Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Vibaka vibaka, wezi na kaka zao majambazi wengi wameshapigwa vyuma [emoji379] na askari.. Ni watoto waliotoka mbagala, Kinondoni na maeneo memgine, ndio walianza kuleta usela mavi.

Nipo kigamboni toka 2000 mwishoni nikitokea kurasini.. Huku maisha yalikuwa shwaari kabisa unaanika hadi nguo na unazikuta asubuhi, walivyoanza kuja watu mbalimbali wakaanza kuharibu mji, ila sasa hali shwaari kabisa, mtaani si chini ya watoto 5 wamekula vyuma.. Kumepoa kinyama.

Hakuna sehemu kuna kosa kero..

Ila yoote kwa yoote kigamboni kuhama inataka moyo saana.
 
Fanya kazi kwanza. Bado tuko Juni 2021.
Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90 .Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo,mambo ni tofauti sana,mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu,ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani , hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne,ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na baraba mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
 
Kero ya Kigamboni ni moja tu - kivuko lazima ulipie kama una gari - 2000 kwenda 2000 kurudi - jumla 4,000, kwa wiki 20,000 kwa mwezi 80,000 kwa mwaka 960,000.

Ukiondoa gharama hizi kigamboni ni mji mzuri mno wa kuishi.. Space kubwa, hewa nzuri , wakazi wengi ni wa umri wa 30 - 50 yrs !!
 
Ukitaka mwisho wako wa Kutembea kutokana na Vibaka na Majambazi kuwa wengi na Kula Kwako Bata ( Kustarehe ) kuwe ni Saa 12 Jioni, basi kaishi Kigamboni.
Probably mara ya mwisho ulitembelea Kigamboni mwaka 2008 .
 
Kero ya Kigamboni ni moja tu - kivuko lazima ulipie kama una gari - 2000 kwenda 2000 kurudi - jumla 4,000, kwa wiki 20,000 kwa mwezi 80,000 kwa mwaka 960,000.

Ukiondoa gharama hizi kigamboni ni mji mzuri mno wa kuishi.. Space kubwa, hewa nzuri , wakazi wengi ni wa umri wa 30 - 50 yrs !!

Mimi na ka passo kangu 4000 ndio bajeti ya mafuta kila siku... kigamboni sipawezi kama darajani tu panataka 4000 kila siku
 
Mimi na ka passo kangu 4000 ndio bajeti ya mafuta kila siku... kigamboni sipawezi kama darajani tu panataka 4000 kila siku
Lakini kama unafanya kazi na ofisi zenu zipo Ilala & Kinondoni Temeke ama Posta basi utabana matumizi kama utaishi Kigamboni sababu mafuta ya kufika kazini ni kidogo, hakuna foleni pia utaamka saa 1 kamili ndiyo unaaza safari.

hiyo hela ya kivuko itajikata humo humo compared kama utaishi Bunju ama Mbweni, Tageta kuamuka saa 11 alfajiri kila siku na ku-drive zaidi ya km 30.
 
Back
Top Bottom