Maisha ni kama movie na MUNGU ndie director. Sisi wanadamu huwa tunaamini tunajiamulia maisha yetu kwenda vile tunataka ila si kweli.
Maisha MUNGU anayaunda mwanzo hadi mwisho, kazi yetu ni kuplay role anazotupa. Ukijipangia roles zako lazima maisha yako yawe full of complications na pain.
Ni kama movie , director anapompa actor movie huwa anataka afuate script aliyo muandikia. Actor akileta ujuaji na kuigiza anavyotaka na kuwa na script yake kinyume na ile ya story ya director then hiyo movie itaharibika.
Maisha especially ya mahusiano yanataka matumizi ya hekima ya asili ingawa watu hutumia busara eneo la hekima. Ushawahi kutana na binti mzuri kwa muonekano anakazana kwenda kanisani kufuata maombi ya ulinzi wa kupata mume mwema kwaajiri yake?!
Dhamira yake ni nzuri ila mbinu zake ndizo zina walakini. Swala hapo hajatumia hekima bali katumia busara kufanya maamuzi. Hekima inakulinda katika nyakati, busara inakusaidia usipokuwa na hekima. Hekima inataka utulivu wa akili na hakuna mwanadamu atakupa hekima ila MUNGU pekee ndio atakupa hekima. Mwanadamu mwenye hekima atakupa busara ukifuata hekima yake, ila busara haidumu vizazi na vizazi sababu ni zao la hekima ya wakati au nyakati fulani.
So kwa kumalizia, mleta mada, jifunze jambo moja, hayo uliyosema ni maneno ya busara sana tena sana. Ila yamekosa uhalali wa hekima ndani yake. MUNGU hafundishwi wala kupangiwa utendaji wake. Akishakuletea mtu wewe ukaleta ufundi matokeo yake ndio yale ya kusema wanaume ni wanyama, au siku hizi hakuna wanawake wa kuoa.
By the way.... First love wako unatakiwa umjue kuanzia miaka 16 hadi 20. Hapo baada ya 20, experience za vurugu za kimahusiano zinakuondoa katika nafasi ya kuielewa asili ya mwanadamu katika mapenzi na mahusiano. Imagine leo kuna mwanamke ukimpenda na kumjali anakuona mjinga na kilaza atatafuta mwanaume wa kumpa stress kisha aje kuomba ushauri.
Pia unaweza mpenda mwanaume kuliko chochote ila akakuona mzigo na kero muda mwingine sababu ya attention unayompa. Haya yote ni matokeo ya kujihusisha na watu wengi kimahusiano katika safari ya maisha.
Sent from my JKM-LX1 using
JamiiForums mobile app