Ukitaka kuishi maisha marefu usioe

Ukitaka kuishi maisha marefu usioe

Ndugu Zangu Oeni Hayo Masuala Yapo Na YataendeleA
Tanzania Inahitaji Nguvu Kazi Bila Kuzaa Maana Yake Tutarudi Nyuma Sasa
Acha Upotoshaji!!
Kuzaa sio mpaka uoe ni swala la kukutanisha vikojoleo mimba inatungwa, mtoto azaliwa, mtoto alelewa, mtoto anakua, kizazi kinasonga
 
Aisee haya Mambo ni magumu sana. Kuna mtumishi mwenzetu aliachana na mke wake miaka kadhaa nyuma(aliniambia mwenyewe) na akamuachia Kila kitu kuanzia nyumba, mashamba, mifugo na miradi yote aliyokuwa nayo kipindi wapo wote.

Akaamua kuanza maisha upya lakini wakati huu akiwa na stress Sana. Baada ya muda akakutana na mama flani ana watoto wawili akajiweka. Mama akajibebisha vya kutosha dingi wa watu akaona dunia si ndio hii Sasa akawekeza akaili yake yote kwa huyo mama. Akajenga, akaanza kusomesha watoto wa huyo mmama. Wamedumu Kama miaka mitano mpaka sasa Ila Cha ajabu hawajapata mtoto mwingine tofauti na wale aliowakuta. Sasa mimi huyo mama ni rafiki yangu Sana kwani huwa nachukua mazaga yote dukani kwake.

Akawa ameniamini sana, nilishangaa Sana siku moja ananiambia hana muda na huyo dingi na hawezi kuzaa nae hata kwa bahati mbaya. Hapo anasubiri astaafu avute mkwanja apite kushoto Kama nyumba ashamjengea na biashara ilishasimama hana mpango tena na huyo mzee.

Nilihisi kufariki alivyokuwa ananipa story ukizingatia Yule mzee nafanya nae ofisi moja na jinsi anavyompenda huyo mama ni hatari tupu. Mbaya zaidi anamshawishi aombe kustaafu akiwa na 55 asisubiri 60 ili mishe ya mama ikamilike chap. Nikajaribu kuwaza siku huyo mzee anaachwa na huyo mama atakuwa katika Hali gani.

WANAWAKE MUNGU ANAWAONA.
Msanue baharia kuwa "proceed with great caution" aliruka mkojo bado hajatua (yupo hewani)akitua tu anayakanyagaaaaaaaahhhhh... asijisahau sana. Avute handbrake. Ni mpango wa Mungu kumuaminisha huyo mmama akuamini na akueleze dhamira yake ili wewe uwe msaada na mkombozi wa mzee wetu.
 
Msanue baharia kuwa "proceed with great caution" aliruka mkojo bado hajatua (yupo hewani)akitua tu anayakanyagaaaaaaaahhhhh... asijisahau sana. Avute handbrake. Ni mpango wa Mungu kumuaminisha huyo mmama akuamini na akueleze dhamira yake ili wewe uwe msaada na mkombozi wa mzee wetu.
Daah ni hatari Sana, napanga kumfanyia mpango ahame kituo Cha kazi kwanza awe mbali na huyo mama then mengine yaendelee.
 
Wewe ndiye mwokozi pekee wa huyo dingi pamoja na Muumba.
Huyo mama anamweka kwenye kilengeo daily
Kwanza mzee ashanunua gari akampa mdogo wake na huyo mama akimbize mjini jamaa akainywa rafiki yangu. Ila kwakuwa mapenzi sijui ndumba mzee akapiga kimya.
 
Naleta kisa kimoja au viwili kutetea uzi wangu.
Baba mmoja mtumishi wa mamlaka moja ya serikali ana kawaida ya kumpa mke sh.300k ya matumizi yake binafsi kama mke kila anapopata mshahara.
Hiyo pesa haina mahusiano na pesa za matumizi ya nyumbani.
Pia kampa fedha mke wake afungue miradi. Mke anaingiza faida ya angalau elfu 30 kila siku.
Mwezi mmoja mambo yaliingiliana, baba akampa mke pesa pungufu, alimpa laki 2 badala ya tatu kama alivyozoea. Uliibuka ugomvi mkubwa sana.
Yaani kazi ufanye wewe, ulishe familia, usomeshe familia, n.k na umpe mke mtaji na laki tatu kila mwezi lakini umefeli mara moja tu unawashiwa moto.
Vijana kataeni ndoa. Mtakufa.
Kisa kingine naona kazi kusimulia ila mwisho wa picha baba mstaafu kaibiwa pesa za mafao na mke wake kisha mke kumwachia nyumba na watoto.
Mzee kabaki na hali ngumu.
Vijana wenye uhakika na maisha msioe.
🤨🤨
 
Naleta kisa kimoja au viwili kutetea uzi wangu.

Baba mmoja mtumishi wa mamlaka moja ya serikali ana kawaida ya kumpa mke Tsh. 300k ya matumizi yake binafsi kama mke kila anapopata mshahara. Hiyo pesa haina mahusiano na pesa za matumizi ya nyumbani.

Pia kampa fedha mke wake afungue miradi. Mke anaingiza faida ya angalau elfu 30 kila siku. Mwezi mmoja mambo yaliingiliana, baba akampa mke pesa pungufu, alimpa laki 2 badala ya tatu kama alivyozoea. Uliibuka ugomvi mkubwa sana.

Yaani kazi ufanye wewe, ulishe familia, usomeshe familia, nk, na umpe mke mtaji na laki tatu kila mwezi lakini umefeli mara moja tu unawashiwa moto. Vijana kataeni ndoa. Mtakufa.

Kisa kingine naona kazi kusimulia ila mwisho wa picha baba mstaafu kaibiwa pesa za mafao na mke wake kisha mke kumwachia nyumba na watoto. Mzee kabaki na hali ngumu.

Vijana wenye uhakika na maisha msioe.
Naam
 
Back
Top Bottom