Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Kama anapenda sehemu iliyotulia, barabara zisizo na foleni basi huku ni chaguo sahihi. Nasikia watu wanasema kuwa huku watu wanakaba sana but mimi sijashuhudia wala kusikia tangu nije huku.Unaonaje maisha ya kigamboni?
Unamshauri nini mtu anayefikiria kujenga huko?
Nimepakubali sana. Napenda sehemu zilizotulia. Kabla ya hapo nikuwa napakubali sana Mbweni, ila kigamboni is far better.umepapenda au ndio hivyo tena bora liende???!
Ukipanga nyumba ni nyumba yako.Acha uongo nawe una nyumba [emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
Nimepakubali sana. Napenda sehemu zilizotulia. Kabla ya hapo nikuwa napakubali sana Mbweni, ila kigamboni is far better.
Kuna mazingira tu yalitokea ikawa ni lazima kigamboni.
Ukiwa kiluvya na ukatakiwe uende ulaya alfajiri itabid uhamie jet lumohapana mku, kigamboni hapafai kabisa, kama ni kwa sababu ya bahari tu sawa lkn kuna changamoto ya usafiri sana, nilifikia huko niliona tabu zake, nilitakiwa kuamka saa 9 usiku kwenda stendi ya Magufuli mbezi, siwezi kuishi mbali na kituo cha mabasi ya kwenda mikoani.
Mpango mzima sasa ni Mbezi, Luguruni, kibamba, kiluvya na kibaha.
Kigamboni hapana aisee, Wapemba ni wengi mno na majini ya kufuga wametapakaa kila mtaa.Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.
Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.
Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.
Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.
Karibuni sana Kigamboni.
Hivi Mungu anakusaidia Ili ujenge kibanda kweli kauli ya hivi siipendagi au unamaanisha kibanda Cha kuku?
Matt----t ako yako hapo goba 😅Watu wa kigamboni mnanuka vikwapa hamuogi kwa wakati.Ni hayo tu.Ahsanteni.
Hauna methali zako binafsi? Mana wewe ni muhenga proKuna wakati pantoon ilikosekana ikawa tunavukia kule TAFICO au kwa kutumia ngwanda ,maji yalikuwa ni tabu nyingine NUWA walitumia mtambo wao wa kule Mtoni Temeke,na ilikuwa tunakaa zaidi ya mwezi bila huduma ya maji Safi zaidi tukitegemea visima vya shimo
Usalama kwa maeneo yetu ulikuwa wa uhakika kwa asilimia zoote,ila kwa kadhia niliyopitia kumenitumbukia nyongo kuishi kigamboni ukijumlisha na gharama chakula kuwa juu
AiseeMatt----t ako yako hapo goba 😅
ni kwa sababu hupajuiSijawahi kutamani kuishi Kigamboni, sijui kwa nini!
Mkuu,Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.
Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.
Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.
Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.
Karibuni sana Kigamboni.
Napajua sana tuni kwa sababu hupajui