Ukitaka kuwa tajiri, usiende shuleni

Ukitaka kuwa tajiri, usiende shuleni

Mpenzi msomaji je ushawahi kukaa chini na kujiuliza ni ma professor wangapi ma billionaire duniani?,au waalimu? ambao ndo wataalamu wa kufikiri inavyosadikika?,
Hawa ndo chanzo cha umaskini..sina maana kwamba nawachukia au nawadharau la hasha ila ni kutokana na mifumo mibovu ya elimu iliyopo nao ndo wanaihubiri au kuisimamia.
kivipi?,
Mara nyingi tumesikia haya maneno.MWANANGU/MWANAFUNZI SOMA SANA PATA MAKSI ZA JUU ILI UJE KUPATA KAZI NZURI YENYE MSHAHARA MKUBWA.
huu ni ujinga kwa sababu mtu akiajiriwa una kuwa na usalama wa kazi tuu lakini unakuwa hauna uhuru wa kiuchumi{financial freedom}.
unapoajiriwa na kampuni unafanyia kazi watu wengi ambao mnagawana nao mshahara pasu kama hivimshahara wako unakatwa haya kabla hujapokea.:
kodi ya serikali
makato ya bima
makato ya benki
makato ya vyama vya wafanyakazi
Alafu ndo unapokea hela yako ndo maana tumesikia wafanyakazi wengi wakilia sana juu ya makato kuwa ni makubwa sana..baada ya hapo unakwenda nyumbani na iyo hela ambapo zinakwenda katika vibobo vya kukutia umaskini ili urudi tena kazini ambavyo ni kodi ya nyumba .maji.umeme na ada za watoto na kama muflisi gari unanunua mafuta na ku li lipia kodi zake.
Huenda ujanipata vizuri sasa utanipata nachomaanisha.
Ni kuwa huyu mwajiriwa hana vitega uchumi miradi ambayo ingemuingizia pesa za kutosha maisha yake yote ndo maana baadhi ya waajiriwa wanapo staafu hufa gafla kwa sababu ya ukkata.
EMBU TUMUANGALIE MWEKEZAJI.
WAWEKEZAJI WENGI MA BILIONAIRE HAWANA DEGREE KWA MFANO.
BAKHRESA WA AZAM
PATRICK NGOWI.TAJIRI MTOO NAMBA MOJA TANZANIA
BILL GATE WA MICROSOFT
JOHN D ROCKEFELA WA STANDARD OIL OF AMERICA
MARK WA FACEBOOK
na wengine wengi unaweza ni PM.
Ma investor wote unajua wanakatajwe kodi?
ni baada ya kutoa garama zote za uendeshaji na ile faida iliopatikana ndo inakatwa kodi.
Mpenzi msomaji bwana HENRY FORD aliwahi kusema thinking is the hardest work there is that is why so few people engage in it.
2;:Wapendwa wasomaji nimepata PM nyingi sana wakitaka vitabu vya Robert kiyosaki na nimewapatia in terms of soft copy na audio.kama na wewe unataka njulishe ntakutumia kwa e mail au basi au njia yoyote ile. nicheki weyosi@yahoo.com
Professor bilionea:becky:Professor Billionaire: The Stanford Academic Who Wrote Google Its First Check - Forbes
 
Unajichaganya, heading inasema ukitaka kuwa tajiri usiende shule halafu unauliza maprofesa wangapi ni mabilionea na kisha unataja mabilionea ambao hawana degree, kwa hiyo kupata degree pekee ndio kwenda shule? Wenye Diploma, Vyeti n.k hawajaenda shule?

Bill Gates alikuwa Havard kabla ya kuacha na kuanzisha Microsoft. Mark Zuckerberg alianzisha Facebook bwenini kwake Havard na Michael Dell alianzisha Dell Computers akiwa anasoma Chuo kikuu cha Texas, Austin kabla ya kuamua kuacha masomo na kujikita kwenye biashara. Hawa huwezi kusema hawakwenda shule na naamini kwenda kwao shule ndio kuliwasaidia mpaka kufanikiwa.

Mwisho hapa chini nakupa majina ya mabilionea wanne maarufu ambao wana degree:

1. Michael Bloomberg ( Bloomberg L.P, Utajiri wa Dola bilioni 27) - Electrical engineering/Business Administration

2. Phil Knight ( NIKE, utajiri wa Dola bilioni 14) - Business Administration

3. Oprah Winfrey ( OWN, utajiri wa Dola bilioni 2.8) - Communications

4. Jeff Bezos ( Amazon, utajiri wa Dola bilioni 25) Electrical engineering/computer science

Umwasahau jamaa wa Google ambao ni PhD drop out. Sasa Mtu ni PhD drop out anasema hakwenda shule?:becky:
 
Ukisikia umasikini jua tatizo kubwa niukosefu wa elimu tu. Masikini wote ni jamii ya watu waliokosa elimu na ni wachache sana waliofanikiwa kama wakina bakhresa. Ktk kundi la wasomi uwez ukakuta maskini ni watu wa kipato cha kati japo wapo na matajiri wachache.

Angalia wa na vijiji na vijiji vyetu jinsi vilivyochoka ni matokeo ya kukosa elimu kama kutokwenda shule kungetufanya kuwa matajiri basi vijiji vyetu vingekua majiji makubwa duniani

Peleka mtoto shule
 
ila pia kwenda ndo usiache kwenda shule kabisaa...u have to go to school to learn the 'basics' na kujua dunia inaendaje,then find ur way out ..wapo wengi waliojiajiri kutokana na visomo vyao na wamefanikiwa sana,mf.auditor kufungua auditing firm,lawyers na firm zao,doctor's na hospitala u medical centres nk...
kubaya ni ile kudhani kwamba ukishaajiriwa basi ndo umefika na maisha yanaishia hapo,unless kama mtu unaridhika na vidogo...ila kama mtu unapenda kuenjoy life zaidi,travels and vacations ,more time kula bata ,and having most of the things u want in life KUJIAJIRI NDO MPANGO MZIMA

Umeolewa ?? Lol
 
Hili lako baba.dont force me to beleive wht ur saying hakuna formula ya maisha kila mtu kaandikiwa chake na atafanikiwa au kifeli kama alivyoandikiwa na muumba wake
Fikira za kila mtu kaandikiwa chake nadhan ndo chanzo cha umaskini wa watu wengi hasa wale wanasema wanaimani.....wanashndwa fanya kazi..wanakata tamaa kwa mawazo kama haya... Fanya kazi kwa juhudi na nia utatoboa acha hayo mawazo ya kila mtu kupangiwa...Jah bless
 
Hakuna tajiri asiyekuwa na elimu. Tatizo la mtoa mada umekariri elimu hadi mwenye degree,masters au PhD. Wenzetu wanapenda kujifunza vitu vingi kwa wakati tofauti. Tatizo letu sisi tumejiwekea kikomo kwenye elimu ya darasani. Ndiyo maana sio ajabu kijana mdogo kwa Japan asiyekuwa na degree akajua vitu vingi kuliko wa huku mwenye masters kutokana na uzoefu na mazingira tangu mtoto na nidhamu ya kujifunza na kufikiri
 
Uwongo mtupu, katika Forbes list ya mabillionaire 400 duniani ni asilimia 15% tu hawana degree.

Kwa maisha ya Tanzania ndo shida zaidi utapata wakati mgumu sana kupata experience ya kuanzia kama haujasoma. Maprofesa sio matajiri kwa vile hilo sio lengo la kuwa profesa, lengo la kuwa profesa ni kufundisha watu.
 
Umwasahau jamaa wa Google ambao ni PhD drop out. Sasa Mtu ni PhD drop out anasema hakwenda shule?:becky:
Warren Buffet -Masters, carlos Slim -Degree, Marissa Mayer -Masters,
Sheryl Sandberg -Masters, Peter Thiel -Masters, Elon Mosk -Phd Dropout, Reid Hoffman -Masters.
 
Hapa Bumbuli wasioenda shule kibao wengi walevi na no maskini wa kutupwa kuliko wenye kazi zao

Yes sema pata Elimu jiaajiri ila usiniambie nisiende shule utakua hunitakii mema

Zaidi ya kipato shule husaidia kujenga personality ya MTU kujua mengi katika maisha .

Tatizo ni kwamba watu hawana uthubutu wa kujaribu kujiajiri.

Hiyo mifano ya mabilionea sio kama hawakuenda shule .Walienda ila walidrop out baada ya kuona opportunity za za kutokea kwenye maisha.

Wapo mabilionea walioenda shule mfano aliko dangote.

My take:

Shule muhimu but wakati unasoma na unapoajiongezea ufahamu kuwa na mtazamo wa kujiajiri

Ova
 
mm nafikiri shule ina umuhimu wake kwenye maendeleo binafsi.....lakini kadiri unavyozidi kusoma ndivyo hivyo hivyo unazidi kupunguza ujasiri wako katika swala zima la biashara kwa kuwa utakuwa unafikiri sanaaaaa katika mambo ambayo hayahitaji kufikiri bali yanahitaji maamuzi,ukichukua watu wawili wanaojielewa ..mmoja aliyeishia form four....na mwingine aliyemaliza degree...ukawapa 5m wafanye biashara,trust me aliyeishia form four atamzidi mwenzie after 1year na unaweza ukakuta hiyo 5m kwa huyo mwenye degree bado anafikiria aifanyie nini!!jiulize huko shule ulipoenda ni masomo mangapi unayoyatumia direct katika kupambana na maisha?...hii ndiyo iliyowatokea wakina Bill Gates na wenzake ambao baada ya kuona mapema kuwa elimu waliyonayo inawatosha wakaamua kupeleka nguvu zao kwenye maisha...

The reality is that school does not make you successful because it does not teach you financial education. In fact, many of the most successful people in history were successful without finishing school.

To illustrate my point, here’s a list of 50 people who did not finish school but went on to be very successful.

George Washington ​President of the United States
Abraham Lincoln ​​President of the United States
Harry Truman ​​President of the United States
Grover Cleveland ​​President of the United States
Zachary Taylor ​​President of the United States
Andrew Johnson ​​President of the United States
John Glenn ​​​Astronaut, U.S. Senator
Barry Goldwater ​​U.S. Senator
Benjamin Franklin ​​U.S. Ambassador
Winston Churchill ​​Prime Minister of England
John Major ​​Prime Minister of England
Robert Frost ​​Poet
Florence Nightingale ​Nurse
Buckminster Fuller ​Futurist and Inventor
George Eastman ​​Founder of Eastman Kodak
Ray Kroc ​​​Founder of McDonald’s
Dave Thomas ​​Founder of Wendy’s
Ralph Lauren ​​Fashion designer and Entrepreneur
Doris Lessing ​​Nobel Prize recipient in Literature
George Bernard Shaw ​Playwright
Peter Jennings ​​News anchor for ABC
Christopher Columbus ​Explorer
TD Jakes ​​​Pastor
Joel Osteen ​​Pastor
John D. Rockefeller ​Founder of Standard Oil
Karl Rove ​​​Presidential advisor
Ted Turner ​​Founder of CNN
Quentin Tarantino ​Movie director
Peter Jackson ​​Movie director (Lord of the Rings)
Mark Twain ​​Author
Leon Uris ​​​Author
Carl Bernstein ​​Washington Post reporter
Carly Fiorina ​​CEO of Hewlett Packard
Charles Dickens ​​Author
Andrew Carnegie ​​Industrialist
William Faulkner ​​Nobel and Pulitzer Prize winner
Li Ka Shing ​​Wealthiest man in Asia
Richard Branson ​​Founder of Virgin Atlantic Airways and Virgin Records
Enzo Ferrari ​​Founder of Ferrari
Henry Ford ​​Founder of Ford Motor Company
J. Paul Getty ​​Founder of Getty Oil
Jack London ​​Author
Larry Ellison ​​Founder of Oracle
Tom Anderson ​​Founder of MySpace
Mark Zuckerberg ​​Founder of Facebook
Steve Jobs ​​Founder of Apple
Steve Wozniak ​​Founder of Apple
Bill Gates ​​​Founder .of Microsoft
Paul Allen ​​​Founder of Microsoft
Ringo Starr ​​Beatle

The point of sharing this list with you is not to suggest that kids should drop out of school, or that school is not important. Education is very important. The question is: What kind of education? And where will your children’s education take them? Will it prepare them for the future? Will it secure their financial future in a world with less and less security?
 
Elimu muhimu ni angalau uwe umemaliza elimu ya sekondari. Hapa utakuwa umejifunza mambo mengi sana, kuanzia hesabu, lugha, bookkeeping etc
Ukisoma.haya yatakusaidia kujua wapi utatakiwa kushika ili uweze endelea. Pia akili ya mtu inahusika sana maana wapo waliosoma hadi hizo phd ila hawajielewi na hawaelewi nini wanataka
 
Unaposema "ukitaka kuwa tajiri usiende shule" unamaanisha nini?
Nafikiri kwako wewe elimu unamaanisha shahada na kuendelea!!
Hivi hao kina Bill Gate, wa facebook utawaita sio wasomi wakati ni bachelor drop out????
UUMEKARIRI! Shule ni LAZIMA, acha kupotosha watu!
 
Napingana na wewe kwa muono mfupi, hivi nyinyi na watoto wenu mnakwenda shule ili muwe tajiri? Ndio maana tunatuibia mali zetu za umma, Escrow, mikataba ya rushwa kwa kutaka utajiri na kuwaacha watu behind na umasikini.

Ndugu yangu hebu njo huku ulaya uwone masikini na tajiri wasomi na wasio wasomi, wote life ni sawa tu, tatizo la kuwa tajiri inategemeana na ubongo wa mtu wa kifikiri na confidence ya mtu katika kufanya mambo.

Mimi mtoto wangu namhamasisha kusoma sio awe tajiri bali atoe ujinga, mtu alie soma na asio soma ni tofauti, na ninapo sema kusoma, iwe professional yoyote tu, hata ukisomea mpira kuwa professional yako, hio inakusanya uwe mtu tofauti na mtu alikaa nyumbani na kupakata matako.

Kuna elimu tofauti, kuna elimu ya juu na msingi, elimu ya msingi ni lazima kwa kila mwanadamu kwa vile ndio itakayo kuwezesha kujua kusoma na kuandika, na Hesabu. Chukulia huku nchi zilizo endelea, tunapopeleka watoto wetu school, akionekana kuwa ana kipaji cha mpira, wazee Tunaitwa na kushauriwa kumpeleka football academic kwenda kusoma mpira na kuwa professional, mtoto huyu huyu naweza kumuweka katika watu walio kuwa na mafanikio na heshima kama proffesa.

Kuwa tajiri haliyakuwa huna elimu, ni moja tu ya maisha, kwani Mungu hakuweka mashart ya mtu kuwa tajiri lazima awe vipi ndio atampatia.

Kila mja huja duniani na rizki yake, kuna wengine Allah amewapa akili za kuzaliwa, kiasi ambacho wanakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kusoma vitu kwa kupitia macho yao tu kama mfano kwao na wao hujituma na hatimae hujikuta katika mafanikio.

Tatizo la wasomi ni moja tu, ambalo wao hushindwa kujitambua, hutaka kuajiriwa, na hawataki kujituma kama mlala hoi, wakati wasomi ndio wenye mbinu za kuwaokoa create jobs, kwa kutumia elimu zao lakini huwa hawataki kwa sababu wanaona wamepoteza muda mwingi katika masomo.

Lakini mimi kusoma nachukulia ni njia ya moja ya kujitoa ujinga na kupanua akili kimtazamo, kujiajiri ni best way ya kuwa tajiri. Iwe msomi iwe si msomi.
 
Duh huyu siyo mzima kakulupika kuandika huu uzi hana utafiti kaambiwa na mtu na yeye bila kuchuja kaleta Kama alivyo ambiwa.
 
Mkuu naomba audio na soft copy ya vitabu vyote vya kiyosaki pamoja na vya business ulivyonavyo
 
shule muhimu mkuu. utajiri ni juhudi zako mwenyewe. lakini elimu itakupa mwanga wa kupambana na maisha.
 
Kuna vitu viwili mto mada ana confuse. Kuna kupata elimu, kuna kupata exposure, kuna kuwa na akili zinazokuwezesha kutambua fursa. Sasa si kila mtu ana uwezo wa kupata exposure au kuwa na akili za kutambua fursa. Wengine inabidi waende shule. Through kwenda shule inategemewa kwamba unaweza ukapata exposure na pia ukanoa akili kuweza kutambua fursa. Lakini tatizo lililop TZ ni kwamba alimu yetu ipo specifically kwa ajili ya kumkaririsha mtu haimjengi kuwa mbunifu na kuwa na uwezo wa udadisi wa kutambua fursa. Unapotoa mfano wa Bill Gates au Mark Zuckerberg ina apply vipi kwa kijana aliyezaliwa namtumbo amabeye kuuona mlo mmoja kwa siku na shida. Sasa utamshauri huyo kijana asiende shule? Huyo kijana hana role models waku mu inspire sasa utashauri asiende shule. Mark au Bill wamekulia mazingira tofauti. Wamekuwa exposed kwenye computers toka wadogo wameona fursa toka wakiwa wadogo kwa hiyo elimu kwao haikuwa kitu cha msingi sana ili kusonga mbele. Barkhesa aliona fursa tangu akiwa kijana. Alibarikiwa kuwa na akili ya kuziona hizo fursa na ni wachche sana wenye kipaji cha kuona fursa bila kupitia kwenye elimu. Watu kama Barhkesa tunasema wapo gifted. Si kila mtu anaweza kuwa na akili za za huyu jamaa bila kupitia shule. Kwa hiyo tuangalie tusipoteshe watu. Kufanikiwa au kutofanikiwa inategemea na mtu na mtu. Elimu inkupa chance atleast lakini ukishindwa kuziona fursa hata baada ya kuelimishwa tena hutakiwi kuilaumu elimu. Elimu imekupa nyenzo zote muhimu unazoweza kuzitumia kuona fursa. Mfano hapa watu wanapoteza muda mwingi sana jamii forums lakini hawajui hiyo privillege ya internet access waliyonayo inaweza kuwafanya kuwa matajiri sana.:becky:
 
Kuna vitu vichache mtoa mada ana confuse. Kuna kupata elimu, kuna kupata exposure, kuna kuwa na akili zinazokuwezesha kutambua fursa. Sasa si kila mtu ana uwezo wa kupata exposure au kuwa na akili za kutambua fursa. Wengine inabidi waende shule. Through kwenda shule inategemewa kwamba unaweza ukapata exposure na pia ukanoa akili kuweza kutambua fursa. Lakini tatizo lililop TZ ni kwamba alimu yetu ipo specifically kwa ajili ya kumkaririsha mtu haimjengi kuwa mbunifu na kuwa na uwezo wa udadisi wa kutambua fursa. Unapotoa mfano wa Bill Gates au Mark Zuckerberg ina apply vipi kwa kijana aliyezaliwa namtumbo amabeye kuuona mlo mmoja kwa siku na shida. Sasa utamshauri huyo kijana asiende shule? Huyo kijana hana role models waku mu inspire sasa utashauri asiende shule. Mark au Bill wamekulia mazingira tofauti. Wamekuwa exposed kwenye computers toka wadogo wameona fursa toka wakiwa wadogo kwa hiyo elimu kwao haikuwa kitu cha msingi sana ili kusonga mbele. Barkhesa aliona fursa tangu akiwa kijana. Alibarikiwa kuwa na akili ya kuziona hizo fursa na ni wachche sana wenye kipaji cha kuona fursa bila kupitia kwenye elimu. Watu kama Barhkesa tunasema wapo gifted. Si kila mtu anaweza kuwa na akili za za huyu jamaa bila kupitia shule. Kwa hiyo tuangalie tusipoteshe watu. Kufanikiwa au kutofanikiwa inategemea na mtu na mtu. Elimu inkupa chance atleast lakini ukishindwa kuziona fursa hata baada ya kuelimishwa tena hutakiwi kuilaumu elimu. Elimu imekupa nyenzo zote muhimu unazoweza kuzitumia kuona fursa. Mfano hapa watu wanapoteza muda mwingi sana jamii forums lakini hawajui hiyo privillege ya internet access waliyonayo inaweza kuwafanya kuwa matajiri sana.:becky:
 
Back
Top Bottom