.........ingawa umetufokea mkuu, ila tutajaribu kubadirika taratibu.....binafsi labda niseme tu Kikawaida kabisa na kiasili psychological weakness ya mwanadamu yoyote ipo ktk kitu kinachomgusa whether positively or negatively .......Sasa kwa kuzingatia hilo mara nyingi mambo yanayofanywa na watu yanategemea vitu vikubwa viwili:
1: Nature, Sasa kiasili binadamu anareact faster katika jambo linalomgusa yeye zaidi kuliko mwingine, Sasa ktk hili mapenzi ni jambo linalomgusa au kumuhusu kila binadamu ktk ulimwengu huu, Ina maana jambo lolote linalonasibishwa na mahusiano lazima litapata wahusika au wachangiaji wengi ambao hao watu ni kutoka makundi yote eg wanasayansi, wanasheria, wahandisi, madaktari etc, mind you kuwa mwanasiasa hakukuondelei ulazima wa kuwaza mapenzi coz mapenzi ndo chanzo cha uhai na familia, wanasema yanarun dunia
2: Nature au mazingira na hapa vitu kama professions, interests vinaingia, watu wanafanya mambo au wanazungumza vitu kutokana na kuvipenda na kuvihitaji Kwa sababu tu mazingira aliyopo yanamuhitaji afanye au ashiriki.....Sasa hapa ndo unakuta watu wenye shida fulani wnazungumza kitu kimoja, watu wa siasa ikitoka hoja ya kisiasa watakutana, wakisema bodaboda utawapata hapo....Kwa mfano hapa tz watumishi wote wa serikali ni zaidi ya laki sita lakini walimu ni nusu ya watumishi wote, kwa hiyo kumbe hata hapa jf ikitoka mada ya mwalimu tegemea itachangiwa na wengi, na ktk swala la interes ni ngumu kumzuia mtu kudeaal na jambo analolipenda au kulihitaji......ndo maana hii psychological weakness inatumiwa vizuri sana na wanatheologia na wachungaji kukusanya sadaka, hapa wanahubiri matatizo na mahitaji ya kimwili na kiuchumi ya mwanadamukama vile kuponya wagonjwa, kupata utajiri, kujenga nyumba, haya yanawagusa watu wengi na ndio mahitaji ya wengi ndio maana mikutano inajaa.....
So niseme tu kwamba Sina uhakika sana kama ishu au za mahusiano zitakuja pungukiwa wachangiaji coz mapenzi sio optional ni compulsory to both serious people and funny people, lakini pia kwenye baadhi majukwaa kama siasa tupunguze ujuaji na kutukanana kunapunguza wachangiaji, mf jukwaa la siasa ambapo tunaamini nchi inajadiliwa eti Ili uonekane una akili na upate likes lazima uilaumu serikali, umtukane mama na udai katiba, na ukijichanganya ukasema katiba iliyop inafaa utashambuliwa hadi umkumbuke rikiboy......
Lakini pia jukwaa la michezo ni usimba na uyanga tu, sasa kama wewe ni mtu wa darts , swimming au gymnastics au hata EPL thread yako itapata likes mbili, lakini halaumiwi mtu si watu hawako interested, kwenye magari pia kule kama huna gari utasemwa na ukiwa na gari wanasema unaringa, lazima watu wapungue tu, hata Mimi ninaepanda daladala naweza changia kuwa gari Ina matairi ya duara...nisikilizwe....
Hitimisho: Waanzisha nyuzi katika mjukwaa yote Siasa,mmu, mahari, michezo, biashara etc tujaribu kuanzisha mada za kujenga na tupunguze mizaha na matusi kwenye koments Ili mijadala iwe ya kujenga zaidi hasa Mmu ili tusiitwe wpumbavu next time.........