Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Upeo wako ndugu ni mkubwa kiasi kuutumia kwa mtu anayeamini katika ushirikina ni ku misuse resources!
Ukiangalia watu kwa Mwamposa na makanisani wanavyosaka miujiza ndo utajua safari ni ndefu sana!
 
Mkuu soma biblia toka mwanzo hadi ufunuo kwa makin
then ukimaliza urudie kama mara mbili then uje usome huu uzi uloandika

Uchawi umetajwa sana huko na mambo ambayo walifanya.
Mapepo ya utambuzi n.K
hebu anza leo kufikiri nje ya hayo ma vitabu!
utajikomboa katika mengi.
fikiri hivi: biblia haipo na hujawai kuiskia, unajiridhishaje katika hoja husika!
 
Upeo wako ndugu ni mkubwa kiasi kuutumia kwa mtu anayeamini katika ushirikina ni ku misuse resources!
Ukiangalia watu kwa Mwamposa na makanisani wanavyosaka miujiza ndo utajua safari ni ndefu sana!
Safari ni ndefu sana.

Mara nyingine hata kufanya mazungumzo na mtu anayeamini ushirikina irreedemably kusipomsaidia huyo ninsyeongea naye moja kwa moja, kunaweza kusaidia wengine wanaosoma.
 
Nikikwambia Mimi ni Mungu niliyeumba vyote ila wewe huwezi kujua hilo kwa sababu hiyo ni habari mpya na huwezi kuipima kwa uwezo wako wa kizamani, utakubali?
Nitafuatilia kujua ukweli, lakini siwezi kukataa tu kabla ya kufuatilia.
 
Nitafuatilia kujua ukweli, lakini siwezi kukataa tu kabla ya kufuatilia.
Utafuatilia nini sasa wakati hiyo ni habari mpya na imezidi uwezo wa akili yako kuielewa? Utafuatilia nini?
 
Utafuatilia nini sasa wakati hiyo ni habari mpya na imezidi uwezo wa akili yako kuielewa? Utafuatilia nini?
Nitachunguza mpaka nijiridhishe kuhusu suala hilo na sio kukataa tu huenda wewe ni Mungu kweli manake yawezekana wewe ndiye. Tatizo la watu wengi ni kutofanya utafiti juu ya mambo tuliyoyakuta na kujiridhisha wenyewe. Hupaswi kuingia katika imani yoyote ile unapokuwa mtu mzima bila kujiridhisha. Ndio maana kuna watu wanaacha imani zao na wengine wanajiunga na imani zingine. Nawe fanya utafiti wa haya mambo ya kiroho ujue ukweli wake upo wapi. Kama upo curious sana na hodari nenda hata kwa waganga wa kienyeji kajiridhishe kuhusu uwepo wa masuala ya kiroho na dimensions zisizoonekana.
 
Utafanya utafiti kwa kutumia nini kwenye habari ambayo iko nje kabisa ya uwezo wako kuielewa?
 
nijuavyo mimi ukishaingiza neno* kuamini* umeachana na kuthibitisha!
Mambo ya kiroho tunatembelea kuamini baas!
Tunapoachana ni kwenye mambo ya kuamini.
Ndo hapo tunakutana na wanaoamini kijinga na wanaomini kwa hekima!
Ndo kusema washirikina wanaamini kijinga.
Mbaya zaidi kuna ushirikina asilia na ushirikina ndan ya imani za kimapokeo.
mf ushirikina wa kikristo
 
Kuamini unaamini tu, ukianza habari za kutenganisha kuamini kijinga na kwa hekima itabidi uingie kwenye kuthibitisha imani gani ni ya kijinga na imani gani ni ya hekima.

Na ukishaanza kuingia kwenye kuthibitisha ndiyo ushaanza kuondoka kwenye kuamini. Maana hata hiyo imani yako mwenyewe itabidi uiweke kwenye chujio ujitafakari kama ni ya kijinga au ya hekima, hicho kitendo cha kuichuja tayari ni kupunguza imani, huwezi kuichuja na kuihakiki imani yako kama una imani 100%.

Ndiyo maana mimi sitaki habari za kuamini, nataka habari zinazoweza kuthibitishwa.
 
hebu anza leo kufikiri nje ya hayo ma vitabu!
utajikomboa katika mengi.
fikiri hivi: biblia haipo na hujawai kuiskia, unajiridhishaje katika hoja husika!
NIshafikiria kuwa biblia takatifu haipo
 
Uzuri wa internet utapata chochote ulichokusudia kukipata, ukitaka kupata maelezo yenye kuhusu hakuna uchawi utapata na ukitaka maelezo yenye kuhusu uchawi pia utapata.
 
Yaani hakuna watu wanakera kama wanaoamini ushirikina, ni wagumu sana kushaurika
Tatizo ni moja, mara nyingi wasioamini uchawi wanapojadili kuhusu uchawi huwa huwezi kuona uhusiano wao wa kuishi jamii zenye kujishughulisha na uchawi ndio maana wakielezea huwa wanaelezea kinadharia zaidi na kutumia mifano ileile siku zote katika kupinga uchawi, na anayeamini uchawi yeye anaishi mara nyingi unakuta anaishi kwenye jamii zenye kujishughulisha na uchawi.
 
Hakunaga uchawi isipokuwa kuna UJINGA yaani mtu kushindwa kujua changes mbalimbali za kifizikia na kikemia.


Ovaaa

Ukifa ghafla haujalogwa tunakupima pressure na heart attack n. K tunakupatieni jibu ya kilichokuua
Kwani mkuu ulikuwa unataka mtu apimwe chanzo cha kifo na ikutwe uchawi?
 
Maswali ni mengi kweli, kuna hili la mchawi kukiri kuwa ni mchawi na madhara aliyoya sababisha kwa uchawi.
 
Siamini uchawi, najua it's all psychological games. Ila mleta mada tungeomba utupe resources zaid, au links za kupata hizo evidence ulizoelezea hapo. Like how does it work step to step!
Ni wazi unaishi mbali na jamii zenye kujishughulisha na matendo ya kichawi na ndio maana uchawi kwako inakuwa kama story tu unazozisikia kwa mbali.
 
Mbona kuna madarasa na vitabu kibao tu vya wazungu vyenye kufundisha uchawi na hao wenzetu wameendelea na ni wasomi.
 
Siku zote nasema uganga ungekuwa hivyo basi hadi leo kusingekuwa na kazi ya uganga tena usingekuwa na soko, hivi mkuu wewe ulishawahi kwenda kwa mganga au umeshawahi kushuhudia rafiki au ndugu yako kwenda kwa mganga ili utupe mfano halisi kwa hayo unayoyasema?
 
NIshafikiria kuwa biblia takatifu haipo
binafsi navitambua na kuviheshimu vitabu vinavyodhaniwa vitakatifu kwa dhana moja tu kwamba ni mkusanyiko wa mafundisho yenye hekma na historia za kweli na kufikirika kwa nyakati hizo.
Ili kuvipa nguvu ya kuheshimika na kufwatwa ilibidi itumike mbinu ya ni ...Neno la Mungu
Kinachothibisha Mungu hajawai kuwa na sifa ya kujihusisha na mambo hayo ya kibinadam moja kwa moja, ni uwepo wa vitabu vilivyokinzana hadi kufutwa!
Kwa upande mwingine ni Neno la Mungu kwa misingi ni ujumbe wenyewe kuwa mwema katika kuleta na kujenga mahusiano mazuri kati ya Mungu na viumbe wake wote!
Nikimaanisha hata mafundisho mema ya mila na desturi zetu ni Neno la Mungu
Tofauti ni tu wengine kufanya coding
Ninachokataa ni habari ya Mungu kushusha amri kwenye bango wala kumkabidhi mtume Quran!
Mungu ni simply WEMA kama ambavyo shetani ni simply UBAYA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…