Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Unaonaje maisha ya kigamboni?
Unamshauri nini mtu anayefikiria kujenga huko?
Kama anapenda sehemu iliyotulia, barabara zisizo na foleni basi huku ni chaguo sahihi. Nasikia watu wanasema kuwa huku watu wanakaba sana but mimi sijashuhudia wala kusikia tangu nije huku.

Na kama mishe zake ni za kuingia sana town (kuvuka maji), basi afanye analysis vyema kama foleni ya kivuko au daraja la kigamboni itakuwa kikwazo kwake.

Ila binafsi, nimepapenda sana.
 
Nimeishi kigamboni 3 years, now nipo Kimara. To me sijaona sehemu nzuri ya kuishi kama kimara.

Na kweny swala la usafiri kwa ambao hawana private car, mwendokasi ndo the best public transport in Dsm. Why?

1. Haina foleni
2. Risk ya ajali ni ndogo maana ina njia yake peke yake
3. Ina accomodate watu wengi
4. Mabus yao ni makubwa unasimana vizuri na kuna uwazi juu wa kutosha
5. Unaweza change sehem za kwenda kwa nauli hyohyo moja
6. Hazikai mda mrefu kituoni, just 30 seconds.
7. Kipindi cha mvua au jua kali, abiria wanaosubiria usafiri kituoni hawakumbani na hyo ghadhabu.
8. Unaweza ukabadilisha kituo cha kazi na bado m/kasi ikawa ni suluhisho kwako. Mfano mm nimefanya kazi moroco, k.koo na sahv nipo posta, so bado haijaniathiri kiusafiri.

Challenge: magari bado ni machache alafu watu ni wengi, yanajaza watu wengi lakini hii unaweza ukaishi nayo2.
 
Na pia Kimara ukiingia ndani kidogo unapata sehem zilizo tulia, nyumba nzuri bei nafuu, hakuna kelele, ni sehen nzuri hata ya ku raise familia. Geografia yake ipo juu ya mwinuko kwahyo upepo wake ni mzuri pia. Ipo karibu na stand kuu ya dsm.
 
hapana mku, kigamboni hapafai kabisa, kama ni kwa sababu ya bahari tu sawa lkn kuna changamoto ya usafiri sana, nilifikia huko niliona tabu zake, nilitakiwa kuamka saa 9 usiku kwenda stendi ya Magufuli mbezi, siwezi kuishi mbali na kituo cha mabasi ya kwenda mikoani.
Mpango mzima sasa ni Mbezi, Luguruni, kibamba, kiluvya na kibaha.
Ukiwa kiluvya na ukatakiwe uende ulaya alfajiri itabid uhamie jet lumo
 
Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
Kigamboni hapana aisee, Wapemba ni wengi mno na majini ya kufuga wametapakaa kila mtaa.
 
Kuna wakati pantoon ilikosekana ikawa tunavukia kule TAFICO au kwa kutumia ngwanda ,maji yalikuwa ni tabu nyingine NUWA walitumia mtambo wao wa kule Mtoni Temeke,na ilikuwa tunakaa zaidi ya mwezi bila huduma ya maji Safi zaidi tukitegemea visima vya shimo
Usalama kwa maeneo yetu ulikuwa wa uhakika kwa asilimia zoote,ila kwa kadhia niliyopitia kumenitumbukia nyongo kuishi kigamboni ukijumlisha na gharama chakula kuwa juu
Hauna methali zako binafsi? Mana wewe ni muhenga pro

Cc. Angel Nylon
 
Kulivyo na joto sasa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]siku bahari imechemka?Mimi ngoja nizeekee huku Goba tu
 
Mvuto wa kigamboni umepotea kabisa hali ya kivuko sio poa. Asubuhi mida ya saa moja mpaka tatu na jioni umati ni mkubwa sana kivuko kina zidiwa.
 
Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
Mkuu,

Asante kwa kuwakilisha.

Ila lile daraja kama unakuja mjini haliko mbali na pembeni? Ukitoka huku Uhasibu au Mandela Road mpaka City Center si bonge la safari? Hakuna foleni pale?

Haingependeza zaidi kama lingejengwa daraja la juu pale Magogoni?

Pale lingepigwa daraja kuanzia Kigamboni mpaka Gymkhana huku Baraka Obama Road kuingia mjini, mtu anatoka Kigamboni mpaka mjini au anaenda kuunga daraja la Tanzanite/ Selandar.
 
Back
Top Bottom