Ukitaka kuwa tajiri, usiende shuleni

Ukitaka kuwa tajiri, usiende shuleni

nakubaliana na wewe kabisa,mimi nina ushuhuda ulio hai,baada ya kumaliza shule ya msingi kuna wenzangu wengi hawakubahatika kuendelea na sekondari wakaamua kutafuta fedha,tulipomaliza kidato cha nne wenzetu wakawa tayari na mitaji inayoweza kuwasafirisha miji mbalimbali kwa biashara,wakati tunamaliza chuo na kukosa ajira wenzetu walikuwa tiyari wana miliki majumba sehemu tofauti hapa tz sisi tuliona haya ya kufanya bishara ambazo ndio ziliwanyanyua wenzetu,......leo hii tuliosoma nao primary wanamiliki viwanda na maghorofa kariakoo,wa sekondari wanafanya shughuli za kipato cha chini,wa chuo wameathirika kwa kutaka vitu vya kufikirika.......wengi huchagua kazi na kudai hakuna, ajira which is not true.

Mkuu hilo darasa lenu lina bahati sana basi, yaani wote waliodrop shule wana magorofa na viwanda!!? Kifupi watu tunapenda kuangalia mafanikio ya wachache na kugeneralize. Ni asilimia ndogo ya wanaodrop shule hasa primary huja kuwa na mafanikio. Wengi wao huchapika tu kwa sana. Someni ndugu zangu, hakuna anayenyimwa kuingia kwenye private business akishasoma lakini hakuna anayeweza kurudi shule mda ukishampita.
 
Kuhusu Bill Gates na Mark Zuckerberg wa facebook.
Hawa mabilionea sio kama hawakusoma bali hawakumaliza masomo yao ili waendeleze project zao.

ukiwa makini utaona tofauti iliyopo kati ya mtu asiyeenda shule kabisa na yule aliyeenda kisha akaacha mwaka wa mwisho wa masomo. Wote hawtokuwa na vyeti lakini vichwani watakuwa tofauti.

Bill na Mark walianzisha prjects zao kutokana na knowledge waliyoipata kutoka chuoni.(ingawa hawakumaliza mwaka miaka ya masomo iliyowekwa na chuo)

hivyo Bill na mark hawana vyeti lakini wamesoma ingawa hawakumaliza miaka iliyopangwa. tena walisoma katika chuo bora kabisa duniani, Havard University.

Vijana mnaosoma hii thread ni vizuri mkainoti hii.

Nchi zilizoendelea kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya computer na electronic wanafunzi wangali mashuleni au vyoni huwa wanaanza project zao na miradi midogomidogo hata wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa wakufunzi wao.

Wakati nilipokuwa chuo second year huko Marekani, nikapahatika kupata kibarua cha kufundicha full time computer teacher kwenye madarasa ya Jr na Senior classes. Nilichokishuhudia kulikuwa na vijana watatu ambao walionekana wanajua elimu ya computer isivyo kawaida na wana projects zao, ingawa darasani hawakutaka kuonyesha umahiri huo, walikuwa wanaiita baada ya darasa kwa mashauriano binafsi tu na pengine hata wazaziw ao walikuwa wanakuja kuniuliza mafanikio ya matarajio yao.

Walichoniambia hao teenage watatu ni kuwa wanachohitaji pale highschool ni certificate ya complition tu kwa mataka ya federal requirement katika employement, lakini walicho nacho ni zaidi ya wanachokisoma pale. Hiyo ni dalili tosha kwamba kuna wenye upeo wa juu katika kuelewa mambo maana yake talented people hawahitaji hii elimu tunayohangaikia wengine, sio wengi ni wachache. Wengine wako sawa tu kuanzisha miradi mingine ya kawaida maisha yakawaendea vizuri kuliko kupotezea muda huko vyuoni ambako kwa ulimwengu wa sasa hakuna uhakika katika ajira.
 
Si kweli asilimia kubwa ya majiri ni wasomi na sio hao wachache wanao onyeshwa kama mfano angalia nchi yeyote wenye kipato cha juu asiliamia 25% utapata wasomi zaidi kuliko wale ambao hawajasoma. Wasomi nina maana ya degree moja au advance diploma. Kama unaangalia mabilionea wachache kuna ambao hawajasoma lakini mabilionea wako wangapi??. Mfano kama mtu ulikuwa unatengeneza $40,000 kwa mwaka na sasa natengeneza $78,000 hata kama si tajiri ni bora sana na maisha yangu yamebadilika. vilevile mambo ambayo naweza kufanya sijazuiwa na mtu kufanya kama biashara. Hao ma professor unaoongelea ni wachache watu wengi hawaendi shule kutafuta PHD kwani PHD inapatikana kwa research na wengi wao hawajawahi kufanya kazi za kawaida hivyo hawaendi kwenye PHD kwasababu ya utajiri

Tatizo linalowaliza wasomi ni makato makubwa katika mishahara yao. Wastani katika nchi nyingi pato la wenye elimu ya juu makato hufikia 33% - 35%, labda kwa Tanzania na chini nyingi za Kiafrika ndio inaweza kuwa chini ya kiwango hicho. Unaona wenye pato kubwa ndio walipaji wakubwa wa kodi na kinachosalia mkononi ukilinganisha na mazingira ya maisha yao ya kila siku kwa standard ya maisha yao inapifika mwisho wa mwezi pengi linaonekana wazi likidao pay check nyingine kama hana mpango wa kubana matumizi.
 
Hapa hakuna maswala ya kuandikiwa na Mola dogo, fanya kazi, the world is not fair...
Mola anamsaidia anayejisaidia. ndo maana akasema asiyefanya kazi na asile.

Hey you guys nimisema mambo ya mungu u dnt mean u just seat an relax ili mambo yawe yawezekana hamjielewi nani alikwambia shile inadanganya jaribu uone.usiishi maisha ya kuiga utachekwa fanya unachoweza utoke mbona mnakua wavivu wa kufikiri.usikurukupuke kujibu kitu kama hujui undani wake.this is for u NDIBALEMA and u LUKANSOLA
 
Mimi nafikiri wewe mwenyewe ndiyo unajichanganya! Kusema hakuna Professor Billionea ni makosa maana hakuna mtu alaiyesema unavyozidi kusoma ndiyo unazidi kuwa tajiri bali wahenga wanasema ukisoma unauhakika zaidi wa kuwa na maisha mazuri. Hivyo badala yake hapo juu ungetutajia mfano wa Maprofessor ambao ni masikini ili utushawishi tusisome na sisi.

Kuna Professor masikini unamjua hata mmoja?

Wapo wengi tu.
 
1533689_10152252297754857_1826467082_n.jpg

Ukiwa na migomba yako haikatwi kodi ni mali yako, kila penny ya mshahara hukatwa kodi

Mleta hoja ana hoja nzuri pengine tunaichukulia kiulaini mno au kimtazamo kuwa kusoma sana ndiko kunakolipa ingawa tumeshuhudia si kila aliyesoma sana anafanikiwa kuelimika.

Elimu ya msingi ni kujua kusoma na kuandika
Maana ya hoja yangu hapo ni kwamba kwa mwenye upeo mzuri wa upongo akishajua kusoma na kuandika ulimwengu utakuwa umeshamfungukia mradi tu anautumia vema ubongo wake na kuwa mbunifu mzuri wa kuyatengeneza maisha yake. Makato ya wafanyakazi ndiyo yaliyojenga majengo marefu hapo Dar na kwengineko duniani lakini wenyewe wamebaki taabani baada ya kustaafu, wachache tu ndio waliokuwa na akili mbili za kuyaweka sawa mazingira yao mazuri baada ya kustaafu.

Kisa cha Mmarekani Thomas Edson kuachishwa shule ndani ya miezi mitatu tu kwa sababu ya utukutu, uvumilivu wa mama yake ni kumfunza mtoto wake kujua kusoma na kuandika, angalia hilo tu lilivyomsalidia kukuza bongo lake na kuvumbua mambo makubwa ambayo leo tunayafaidi duniani kama hisi battery, bulbs, vyombo vya muziki nk.

Mfumbuzi wa Apple aliyefariki miaka michache iliyopita vyuo kadhaa aliviruka kihunzi na kaumua kutuliza bongo lake na angalia sasa teknolojia yake inavyotesa kwenye ulimwengu wa computerization na mobile phones.

Sina maana mbaya kusema wavivu wa ubunifu ndio wanaofikiri kusoma sana ndio kutawafikisha kwanye mafanikio, ingawa wachache wao wamefanikiwa. Wengi wamejutia kushuhudia muda mwingi waliomaliza huko vyuoni na kurudi wakitangatanga mitaani kutafuta kazi wakati wenzao walishasetirika na maisha yanawaendea vizuri tu. Baya zaidi hao wasomi badala ya kutulia katika fani zao, kwa sababu ya kuona kile wanachokipata hakifikii ndoto zao ndio wimbi la kukimbilia kwenye siasa ambako inaonekana ni kuchota bila jasho.

Unachokipata kwenye siasa kinakodolewa macho na kila mlipa kodi unakila huku ukisimangwa, raha gani hii ya kuchumia majukwani na kula kwa kusimangwa badala ya kuchumia juani kiulaini unakitelemshia kinywani ukiwa kivunili bana.
mkuu ni kweli we upo makini una fikra pevu.
 
Swala sio kutokwenda shule,huyo robert kiyasaki mwenyewe alikwenda shule na akafanya kazi za kuajiriwa in different companies akisisitiza alikua akipata experience ya management ya human resources e.t.c.na mwisho wa siku anasisitiza if u like to do the job remember to mind ur own business.So tukirudi kwenye mazingira yetu ya kibongo ukipata kazi ya mshahara mkubwa unapata nafasi kubwa ya kupata mtaji mkubwa kirahisi ukizingatia kupata mtaji ni problem so ukiwa mjasiriamali unapiga bao kirahisi!!So shule inasaidia mentally even kupata capital easily so big deal kwa waajiriwa is to mind ur own business
 
Mkuu uko sahihi lakini umeweka heading yako vibaya. Elimu ndio moyo wa nchi yoyote ile. Ulitakiwa useme kuwa soma angalau degree moja au mbili then jiajiri. Elimu + kujiajiri ni mafanikio, ndio maana utaona darasa la saba waliowengi uishia kufuata bidhaa kwa Muhindi, lakini kwa kuwa Muhindi kasoma anaweza hata kuingia mtandaoni na kufanya biashara na watu wa nje ya nchi, wanamletea mzigo na anawauzia wenye maduka wa darasa la saba. Iko wazi kuwa ukisoma sana unakuwa ni wa kufanya analysis sana kabla ya kuwekeza, kitu ambacho ni kibaya. Ndio maana wale wanaopata A darasani wanaogopa kuwekeza kwa kuwa hawajazoea kufanya makosa, ndio maana huwa wanapata A.

Hasara za kutosoma kabisa, mfano angalia jamii za wafugaji wanamiliki ng'ombe 800 lakini kwa kukosa elimu anashindwa ku convert hao ng'ombe na kwenda kwenye utajiri, wengi wao uishia kulala kwenye ngozi na kuishi maisha ya ovyo
 
Nimelazimika kuingilia kati huu mjadala maana nadhani kuna mambo ya msingi ya kuzingatia wakati unapozungumzia KWENDA SHULE vs KUWA TAJIRI vs MAISHA MAZURI.

Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kwenda shule na kuwa tajiri, wala hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuwa tajiri na kuishi maisha mazuri na ya furaha. Mimi nadhani lengo la binadamu sio KUWA TAJIRI bali ni KUISHI MAISHA MAZURI YENYE FURAHA. Ni ukweli usiopingika kwamba kuna baadhi ya watu hawakwenda shule na ni matajiri, lakini pia kuna watu wengi zaidi ambao wamekwenda shule na wanaishi maisha mazuri japo sio MATAJIRI. Na pia ni ukweli usiopingika kwamba kuna watu wengi MATAJIRI lakini wanaishi maisha ya HOVYO ambayo hayana furaha.

Mimi binafsi nadhani kwenda shule kumesaidia sana kuwainua watu wengi sana waliotokea kwenye familia duni na kuwapa nafasi ya kupata mafanikio kimaisha kuliko wale ambao hawakwenda shule. Nadhani ni makosa kuchukua mifano ya watu wachache WALIOBAHATISHA utajiri bila kusoma na ku generalize kwamba kila mtu anaweza kuwa tajiri bila kwenda shule, wakati kuna mamilioni ya watu ambao hawakusoma na ni MASIKINI. Ikumbukwe pia kwamba sio kila mtu anaweza kufanya biashara na kufanikiwa! Wapo watu wengi (waliosoma na wasiosoma) ambao huanzisha biashara kila siku, lakini sio wote wanaofanikiwa.

Kwa karne hii tunayoishi nadhani ni upotofu kusema "kama unataka kuwa tajiri usiende shule" halafu unatoa mifano ya akina bill gates ambao kiuhalisia, utajiri wao umetokana na KWENDA SHULE, bila kuangalia tofauti za kimazingira. Mimi naona kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa mtu aliekwenda shule kuishi maisha mazuri na ya furaha kuliko mtu ambaye hakwenda shule.
 
Hey you guys nimisema mambo ya mungu u dnt mean u just seat an relax ili mambo yawe yawezekana hamjielewi nani alikwambia shile inadanganya jaribu uone.usiishi maisha ya kuiga utachekwa fanya unachoweza utoke mbona mnakua wavivu wa kufikiri.usikurukupuke kujibu kitu kama hujui undani wake.this is for u NDIBALEMA and u LUKANSOLA



Samahani sana mkuu nisamehe, namuombea msamaha ndugu yangu Ndibalema pia.
 
Last edited by a moderator:
Kwa majibu hayo kwenye red yamejitosheleza.
Ndio maana Waafrika wengi ni masikini ni kwa sababu ya mawazo mgando kama hayo ya IBM2014

Sidhani kama hata anaelewa kinachojadiliwa hapa, halafu badala ya kujifunza analeta usharobaro tu hapa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu uko sahihi lakini umeweka heading yako vibaya. Elimu ndio moyo wa nchi yoyote ile. Ulitakiwa useme kuwa soma angalau degree moja au mbili then jiajiri. Elimu + kujiajiri ni mafanikio, ndio maana utaona darasa la saba waliowengi uishia kufuata bidhaa kwa Muhindi, lakini kwa kuwa Muhindi kasoma anaweza hata kuingia mtandaoni na kufanya biashara na watu wa nje ya nchi, wanamletea mzigo na anawauzia wenye maduka wa darasa la saba. Iko wazi kuwa ukisoma sana unakuwa ni wa kufanya analysis sana kabla ya kuwekeza, kitu ambacho ni kibaya. Ndio maana wale wanaopata A darasani wanaogopa kuwekeza kwa kuwa hawajazoea kufanya makosa, ndio maana huwa wanapata A.

Hasara za kutosoma kabisa, mfano angalia jamii za wafugaji wanamiliki ng'ombe 800 lakini kwa kukosa elimu anashindwa ku convert hao ng'ombe na kwenda kwenye utajiri, wengi wao uishia kulala kwenye ngozi na kuishi maisha ya ovyo

Kama kuna elimu ambayo nilifikiriaa madarasa hayo niliona nimepotea njia na kupoteza muda wangu ndio hiyo elimu ya GRADUATE COLLEGE, bora undergraduate unapata elimu ya kuishia. Hizi graduate school zinawafaa wasio na uwezo wa kupambanua mambo hivyo waende kujifunza kubishana, maana huko ni madarasa ya kubishana na kama hoja ni hoyo ndicho tunachofanya hapa JF ni chuo kikuu cha PHD, asiyefika graduate school hatanielewa, lakini waliopitia huko tanishona midomo.

Undergraduate wanachuoa hujifunza mengi, lakini graduate wanachuo hushinda wanabishana tu, kwa asiyejua kujenga hoja na kuitetea kama tufanyavyo hapa aende huko akapoteze miaka miwili hadi minne na atarudi hutakuta ana hoja kuzidi ya tunazoleta hapa. Tunao wengi hapa ambao ni graduate na ambao ni undergraduate unaweza kutofautisha kwamba hoja imetolewa na graduate? Sanasana hutumia vidokezo vya lugha ili kuwanyamazisha wasiojua lugha.
 
Not real!nianze na wewe,vp wewe umeenda/ulienda shule?je kama una watoto hutawapeleka shule ?shule ni muhimu ndugu!!!!Tatizo aina ya elimu inayotolewa,je inamuandaaje mtu kukabiliana na mazingira yake?Elimu ya Tanzania inamfanya mtu awe tegemezi sababu wazazi huwalazimisha watoto wasome lakini hawajui watoto wana vipaji gani,unakuta mtu anamaliza form4 hajui hata atasoma nini advance, wengi wanachaguliwa masomo ya kusoma na kufuata mkumbo!hivohivo hadi chuo mtu anachagua kozi kutokana na kuangalia fulani alisoma hivo atakua dependant na hawezi kuwa na akili ya kijasiriamali na hawezi kuwa tajiri!! Lakini wazazi wakiwachunguza watoto wao wakiwa wadogo na kuona wanapendelea nini na kuendeleza kipaji cha mtoto tangu akiwa mdogo hakika kutakuwa na matajiri wengi sana!! maana vipaji vingi vinakufa udogoni..Na vipaji vinaendelezwa na SHULE!!!so shule ni muhimu ndugu!!!hata hao mabilionea unaowaona wanapata ushauri kwa walionda shule!!!
 
Mkuu uko sahihi lakini umeweka heading yako vibaya. Elimu ndio moyo wa nchi yoyote ile. Ulitakiwa useme kuwa soma angalau degree moja au mbili then jiajiri. Elimu + kujiajiri ni mafanikio, ndio maana utaona darasa la saba waliowengi uishia kufuata bidhaa kwa Muhindi, lakini kwa kuwa Muhindi kasoma anaweza hata kuingia mtandaoni na kufanya biashara na watu wa nje ya nchi, wanamletea mzigo na anawauzia wenye maduka wa darasa la saba. Iko wazi kuwa ukisoma sana unakuwa ni wa kufanya analysis sana kabla ya kuwekeza, kitu ambacho ni kibaya. Ndio maana wale wanaopata A darasani wanaogopa kuwekeza kwa kuwa hawajazoea kufanya makosa, ndio maana huwa wanapata A.

Hasara za kutosoma kabisa, mfano angalia jamii za wafugaji wanamiliki ng'ombe 800 lakini kwa kukosa elimu anashindwa ku convert hao ng'ombe na kwenda kwenye utajiri, wengi wao uishia kulala kwenye ngozi na kuishi maisha ya ovyo

mkuu nisingeweka iyo heading ningesoma mimi na mke wangu tuu.hakuna mtu angepata maudhui.na kujadili hii mada
mi ni mdau wa elimu ila tumekosa elimu ya finance
 
Not real!nianze na wewe,vp wewe umeenda/ulienda shule?je kama una watoto hutawapeleka shule ?shule ni muhimu ndugu!!!!Tatizo aina ya elimu inayotolewa,je inamuandaaje mtu kukabiliana na mazingira yake?Elimu ya Tanzania inamfanya mtu awe tegemezi sababu wazazi huwalazimisha watoto wasome lakini hawajui watoto wana vipaji gani,unakuta mtu anamaliza form4 hajui hata atasoma nini advance, wengi wanachaguliwa masomo ya kusoma na kufuata mkumbo!hivohivo hadi chuo mtu anachagua kozi kutokana na kuangalia fulani alisoma hivo atakua dependant na hawezi kuwa na akili ya kijasiriamali na hawezi kuwa tajiri!! Lakini wazazi wakiwachunguza watoto wao wakiwa wadogo na kuona wanapendelea nini na kuendeleza kipaji cha mtoto tangu akiwa mdogo hakika kutakuwa na matajiri wengi sana!! maana vipaji vingi vinakufa udogoni..Na vipaji vinaendelezwa na SHULE!!!so shule ni muhimu ndugu!!!hata hao mabilionea unaowaona wanapata ushauri kwa walionda shule!!!

mkuu umeanza na not real.lakini mawazo yako yanaendana na great thinkers like me kuwa mfumo wa elimu ni mbovu
 
Nafikiri hoja ya mtoa mada hapa ni HAKUNA UHUSIANO WA KARIBU KATI YA KUSOMA SANA NA KUWA TAJIRI. Kwa mifano aliyoitoa na mingine mingi watu waliofanikiwa sana na kuwa matajiri hawana elimu kubwa sana.
Mfumo mbovu wa elimu unaandaa waajiriwa ambao kama wakibahatika kupata kazi wataishi maisha ya kusukuma siku na kulipa bili, ila uhuru wa kifedha ni mgumu sana. Nadhani wafanyakazi kwa asilimia kubwa wanalipitia hili kwa kujikuta mishahara haikutani na gharama za maisha haziendani na kipato cha mshahara.
Lakini wale ambao hawakupata elimu kubwa ya kuwashawishi kuajiriwa wanatafuta njia nyingine za vipato mbali na ajira. Hapa ndipo wanapoingia kwenye biashara na uwekezaji na kutengeneza uhuru wao wenyewe.

Tunaondoka na ushauri gani hapa?
1. Ni muhimu kwenda shule au kupata mfumo wowote wa elimu ambao utakuweka sawa na mwenendo wa dunia hii. Binafsi naamini elimu kubwa niliyowahi kuipata kwenye maisha yangu ni kujua kusoma na kuandika. Kwa kujua hivyo tu nimeweza kujifunza vitu vingi sana mimi mwenyewe. Hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kupata elimu ya mambo ya msingi kama KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU.
2. Tusome alama za nyakati. Mambo yamebadilika sana sasa, ajira zimekuwa ngumu kupatikana na ngumu kufanyika pia. Usalama wa ajira uliokuwa ukipatikana zamani kwa sasa haupo tena na upandaji wa gharama za maisha hauendani na ongezeko la mshahara.
3. Tuanze kuangalia njia nyingine za kipato tofauti na ajira. Anza kujifunza na kufanya biashara ili kuondoka kwenye utumwa wa ajira. Kama bado unatafuta ajira na hujapata badili mtazamo wako mara moja na uanze kujikita kwenye njia nyingine za kutengeneza kipato. Kwa mengi zaidi unaweza kutembelea AMKA MTANZANIA na ukajiamsha kutoka usingizini.
 
Mpenzi msomaji je ushawahi kukaa chini na kujiuliza ni ma professor wangapi ma billionaire duniani?,au waalimu? ambao ndo wataalamu wa kufikiri inavyosadikika?,
Hawa ndo chanzo cha umaskini..sina maana kwamba nawachukia au nawadharau la hasha ila ni kutokana na mifumo mibovu ya elimu iliyopo nao ndo wanaihubiri au kuisimamia.
kivipi?,
Mara nyingi tumesikia haya maneno.MWANANGU/MWANAFUNZI SOMA SANA PATA MAKSI ZA JUU ILI UJE KUPATA KAZI NZURI YENYE MSHAHARA MKUBWA.
huu ni ujinga kwa sababu mtu akiajiriwa una kuwa na usalama wa kazi tuu lakini unakuwa hauna uhuru wa kiuchumi{financial freedom}.
unapoajiriwa na kampuni unafanyia kazi watu wengi ambao mnagawana nao mshahara pasu kama hivimshahara wako unakatwa haya kabla hujapokea.:
kodi ya serikali
makato ya bima
makato ya benki
makato ya vyama vya wafanyakazi
Alafu ndo unapokea hela yako ndo maana tumesikia wafanyakazi wengi wakilia sana juu ya makato kuwa ni makubwa sana..baada ya hapo unakwenda nyumbani na iyo hela ambapo zinakwenda katika vibobo vya kukutia umaskini ili urudi tena kazini ambavyo ni kodi ya nyumba .maji.umeme na ada za watoto na kama muflisi gari unanunua mafuta na ku li lipia kodi zake.
Huenda ujanipata vizuri sasa utanipata nachomaanisha.
Ni kuwa huyu mwajiriwa hana vitega uchumi miradi ambayo ingemuingizia pesa za kutosha maisha yake yote ndo maana baadhi ya waajiriwa wanapo staafu hufa gafla kwa sababu ya ukkata.
EMBU TUMUANGALIE MWEKEZAJI.
WAWEKEZAJI WENGI MA BILIONAIRE HAWANA DEGREE KWA MFANO.
BAKHRESA WA AZAM
PATRICK NGOWI.TAJIRI MTOO NAMBA MOJA TANZANIA
BILL GATE WA MICROSOFT
JOHN D ROCKEFELA WA STANDARD OIL OF AMERICA
MARK WA FACEBOOK
na wengine wengi unaweza ni PM.
Ma investor wote unajua wanakatajwe kodi?
ni baada ya kutoa garama zote za uendeshaji na ile faida iliopatikana ndo inakatwa kodi.
Mpenzi msomaji bwana HENRY FORD aliwahi kusema thinking is the hardest work there is that is why so few people engage in it.
2;:Wapendwa wasomaji nimepata PM nyingi sana wakitaka vitabu vya Robert kiyosaki na nimewapatia in terms of soft copy na audio.kama na wewe unataka njulishe ntakutumia kwa e mail au basi au njia yoyote ile. nicheki weyosi@yahoo.com


Unajichaganya, heading inasema ukitaka kuwa tajiri usiende shule halafu unauliza maprofesa wangapi ni mabilionea na kisha unataja mabilionea ambao hawana degree, kwa hiyo kupata degree pekee ndio kwenda shule? Wenye Diploma, Vyeti n.k hawajaenda shule?

Bill Gates alikuwa Havard kabla ya kuacha na kuanzisha Microsoft. Mark Zuckerberg alianzisha Facebook bwenini kwake Havard na Michael Dell alianzisha Dell Computers akiwa anasoma Chuo kikuu cha Texas, Austin kabla ya kuamua kuacha masomo na kujikita kwenye biashara. Hawa huwezi kusema hawakwenda shule na naamini kwenda kwao shule ndio kuliwasaidia mpaka kufanikiwa.

Mwisho hapa chini nakupa majina ya mabilionea wanne maarufu ambao wana degree:

1. Michael Bloomberg ( Bloomberg L.P, Utajiri wa Dola bilioni 27) - Electrical engineering/Business Administration

2. Phil Knight ( NIKE, utajiri wa Dola bilioni 14) - Business Administration

3. Oprah Winfrey ( OWN, utajiri wa Dola bilioni 2.8) - Communications

4. Jeff Bezos ( Amazon, utajiri wa Dola bilioni 25) Electrical engineering/computer science
 
Back
Top Bottom