Lububi
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 2,158
- 3,808
Upeo wako ndugu ni mkubwa kiasi kuutumia kwa mtu anayeamini katika ushirikina ni ku misuse resources!Anayesema kitu kipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha kitu kipo.
Kwa sababu kilichopo ndicho kinathibitika kipo.
Kisichopo, nje ya nadharia tupu, hakithibitiki hakipo, kwa sababu hakipo na kama hakipo, hakithibitishiki kwamba hakipo.
Ukitaka mtu anayesema uchawi haupo athibitishe uchawi haupo, ni sawa na kumwambia mtu ambaye hajavamiwa na wezi na kuibiwa athibitishe kwamba hajavamiwa na wezi na kuibiwa.
Atathibitishaje?
Anayeweza kuthibitisha ni yule anayesema jambo limetokea.
Anayesema kavamiwa na wezi na kaibiwa anaweza kuthibitisha kwa alama za vidole za hao wezi, anaweza kutoa video ya kuonesha wezi wakiingia kwake.
Sasa mtu anayesema hakuna wezi walioingia kwake unamtaka athibitishaje kuwa hakuna wezi walioingia kwake?
Unataka atoe alama za vidole za wezi ambao hawapo? Unataka atoe video ya kuonesha wezi ambao hawapo?
Polisi wakisema una madawa ya kulevya nyumbani kwako, wao ndio wana wajibu wa kuyasaka na kuyapata.
Hawakuambii wewe mtuhumiwa ambaye unasema huna madawa ya julevya uthibitishe huna madawa ya kulevya.
Utathibitishaje huna madawa ya kulevya?
You can't prove a negative.
Wewe unayesema uchawi upo ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisha uchawi upo.
Anayesema uchawi haupo yeye kazi yake ni kutaka uthibitisho tu kuwa uchawi upo.
Ukiangalia watu kwa Mwamposa na makanisani wanavyosaka miujiza ndo utajua safari ni ndefu sana!