Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

hapana mku, kigamboni hapafai kabisa, kama ni kwa sababu ya bahari tu sawa lkn kuna changamoto ya usafiri sana, nilifikia huko niliona tabu zake, nilitakiwa kuamka saa 9 usiku kwenda stendi ya Magufuli mbezi, siwezi kuishi mbali na kituo cha mabasi ya kwenda mikoani.
Mpango mzima sasa ni Mbezi, Luguruni, kibamba, kiluvya na kibaha.
 
Shida kweli kweli na ma gharama yani ina maana wewe kuvuka itakulazimu upoteze 90-100K per months kwenda na kurudi kwako! Huu ujinga ndio unanifanya kigamboni sitaki hata kupasikia

Kabisa mkuu ukipita darajani kule unaacha 1500 go and return
 
Ukitaka mwisho wako wa Kutembea kutokana na Vibaka na Majambazi kuwa wengi na Kula Kwako Bata ( Kustarehe ) kuwe ni Saa 12 Jioni, basi kaishi Kigamboni.
Acha fix wewe. Mimi kuna siku nakaa huko Juliana,samaki samaki Hadi saa Saba nane na ninarudi Kigamboni usiku sina mlinzi geti nafungua mwenyewe. Niliishi miaka mitatu bila geti
 

Uber hazipo, bajaj za shida hasa usiku ukipata uber ubhatike feri ila anaweza asije. Bora niishi buza sio kigamboni [emoji23]
 
Ukiwa na gari ndo utaona tabu yake kama huna huwezi ona. Kwanza kigamboni imejitenga na mji wakati wa usiku vivuko vinasumbua sana
Kwahio tunakaa huku hatuna magari? Natumia average 45minutes kwenda Kijitonyama asubuhi jioni kurudi average one hour via darajani.
Usiku 15-20 minute's kivukoni niutafute nini
 
Wakati mwingine foleni ya magari kuingia kwenye kivuko inapita ofisi ya waziri mkuu hadi chuoni
Yan mm ndo nafikiria kuhama huku kigamboni nihamie tegeta nyuki maana stress za kuvuka na ma panton haya imenishinda aiseehh. sometimes bora folen kulko ule ujinga wa kuvuka maji
 
Kigamboni imebadilika sana mkuu huku mambo moto na hayo mambo yalikua miaka nyuma.Kigamboni ndo mji utakao kua umepangika vizuri sana hata masaki huko na obey watapasikia tu ...
Kigamboni panamfaa kwanza mtu asiye na Mambo mengi uwe saa 1 usiku upo kwako nje ya Hapo uwe na usafiri wako. Gari za abiria zinakata saa mbili tu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…