KERO Ukitaka kukata tiketi SGR unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi

KERO Ukitaka kukata tiketi SGR unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ukitaka kukata ticketi unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi mabehewa hayana watu kumbe kuna hujuma ya watu wa mabasi, wanafanya booking na hawasafiri. Serikari iangalie hili swala kwa upana.

Pia, Soma=> Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
Hii siyo kweli. Kama siyo wanapanda vituo vya mbele basi wamechelewa. Kwa sababu ukifanya booking inatoa muda wa kulipia. Ni chini ya dakika 50 kama sikosei
 
Kweni Abiria wote wataondokea Central Station?! Si wengine wamebuku wanapandia kwenye Vituo hata Pugu.

Labda ungesema waongeze Mabehewa au hata safari ziongezwe.

Lakini watu wanaotuhumu kuwa ni Makampuni ya Mabasi ndio yanahujumu mimi naona ni UFINYU wa FIKRA.
Uko sahihi..lakini ndio iwe kwa behewa zima? Yaani ukiwa unaomba zile siti hazifunguki kwa kumaanisha zimeshanunuliwa.
 
Sisi wengine hatupendi kuonekana kwa hiyo, ukija kwa lengo la kutuangalia kama unatukagua basi tunabonyeza transparent mode hutuoni lakini sisi tunakuwa tunakuchora vizuri tu.
 
Mfumo wao ndio unahujumiwa, na wanalojua hilo.
Mimi juzi nilikuwa nakata tiketi ya kuondoka kesho. Mfumo ulionyesha mabehewa yapo na nikapata mpaka namba ya kiti. Lakini hatua ya mwisho ilikuwa haifanyi kazi kabisa. Wanafanya makusudi hao.
Kuna kipindi walifanya hivyo hivyo tulipofika stesheni walituingiza kwenye tren bila tiketi, na tulipoingia ndani tulikatiwa humo ndani kwa vi device vya mkononi.
 
Ukitaka kukata ticketi unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi mabehewa hayana watu kumbe kuna hujuma ya watu wa mabasi, wanafanya booking na hawasafiri. Serikari iangalie hili swala kwa upana.

Pia, Soma=> Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
kama TRC inataka kufanya biashara,iangalie suala hili
mimi imeishanikuta lakini nikawa postive nikidhani imejaa kweli.
Lakini hapa umenifungua macho,mbali na hujuma wafanyakazi wa reli wanaweza tumia wingi wa wateja kuomba rushwa kwa kutoa taarifa zisizo sahihi,ili wahusika wajijtetee kwa kuwapa rushwa.
 
Hii nilishaiona week sasa.
Siku tatu treni zote zimajaa na ukienda huoni kuwa zimejaa
Nilijua ni mm tu ndiyo nakutana na hiyo hali aisee, yaani unakuta siti zote ziko inactive huwezi kuselect maana yake ziko booked ila ukienda pale station unakuta watu wananunua ticket, na ukiingia ndani empty siti unakuta za kutosha tu.
 
Ukitaka kukata ticketi unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi mabehewa hayana watu kumbe kuna hujuma ya watu wa mabasi, wanafanya booking na hawasafiri. Serikari iangalie hili swala kwa upana.

Pia, Soma=> Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
Siyo sawa ulivyoongea. Kwani ticket inatolewa ukifanya booking au ukilipa pesa? Kama pesa inalipwa kuna hujuma gani?
 
Mradi ulishaanza na gundu hairisho za kuanza zilikuwa nyingi
 
Ukitaka kukata ticketi unaambiwa treni imejaa, muda wa kuondoka treni inakuwa wazi mabehewa hayana watu kumbe kuna hujuma ya watu wa mabasi, wanafanya booking na hawasafiri. Serikari iangalie hili swala kwa upana.

Pia, Soma=> Online booking SGR haifanyi kazi, nifanyaje?
Utapeli mwingi na kukomoa wananchi wa kawaida. Unakuta mwenye pesa anaamua tu kukatia tiketi watu kama 20 lakini hasafiri na hakuna taarifa ya yeyee kuahirisha safari ndio maana unaona joka linaondokaa sismizi kudandia juu yake.......
Kuna safari ndefu sana mwananchi wa kawaida kujihisi ni sehemu ya wenye neema ya kipato kikubwa
 
Back
Top Bottom