Kingmairo
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 4,936
- 3,542
nakubaliana na wewe kabisa,mimi nina ushuhuda ulio hai,baada ya kumaliza shule ya msingi kuna wenzangu wengi hawakubahatika kuendelea na sekondari wakaamua kutafuta fedha,tulipomaliza kidato cha nne wenzetu wakawa tayari na mitaji inayoweza kuwasafirisha miji mbalimbali kwa biashara,wakati tunamaliza chuo na kukosa ajira wenzetu walikuwa tiyari wana miliki majumba sehemu tofauti hapa tz sisi tuliona haya ya kufanya bishara ambazo ndio ziliwanyanyua wenzetu,......leo hii tuliosoma nao primary wanamiliki viwanda na maghorofa kariakoo,wa sekondari wanafanya shughuli za kipato cha chini,wa chuo wameathirika kwa kutaka vitu vya kufikirika.......wengi huchagua kazi na kudai hakuna, ajira which is not true.
Mkuu hilo darasa lenu lina bahati sana basi, yaani wote waliodrop shule wana magorofa na viwanda!!? Kifupi watu tunapenda kuangalia mafanikio ya wachache na kugeneralize. Ni asilimia ndogo ya wanaodrop shule hasa primary huja kuwa na mafanikio. Wengi wao huchapika tu kwa sana. Someni ndugu zangu, hakuna anayenyimwa kuingia kwenye private business akishasoma lakini hakuna anayeweza kurudi shule mda ukishampita.