Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Hii longoni iko karibu na wapi mkuu?
Yaani sjui nikuelezeaje Ila Longoni inaanza ndo inakuja mikadi pweza na zingine uko zinaendelea iko ndani Navy special forces
 
Kwani hospitals kubwa Dar ziko ngapi? Si Muhimbili na Mlongazila tu? Kuna hospitali ya wilaya tu kama Mwananyamala/Temeke/Ilala. Hakuna kitu kama Aga Khan.
Sijawahi kusikia hospital ya wilaya kigamboni
 
hapana mku, kigamboni hapafai kabisa, kama ni kwa sababu ya bahari tu sawa lkn kuna changamoto ya usafiri sana, nilifikia huko niliona tabu zake, nilitakiwa kuamka saa 9 usiku kwenda stendi ya Magufuli mbezi, siwezi kuishi mbali na kituo cha mabasi ya kwenda mikoani.
Mpango mzima sasa ni Mbezi, Luguruni, kibamba, kiluvya na kibaha.
Viwanja bei zikoje huko?

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Viwanja bei zikoje huko?

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
sijui bei mkuu, mimi kwa sasa naishi ipalamwa, ila natarajia kama nitaamua kuishi Dar basi nitajenga maeneo ya Mbezi karibu na kituo cha Magufuli, au Kibamba au kiluvya, maeneo hayo kwa sasa ni muafaka sana kwa sababu ya huduma zote muhimu zipo karibu kama vile; Hospitali ya Taifa Muhimbili mloganzila ipo huko, Kituo cha mabasi, barabara njia 8 n.k.
kuna nafasi na hewa safi, hakuna msongamano/uswahili.
 
Fikiria mawasiliano kwanza!
Mabasi ya mkoa mengine yanafika 7usiku!
Hebu muelekeze mgeni wako wa dharula namna ya kuifikia kigamboni kati!
 
Fikiria mawasiliano kwanza!
Mabasi ya mkoa mengine yanafika 7usiku!
Hebu muelekeze mgeni wako wa dharula namna ya kuifikia kigamboni kati!
Ha ha ha wabongo mna mambo! Kwanza siishi sehemu kwasababu ya wageni. halafu mabasi yanaanzia Kigamboni na kuishia Kigamboni yapo zaidi ya kampuni tatu.
Airport iko less than 15km from Kigamboni. Zanzibar boats just few yard away. Usafiri sio mabasi peke yake acheni kuwaza kinasikini.
 
Kigamboni kuna sehemu kuanzia Kibada mpaka Mikwambe ni kutamu sana. Upuuzi wa Kigamboni nikiwa kama mkazi wake ni kuvukavuka inakera kwa kweli. Pale wangejutengea tu daraja la kufunguka. Wakati inapita meli linajifungua.

Kigamboni uhalifu umeisha kama si kupungua kwa 90%. Sie wa huku mbali na kule mwanzoni maji tunapata kisima baridi. Mchanga kama wa beach, tabu kubwa bado wanapata bodaboda wanauwawa sana. Kero nyingine ni malori ya mchanga.
 
Uhalifu hauwezi pungua kigamboni hasa kibada, kisiwani, tungi, mji mwema na midizini. Wanakaba balaa!
 
Back
Top Bottom