Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

sijui bei mkuu, mimi kwa sasa naishi ipalamwa, ila natarajia kama nitaamua kuishi Dar basi nitajenga maeneo ya Mbezi karibu na kituo cha Magufuli, au Kibamba au kiluvya, maeneo hayo kwa sasa ni muafaka sana kwa sababu ya huduma zote muhimu zipo karibu kama vile; Hospitali ya Taifa Muhimbili mloganzila ipo huko, Kituo cha mabasi, barabara njia 8 n.k.
kuna nafasi na hewa safi, hakuna msongamano/uswahili.
Viwanja vinaendaje maeneo ya Mbezi huko?

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Ha ha ha wabongo mna mambo! Kwanza siishi sehemu kwasababu ya wageni. halafu mabasi yanaanzia Kigamboni na kuishia Kigamboni yapo zaidi ya kampuni tatu.
Airport iko less than 15km from Kigamboni. Zanzibar boats just few yard away. Usafiri sio mabasi peke yake acheni kuwaza kinasikini.
Hata ww unaweza kuwa mgeni!
Nielekeze mkuu hii sasa ni sawa.7½ nipo mbezi nifike ktkt Kigamboni
 
Kigamboni kuna sehemu kuanzia Kibada mpaka Mikwambe ni kutamu sana. Upuuzi wa Kigamboni nikiwa kama mkazi wake ni kuvukavuka inakera kwa kweli. Pale wangejutengea tu daraja la kufunguka. Wakati inapita meli linajifungua.

Kigamboni uhalifu umeisha kama si kupungua kwa 90%. Sie wa huku mbali na kule mwanzoni maji tunapata kisima baridi. Mchanga kama wa beach, tabu kubwa bado wanapata bodaboda wanauwawa sana. Kero nyingine ni malori ya mchanga.
Afande khamis amefanya kazi kubwa
 
Uhalifu hauwezi pungua kigamboni hasa kibada, kisiwani, tungi, mji mwema na midizini. Wanakaba balaa!
Uo uongo balaa la afande khamis wahuni wote wanalijua waulize vizuri
 
Natamani sana kuishi Mbezi au Kibaha

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
Njoo kibaha kongowe soga msufini kulipo na kituo kikubwa cha treni mwendokasi ..plot zinaanzia 1.5m kwa 400sq tayar kuna barabara ya ya lami washaanza kutengeneza ..na kuna eneo la viwanda limetengwa ...yan soon patapanda thamani
 
sehemu sahihi ya kuishi kwa raha mustarehe ni maeneo ilipo stendi ya Mabasi ya kimataifa ya MAGUFULI/ MAGUFULI BUS TERMINAL MBEZI, Luguruni, kibamba, kiluvya na maeneo hayo mengine.
 
Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
Weka ramani basi!
Na useme kwanini pantoni zinajaza watu wengi kupindukia?
 
Mkuu mikad sio wakaz wa kigambon asilimia kubwa wanaojaza mikadi ni viumbe wa mbagala videm wanyoa viduku chupi minuko ndio wanajaa san huko ukitaka kuamin hilo nenda weknd angalia magar yao waliyokod yanatokea wap
Hivi kwanini unapenda dharau binadamu wenzako tuseme wewe unamaisha ya mfalme wa Uingereza?
 
Back
Top Bottom