanza kusomesha watoto wa huyo mmama. Wamedumu Kama miaka mitano mpaka sasa Ila Cha ajabu hawajapata mtoto mwingine tofauti na wale aliowakuta. Sasa mimi huyo mama ni rafiki yangu Sana kwani huwa nachukua mazaga yote dukani kwake.
Akawa ameniamini sana, nilishangaa Sana siku moja ananiambia hana muda na huyo dingi na hawezi kuzaa nae hata kwa bahati mbaya. Hapo anasubiri astaafu avute mkwanja apite kushoto Kama nyumba ashamjengea na biashara ilishasimama hana mpango tena na huyo mzee.
Nilihisi kufariki alivyokuwa ananipa story ukizingatia Yule mzee nafanya nae ofisi moja na jinsi anavyompenda huyo mama ni hatari tupu. Mbaya zaidi anamshawishi aombe kustaafu akiwa na 55 asisubiri 60 ili mishe ya mama ikamilike chap. Nikajaribu kuwaza siku huyo mzee anaachwa na huyo mama atakuwa katika Hali gani.
WANAWAKE MUNGU ANAWAONA.