Ukitaka kuoa usiangalie kabila wala Nyash bali chunguza kama Baba wa mkeo mtarajiwa ni mkoloni, utakuja kunishukuru

Ukitaka kuoa usiangalie kabila wala Nyash bali chunguza kama Baba wa mkeo mtarajiwa ni mkoloni, utakuja kunishukuru

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Malezi ya mtoto ni conditioning, na kama tunaongelea mtoto wa kike basi uhusiano wake na baba yake utakupa ishara bora jinsi utakavyokuwa ndani ya ndoa na wewe

Kuna wale mababa ambao huwaita watoto wao wa kike maneno ya kiutani utani; utasikia "my little angel", "Sweetheart" na ukurutu mwingine. Basi muoaji ukikutana na sampuli hii KIMBIA maana utateseka sana; huyo mwanamke mtu pekee anayeweza kummudu ni Baba yake tu (wewe hauna tofauti na mwalimu wa field), heshima atakayokupa wewe haitalingana na anayompa Baba yake na mkizinguana kidogo tu ni rahisi kurudi nyumbani

SASA kuna hawa mababa ambao inabidi wawe mifano ya mababa wote, hawa ni mababa ambao ni vichwa hasa hasa wa nyumba zao, hawa ni mababa ambao mtoto wa kike akipata mimba nyumbani anafukuzwa mtoto na mama yake, hawa ni mababa ambao hata kama umenasa kituo cha mabasi kisa umeibiwa nauli hakutumii (ingawa anayo) ili uchangamshe ubongo ufike nyumbani na ukifika atakwambia "ubongo ni kama kisu, lazima kinolewe", hawa ni mababa ambao wakikukabidhi mke wamekukabidhi mke kweli kweli; unakuta mke kakulia mjini ila anajua kuwasha moto wa kuni na mkipigika kimaisha hakuangalii usoni kama mtoto kichanga, ataazima jembe atalima matembele watoto wale na wewe mme akupunguzie mizigo uwaze mambo makubwa makubwa kama kodi na ada za shule za watoto

Kwa ndugu zangu wa nyanda za juu kusini nadhani wako very familiar na sampuli hii ya wanawake, maana wazee wa kikoloni wa kihehe na kibena hawafanyi utani kabisa kwenye masuala ya malezi
 
Back
Top Bottom