Ukitaka kumuona shetani 'live' funga ndoa

Ukitaka kumuona shetani 'live' funga ndoa

Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Kama kuna sehemu ambapo shetani anapenda kukaa basi ni ndoa. Yaani anakusubiria tu uingie kwenye ndoa takatifu aanze kukutesa. Kama sio ugomvi na huyo mkeo au mumeo unayeona ni halali basi ni ngumi. Sasa Yale ambayo ulikuwa hujui kuhusu mkeo na mumeo unayajua.

Hamna rangi ambayo utaacha ona, anaweza shika tumbo na msipate mtoto. Akiona haitoshi anashika na uchumi ili mkome mkomae kabisa. Mbona Bado, akikuachia huku anakimbilia kwenye tendo husika anaweka mazoea, apo unamuona mkeo kama dada yako.

Ukute Sasa amekalia zinaa ni mwanaume na mwanamke wanachepuka. Achana na huo uchumba sugu ambao unajifanya unamchunguza mwanamke na mwanaume ili umjue. Huwezi mjua mkeo wala mmeo.Ingia kwenye ndoa umuone shetani live.

Donatila
Umepiga kwenye mshonooo..!!!
 
Unashangaa dada mzuri mbona ananipiga ngumi za mandonga..

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
IMG-20220319-WA0032_094648.jpg
 
Ukristo wa kileo ndii uliharubu ndoa baada ya kuifanya kuwa kinga ya wanawake na wanaumenkuwa wahanga wakuu wa ndoa!!

Leo mwnamke akishafunga ndoa ndio ana jiona ana haki ya mgao wa Mali yaani mtaji was maisha kwa nguvu za mwanamme!!

Ndio maana tunashudia viburi vya kina mama huibuka na mwanamme rijali akiona hivyo Hana namna zaidi ya kifo kuwa ndio utatuzi wa tatizo coz akiona talaka inamnufaisha mwanamke Alie zaa watoto!Sasa atafanya ninni!!?kuua make au kujiua!ndio maamzi common Hadi sasa!


Wanaume hatujapata Tiba halisi ya ndoa inapoharibika zaidi ya kuua make au kujiua tafiti zinaonyesha hivyo!yaani una muwahi mwenzio kabla hajakutilia sumu kimya kimya ukafa Kwa ugonjwa was muda mrefu!!

Mfumo dume ulidumisha ndoa ndio sisi tukazaliwa na viongozi was Leo ,sasa mfumo dune unge be modified lakini serikali na dini wanaua kabisa mfumo dume hawajui bila mfumo duke hakuna ulimwengu Wala kustawi Kwa chochote kabisa fikiria viongozi was kesho,yaani kina samiah,kikwete,jpm was kesho yaani was uzao wako watakuaje!!we fikiria kama mfumo duke ulizaaa kina nyerere he mfumo jike utazaa kina Nani!!!?
Mimi ningekua mkristo nisinge oa kabisa, ndoa ya kikuristo ina kufanya mwanaumme kua mtumwa wa Mwanamke af uko gerezani hutoki umefungwa wa kifungo cha maisha, wanawake wenyewe ni know much loh!!!
 
Shetani Hayupo.

Ubinafsi,Tamaa, mipango mibovu, ujinga n.k ndio vyanzo vya matatizo mengi ndoani.

Chanzo cha matatizo kwenye ndoa ni wanandoa wenyewe na tabia zao.

Shetani ni Fictional character anayetumiwa kama kichaka cha kukwepa uhalisia wa Tabia mbovu za wanandoa kiujumla.
 
Hapa katafutwa mbuzi wa kafara kabatizwa Jina la SHETANI. Kiasili binadamu hajaumbwa amchukue binadamu mmoja duniani kote aishi nae kwa kigezo cha eti kuanzisha familia. Ndo maana hakuna kitu kigumu kama kulala kitanda kimoja na mtu ambaye mmekutana ukubwani kwa muda usiojulikana. Hata mama yako au kaka yako au dada yako mliyeshea ziwa la mama mmoja huwezi kuvumilia kulala naye chumba kimoja milele mpaka kifo kiwatenganishe. Vitabu vya dini vinatuongopea, ndo maana kipindi kitamu na kizuri cha mahusiano ni mkiwa kwenye uchumba, sababu Kila mtu anakaa kwake, mnakutana kwa ishu maalum au outing, saa nyingine weekend nzima pamoja jumatatu Kila mtu kwake. Na kipindi chote hicho kuna vitu huwezi kuvijua hata ufanyeje kwasababu kila mtu anaamkia kwake. Shida huwa inaanza baada ya honeymoon ndo kila mtu anajiachia, hapo mnamuingiza SHETANI kuhusika kumbe ndo mmeanza kujuana vizuri. Ndoa zote zilizodumu ukiacha za kuvumilia tabia za wazee wetu, ni zile ambazo wapenzi wameishi pamoja hata miaka 10 pengine hata na kupata watoto, halafu wanafunga ndoa baadae. Sababu hakuna aliyeigiza kabla ya kufunga ndoa. Hizi nyingine za mtu anaigiza Ili mfunge ndoa, baadae lazima mapichamapicha yaanze mkimbilie kusingizia SHETANI. SHETANI ni kichaka cha kutokukubali ukweli. Na jamii nzima imekubaliana na huo unafiki. Ndoa lazima litaendelea kuwa kaa la moto mpaka siku binadamu akiacha UNAFIKI.
Kwa kifupi changamoto zinazo jitokeza baada ndoa ndio mtoa mada amezipa jina shetani.... Ile milima na mabonde wanandoa wanayo pitia ndo hivyo...

Kiualisia alicho sema kipo na mimi ni shaidi mbichi kabisa.
 
Back
Top Bottom