Ukitaka kujua serikali haijawahi kuwa serious na maendeleo ya kweli, Kabudi na michezo wapi na wapi?

Ukitaka kujua serikali haijawahi kuwa serious na maendeleo ya kweli, Kabudi na michezo wapi na wapi?

Tatizo langu, nchi yenye watu milioni 60, tunatawaliwa na watu wale walewale miaka yote, utadhani sisi wengine waliisha tupima wakakuta tuna matatizo ya akili.

Yani hata rais akitangaza baraza jipya kesho utakuta ni wale wale, ila wizara tofauti.

Tatizo ni nini wadanganyika wenzangu.?
Tatizo nyie vijana mna papara sana: nilimpa February uwaziri wa kule nje badala ya kunipigia promo, yeye akataka na kiti changu.

Yule mwingine anayevaa nepi yule na mwenzake wa ngorongoro sijui longido, wao wakaamua kauza ramani jinsi tunavyoshinda uchaguzi.

Yaani vijana mna haraka sana na hamuaminiki

Na ndiyo maana niliamua nimpe kile kibabu kile(99years old) nafasi kuuubwa kwenye chama chetu.
 
Kabudi amealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya ligi daraja la kwanza akaomba mpira aonyeshe uwezo wake akakosa hata danadana moja
 
Michezo siyo mpira wa miguu tu, uwaziri ni utawala,siyo lazima waziri wa madini awe na shahada ya miamba,wa kilimo awe bwana shamba, acheni ujuaji wa kijuha
Hilo ndo kosa kumpa mtu kuongoza asichokuwa na weledi nacho.
Mbn mnatenganisha utawala na ujuzi,weledi?
 
Kha! Uchawa ukienea kichwani wawezamwambia baba yako we huna baba
Sasa waziri wa michezo awe mtaalam wa michezo,michezo gani?..riadha,kuogelea,kikapu,kandanda, netball, hockey,kurusha tufe!?..chuo gani kinatoa kozi ya kufundisha michezo yote?
 
Sasa waziri wa michezo awe mtaalam wa michezo,michezo gani?..riadha,kuogelea,kikapu,kandanda, netball, hockey,kurusha tufe!?..chuo gani kinatoa kozi ya kufundisha michezo yote?
Kuna wataalamu waliosomea utawala wa michezo. "Sports management " hii ni taaluma .
Tusijifanye kuzoa makosa hii ndo sababu Baraza Lile Lile kutawala miaka 20 kwa kupumzishwa na kurejeshwa maona sawa.
Haya jiandae kumpongeza makamba na nape
 
We unafikiri wizara ni sehemu ya kila mtu kuteuliwa kukalia!?..sports management kasomea tennis, kandanda,kikapu,riadha, hockey, kurusha tufe, kuogelea,mieleka,mishale nk?..
 
We unafikiri wizara ni sehemu ya kila mtu kuteuliwa kukalia!?..sports management kasomea tennis, kandanda,kikapu,riadha, hockey, kurusha tufe, kuogelea,mieleka,mishale nk?..
Ungejipa hata dk 1 kujua sports management ni nn ungejifunza kdogo. Kumbe weledi siyo kigezo bali mjuano! Weledi wa kitu unachoenda kusimamia kwanza Kisha sofa zngne akikosa tunaendelea tuna taifa ukubwa.
 
Back
Top Bottom