Ukitoka kidogo nje ya nchi na ukarudi kwenye viwanja vyetu vya ndege utatamani kulia machozi

Nakumbuka miaka ile ya 90 nilikuwa naenda airport dar kuangalia midege ya KLM, BA,SWISS Air, SABENA nk. Sijui kama yote yanakuja
 
Wewe imewahi kutua chato international airport pale kitobuni m wa utalii kanda ziwa?
 
Nenda tu hata hapa Kenya, Ethiopia, Africa ya Kusini nk
Mkuu Kenya ni conneting hub, mashirika mengi ya ndege yanatua Kenya na kuunganisha safari nyingine kwenda mahala pengine.

Ndio maana safari za ndege Nairobi ni nyingi sana kuliko Dar es Salaam. Ethiopia the same.

Afrika kusini ni nchi iliyoendelea mkuu, huwezi kuilinganisha na Tanzania. Miundombinu yao ya barabara, viwanja vya ndege ni level nyingine kabisa. Nchi inapata watalii 9m kwa mwaka na kabla ya covid ilikua inapata zaidi ya 10m kwa mwaka huku sisi tukiambulia 1m hadi 1.5m kwa mwaka.

Kutokua busy kunasababisha uwanja wetu wa Mwalimu Nyerere kukosa huduma za kisasa, mfano pale airport hakuna free wifi, hii ni huduma ya msingi airport lakini JNIA sijawahi kupata free wifi pale.

Bado tuna safari ndefu sana ya kwenda.
 
Shida ni mashirika kujaza ndege au wasafiri? Maana mashirika yasije kujaza ndege hapo air port halaf nyny watanzania munaogopa kusafir, me nadhan siku wasafiri/watalii wakiwa wengi na ndege zitakuwa nying ili kuendana na kasi ya watu,
Utakuta watanzania wengi wakija toka nje ya nchi lazima wapite Kenya. Kama kuna wasafiri wa kutosha toka Nairobi kuja Dar au KIA basi tungeweza kuwa na Direct flights kama mambo yakiwekwa vizuri
 
Viwanja vya ndege ambavyo kwa kiasi fulani viko busy hapa kwetu ni pamoja na JKIA, KIA, SONGWE, Z'BAR, BUKOBA, MWANZA... kwingineko pia lakini umaskini ni chanzo kikubwa cha kufanya viwanja vyetu kuwa utupu muda mwingi, na tunategemea route za nje kuliko za ndani ambazo zingeweza kuongeza route za ndege. Serikali upunguze siasa katika mambo haya.
 
Songwe ipo busy? Au mimi sielewi maana ya busy?
 
Shida uchumi wa wananchi wa Tanzania ni mdogo katakana na wizi wa wanasiasa. Ili usafiri wa Anga uweze kuwa profitable ni lazima uchumi wa wazaqa wa nchi husika uwe vizuri. Na ili uchumi uwe vizuri laziwa nchi iwe na utawala wa sheria. Sasa hivi Tanzania hela Zina thamani kuliko kitu chochote ikiwemo mdaa. Usafiri wa anga hauwezi kuwa biashara kwenye nchi isiyo Jari mda .
 
Uchumi uko chini, kusafiri na kusafirisha mizigo ni indicator ya ukuaji wa uchumi

Tuliambiwa royal tua ilateleta watalii wengi labda secta hii inaweza kuleta ndege nyingi nchini
 
Vyoo vinanuka!
Upatikanaji wa maji ni mdogo sana.
Customer services za uhamiaji na wasimamizi wa kiwanja ni hovyo hovyo hovyo.
Mashine, vifaa, kulivyo ni kama umeenda Afghanistan!
Bure, zero, hovyo, aibu...
 
Shida ni mashirika kujaza ndege au wasafiri? Maana mashirika yasije kujaza ndege hapo air port halaf nyny watanzania munaogopa kusafir, me nadhan siku wasafiri/watalii wakiwa wengi na ndege zitakuwa nying ili kuendana na kasi ya watu,
Kweli, ila pia bei ziwe rafiki kidogo kwa Watanzania ili waweze kuafford kusafiri na sio kutegemea tu watalii hii nadhani ingesaidia kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…