Ukitaka Kujua ni Jinsi Gani na Kiasi Gani WaZanzibari Wanautaka na Kuufaidi Muungano

Ukitaka Kujua ni Jinsi Gani na Kiasi Gani WaZanzibari Wanautaka na Kuufaidi Muungano

Kama usemavyo ndivyo, basi tuna safari ndefu sana, kwa sababu tuliowategemea wauvunje Muungano, sasa ndio wasiotaka kabisa kusikia hiyo habari.
Kwa maana yako ni kwamba tutakuwa nao CCM kwa muda mrefu sana.

Matumaini tuliyokwishayaweka kwa CHADEMA na yenyewe yanazidi kuwa hafifu sana. Hatujui Mbowe alirogwa na Samia kwa uchawi toka wapi, maanake hatujapata kuuona ukitumika ndani ya nchi hii tokea tuwe nchi huru.

Mbowe anajiapiza ataendelea na majadiliano ya Maridhiano, sijui wanaridhiana juu ya jambo gani tena!

Kwa hiyo CCM ipo palepale, haiendi popote.
Wanasiasa wengi wa Tanzania ni mamluki. Hivyo siyo wa kuwaamini hata kidogo.
 
Wale wamezoea vijembe tu, sisi tukisema hatuutaki Muungano kwa sababu zetu zenye mashiko, wao watakuja na vijembe vyao walivyozoea, kusema tu ilimradi wasikike.

Wanajua fika, huu muungano wa hovyo ndio unawafanya wao waishi kwa raha huko visiwani, marupurupu na mafuta ya magari yenye vin'gora vinachangiwa na muungano, either direct or indirectly..

Ndio maana naungana nawe ulipoandika kelele wanazopiga ni sawa na kucheza sinema chovu, sizivutia kutazama machoni petu watanganyika.
 
Hapana, sijataka hivyo; ninachosema tu ni kuwa waZanzibari hawataki tena Muungano uvunjike.
Kuna wakati, hasa lile kundi la akina Jussa na OMO, ilikuwa siku haipiti bila kusikia wakiimba wimbo wa kuuvunja Muungano.
Sasa hivi huwasikii tena wakiimba wimbo huo. Bila shaka Samia kawapa dawa ya kuuponya ule uhayawani uliokuwa umewaingia hao watu.
👏
 
Muungano upo kwa nguvu ya Watanganyika. Kama wakiamuwa hawautaki utavunjika kirahisi. Wala sioni manufaa Tanganyika inayoyapata.
 
Hivi kama nilisikia vizuri, eti ni kuwa Samia katika Ikulu ya Chamwino ametoa nafasi kwa ofisi ya Rais wa Zanzibar kuwemo mule?
Au sijaelewa vizuri hilo?
 
Back
Top Bottom