Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Hadi unasema hakipo ni kwamba umeshaona kuna sehem/watu wanasema kipo......kisingekuepo hata mawazo ya hiko kitu yasingekuwepo
Kusema tu kuwa kitu flani kipo hakukifanyi kitu hicho kuwepo kweli.

Kwani Wagagagigikoko wapo kweli?
 
Hili jambo lina maswali mengi sana yanayohitaji majibu ili kuweza kulithibitisha.

Kwa sababu ukijaribu kuangalia unaona kuna watu wanapata matatizo wanaenda kwa waganga na matatizo yao kweli yanaisha. Ukiangalia kuna watu wanatumia ndagu kupata pesa na kweli wanapata pesa na mali zinaonekana, jambo zinakua na mambo mengi ila still watu tunamuona kua flani kapata pesa na kunakua 'na za chini' za kuaminikakua pesa alizopata ni za kishirikina(manake ushirikina umefanya kazi).

Ila still pia kuna kesi mtu kapata tatizo anakimbilia kwa waganga ila ukiangalia tatizo ni la kawaida wala sio hata la kishirikina, lakini waganga wanamwambia ni la kishirikina na mtu anawaamini, wanaishia kumpiga tu hela na kufanya kweli ionekane kua waganga na ushirikina kwa namna flani kama havina ukweli.

Kwaio ni maswali juu ya maswali
Hiyo ni michezo ya akili tu kuna namna ata mimi naweza kukutengeneza ukawa super hero kwa maneno machache tu .
 
Bado elimu yako mzee rudi tena darasani ,kuna magic tricks ambazo ni mazingaombwe halafu kuna uchawi (ushirikina) jaribu kusoma.

Katika ushirikina waganga 90% ni matapeli pia ushirikina ni imani ya watu kuamini upande wa pili kwa hiyo hauwezi kukuta kweny vitabu vyako.

Hizo hapo ni tricks hata shule za msingi zinaonyeshwa kama sehemu ya entertainment...Hakuna Shule inaruhusu maonyesho ya kichawi ila hizo magic tricks ni sehemu ya buruma ndio maana show kubwa kama America's got talent wanaonyesha.

Nafikiria hujui kuhusu uchawi na ushirikina zipo hata movie za kizungu wamejaribu kuonyesha mambo ya kichawi .
 
Kusema tu kuwa kitu flani kipo hakukifanyi kitu hicho kuwepo kweli.

Kwani Wagagagigikoko wapo kweli?
Hapo ni kama wakutane muislam na mkristo na kila mmoja awe anasema huku ndo kuna mungu,, mwisho wa siku ni experience binafsi ya mtu ndo itakayompa jibu, na hata kwenye uchawi kuna atakaeamini haupo na kuna atakaeamini upo, wote wako sawa maana ni experience tofauti za binadamu
 
Bado elimu yako mzee rudi tena darasani ,kuna magic tricks ambazo ni mazingaombwe halafu kuna uchawi (ushirikina) jaribu kusoma.

Katika ushirikina waganga 90% ni matapeli pia ushirikina ni imani ya watu kuamini upande wa pili kwa hiyo hauwezi kukuta kweny vitabu vyako.
Hapa ndo napoona wanachanganya mazingaombwe na uchawi
 
Na nyie thibitisheni haupo, maana na nyie mmeweka maneno tu
Anayesema kitu kipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha kitu kipo.

Kwa sababu kilichopo ndicho kinathibitika kipo.

Kisichopo, nje ya nadharia tupu, hakithibitiki hakipo, kwa sababu hakipo na kama hakipo, hakithibitishiki kwamba hakipo.

Ukitaka mtu anayesema uchawi haupo athibitishe uchawi haupo, ni sawa na kumwambia mtu ambaye hajavamiwa na wezi na kuibiwa athibitishe kwamba hajavamiwa na wezi na kuibiwa.

Atathibitishaje?

Anayeweza kuthibitisha ni yule anayesema jambo limetokea.

Anayesema kavamiwa na wezi na kaibiwa anaweza kuthibitisha kwa alama za vidole za hao wezi, anaweza kutoa video ya kuonesha wezi wakiingia kwake.

Sasa mtu anayesema hakuna wezi walioingia kwake unamtaka athibitishaje kuwa hakuna wezi walioingia kwake?

Unataka atoe alama za vidole za wezi ambao hawapo? Unataka atoe video ya kuonesha wezi ambao hawapo?

Polisi wakisema una madawa ya kulevya nyumbani kwako, wao ndio wana wajibu wa kuyasaka na kuyapata.

Hawakuambii wewe mtuhumiwa ambaye unasema huna madawa ya julevya uthibitishe huna madawa ya kulevya.

Utathibitishaje huna madawa ya kulevya?

You can't prove a negative.

Wewe unayesema uchawi upo ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisha uchawi upo.

Anayesema uchawi haupo yeye kazi yake ni kutaka uthibitisho tu kuwa uchawi upo.
 
Ni ngum kidogo kuamini unachosema kwa sababu unakuta mtu huyo ambae anasemwa kua katumia ushirikina kupata mali, ni mtu ambae hakua na biashara kubwa ya kusema imempa mali nyingi ndani ya muda huo mfupi hata kama angetumia elimu ya aina gani kuongoza biashara yake

mganga maarufu dokta mwandulami. anakupa majibu ya swali lako msikilize

Hapo ni kama wakutane muislam na mkristo na kila mmoja awe anasema huku ndo kuna mungu,, mwisho wa siku ni experience binafsi ya mtu ndo itakayompa jibu, na hata kwenye uchawi kuna atakaeamini haupo na kuna atakaeamini upo, wote wako sawa maana ni experience tofauti za binadamu
Hakuna uchawi.
 
Anayesema kitu kipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha kitu kipo.

Kwa sababu kilichopo ndicho kinathibitika kipo.

Kisichopo, nje ya nadharia tupu, hakithibitiki hakipo, kwa sababu hakipo na kama hakipo, hakithibitishiki kwamba hakipo.

Ukitaka mtu anayesema uchawi haupo athibitishe uchawi haupo, ni sawa na kumwambia mtu ambaye hajavamiwa na wezi na kuibiwa athibitishe kwamba hajavamiwa na wezi na kuibiwa.

Atathibitishaje?

Anayeweza kuthibitisha ni yule anayesema jambo limetokea. Anayesema kavamiwa na wezi na kaibiwa anaweza kuthibitisha kwa alama za vidole za hao wezi, anaweza kutoa video ya kuonesha wezi wakiingia kwake.

Sasa mtu anayesema hakuna wezi walioingia kwake unamtaka athibitishaje kuwa hakuna wezi walioingia kwake?

Unataka atoe alama za vidole za wezi ambao hawapo? Unataka atoe video ya wezi ambao hawapo?

Polisi wakisema una madawa ya kulevya nyumbani kwako, wao ndio wana wajibu wa kuyasaka na kuyapata.

Hawakuambii wewe mtuhumiwa ambaye unasema huna madawa ya julevya uthibitishe huna madawa ya kulevya.

Utathibitishaje huna madawa ya kulevya?

You can't prove a negative.

Wewe unayesema uchawi upo ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisha uchawi upo.

Anayesema uchawi haupo yeye kazi yake ni kutaka uthibitisho tu kuwa uchawi upo.
Haya nathibitisha niliroga na kurogwa pia basi conclusion uchawi upo
 
Back
Top Bottom