Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakianza kutoa malalamiko yaukosefu waajira utadhani watapiga kaz kwelikwelMimi naona,mtu kama hujaridhika na malipo ya sehemu unayofanyia kazi, ni bora ukacheki issue zingine kuliko kupoteza muda wako au kuharibu kazi za watu coz mpaka unaanza hiyo kazi lazima utakua umesign contract au umekubaliana na muajiri wako,
Kufanya kazi kivivu hakuwezi kubadili chochote kisa unalipwa kidogo bali kinaweza kukusababishia hata hicho kidogo ukakikosa,
Mtu mvivu hata umlipe mshahara anaoutaka,atabadilika kwa muda tu ila ile hali yake ya uvivu na kutokuwajibika itarudi pale pale,uwajibikaji na kujituma ni tabia.
Piga kazi,timiza majukumu yako ipasavyo, Mungu atakuona tu na malipo yako utayapata tu,kama sio hapo ofisini kwako basi Mungu atakupa kazi bora zaidi hata sehemu nyingine, juhudi na kujituma hua haziendi bure,piga kazi huku ukimtegemea Mungu, hawezi kukutupa,jasho la mtu haliendi bure, jijengee tabia ya kujituma na uwajibikaji ni jambo zuri hata kama utaamua kufanya kazi zako binafsi.
Ndo Hali ilivo watu wanatanguliza pesa mbele wakati huduma mbovu....Hili tatizo lipo huyu alieleta mada hii ninahakiki amefanya kautafiti kidogo anajua alichoandika ww kama unaleta ushabiki sawa hata huku mtaani kwenye vibarua vidogovidogo tunayaona watu wanataka hela sio kaz
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ni kweli mkuu. .but kipindi hicho kumbuka tulikua tunaishi kwa Muongozo... Yan hata Kama hatupend kusoma lakini tunabanwa kutokana na Sheria za shule ...Ila huku makazini especially serikalini watu wanalindana Sana ... Mtu anaweza akatega hata week na bado mshahara uko pale pale ...tofaut kidogo na hz Taasisi au Kampuni binafsiNa wewe umesahau kipindi upo shule, ulikua unahaha ukiona muda wa kula unakaribia
Agreed [emoji817] ...Malezi yanamchango mkubwa Sana sanamkuu umeongea jambo la msingi sana, mfumo wetu wa malezi una kasoro, zipo tabia ambazo ni matokeo ya makuzi tuliyopitia tungali wadogo, Leo tunaziona familia za Wahindi hazitetereki kiuchumi kwasababu Wazazi wao huwashirikisha watoto katika kutafuta mali toka wangali wadogo, tunaona miji ya wenzetu ikiwa misafi hata majengo ya miaka mingi yanadumu ni kwasababu ya malezi na ustaarabu waliokuwa nao toka wakiwa wadogo.
kwa kweli yapo mambo ili tufanikiwe kama taifa lazima wazazi wawalee watoto katika misingi itakayowafanya kesho wawe watu bora. Sijisifii lakini najivunia Mama yangu alikataa kuajiriwa akachagua kuwa mjasiriamali ili awe na muda wa kutosha kutulea, aliwahi kuwa na Dada wa kazi lakini nakumbuka hatukudumu naye hata miezi 6 baada ya binti kushindwa kutekeleza majukumu yake. kumbukumbu zangu mara ya Mwisho familia yetu kuwa na Dada wa kazi ni mimi nilikuwa na miaka 3, tokea kipindi hicho kazi zote Mama na Baba walizifanya na kazi ndogo ndogo kama kusuuza vyombo kufuta vyombo, kufua nguo za ndani tulifundishwa tukiwa wadogo sana. Katika uzima sasa hivi ndo naelewa faida ya yale malezi.
leo wapo mabinti wakubwa tu hawawezi hata kupika chai sababu wana mfanyakazi nyumbani, tuna kizazi cha Wavivu, Wazembe ambao wanataka maisha mazuri na bora bila kufanya kazi. Hapa hata kutokomeza tabia mbaya ni changamoto. Kwa kweli tuanzie katika familia
Ndiyo hivyo tena. Kibarua kikiota nyasi ni afadhali nimeona watu wakichungulia kaburi. Hayo ndiyo matokeo ya hizi nchi yetu. Tukubali tu kuna tatizo mahali.Kuwa committed ukwamishe deal la wenzio 10 tu uone kama kibarua hakijaota nyasi😅
Kama mtu yupo ikulu na anaharibu imagine hizi ofisi za kawaida niaje, wale jamaa wa Ikulu kila siku wanakosea kuhusu teuzi na wakati wana mishahara mizuri nasikia na chai wanapiga nzito. Yani wanashindwa kuangalia tu kwa makini kazi kabla ya kuiweka publicMimi nikimkuta mtoa huduma mwanamke kwanza akili tayari inaanza kuchoka.. maana lazima utakutana na excuse au huduma ya kivivu, kama sio benki basi tegemea kuambiwa njoo kesho.
Yaani mtu yupo kwenye kutoa huduma akikuona mteja umekuja anaanza kukasirika maana alikuwa anachati