Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Kiranga unaijua definition ya HEALTH according to WHO kwa usahihi? je unawezaje kutenganisha physical, mental, social na spiritual well being ktk afya? tuanzie hapa kwanza
Rusha ungo watu wote waone tumalize ubishi.

Wacha longolongo.
 
Basi wachawi wa JF watajaribu kurusha makombora yao kwa mtoa mada, utupe mrejesho tu mkuu lol

Hawawezi kuniroga maana uchawi haupo na haujawai kuwepo. Wamebaki wanafyonza tu nimewatia aibu
 
Mkuu hiyo michezo mbona hata kwa email tu unafanya, kuna uchawi gani hapo?

Fanya uchawi mtu apae na ungo tuone.

Kesho itoke kwenye TV kila mtu kaona.

Halafu tuje tujadili hapa.
Mkuu wewe una amini kuwa Mungu yupo au hayupo? Je una amini juu ya nguvu za asili ambazo zinaendesha kila kitu hapa duniani?
 
Ngoja nikuulize swali hili unijibu: Una amini kuwa Mungu yupo? Na je, wewe ni muumini wa dini kuu mbili hapa Tanzania yaani Ukristo na Uislamu? Nijibu ili tuanzie hapo

Hata Mungu hayupo na hajawai kuwepo.

Mungu na uchawi ni kama simba na yanga wanategemeana

Uchawi hakuna. Waliomtengeneza Mungu Ndio walioleta neno uchawi. Ni kama movie. Kunakua na steringi na kubwa la maadui. Hapa kwenye movie hii Mungu ndo stering na uchawi ndio kubwa la maadui
 
Mimi niseme tu kuwa watu mnapenda sana kurahisisha mambo pia mnapenda kutafuta habari zinazowafurahisha, mtu anajigamba amesoma PHYSIOLOGY yotn googln na pia amesoma PSYCHOLOGY yote google yaani hii ni dharau kubwa sana watu wanakaa darasani zaidi ya miaka minne wewe uje useme ni umemaliza kila kitu? ungekua umesoma human psychology na kuielewa vizuri usingeanzisha uzi wako maana umetaja mpaka mambo ya COGNITIVE ndani yake kuna PSYCHOLOGY of education na learning theories ungekuwa unazijua usingewaona watu wote wenye smartphone ni wajinga . pia ungekua unaijua history ya medicine vizuri usingeleta uzi wako. hivi ALBERT BANDULA, HYPOCRATES, TO YOUYOU na KEKULE unawajua? tumia simu yako kugoogle sawa! pia uchawi na uganga ni elimu ya siri na ni ngumu kuliko udaktari pia si kila mtu anaweza kufundishwa na shule yake huchukua miaka mitano mpaka kumi ndio maana hao unaowaona mtaani wengi ni matapeli ntaishia hapa wajuvi watakuwa wamenielewag
Hawa wanaopinga uwepo wa uchawi wana shida mahali. Sema tu ni kwa sababu mleta uzi amesema yeye haamini juu ya uwepo wa Mungu, nimegundua kuwa ni mtu wa kumpuuza.
 
Sawa. Hapa mjadala umemaliza. Nimejua wewe ni mtu wa namna gani. Kwani wewe unavyo jua, nini maana ya Mungu? Watu wanaposema Mungu huwa wanamaanisha nini?

Wanamaanisha kiumbe mwenye nguvu, muweza wa yote aliyetajwa kwenye bibilia na quran
 
Mimi natoka Bariadi, Simiyu. Habari ni ile ile tu. Hakuna uchawi. Na mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa kuniroga hapo Bariadi.

Hakuna aliyefanikiwa kuniroga kwa sababu uchawi haupo. Ni fiksi tu zinazotumika kutishia wajinga!
Usichojua ni kuwa kuna factors nyingi sana zinazopelekea mtu arogwe au afanyiwe ushirikina. Kutokurogwa inategemea pia mazingira uliyo kulia, ukoo, utamaduni wa ukoo wenu nk. Ila usiseme uchawi haupo. Pia kurogwa kutategemeana na unafanya nini na una nini. Siyo kila mtu anaweza kurogwa.
 
Huyu amachanganya mambo, kuna uchawi wa kuloga na uchawi wa mazingaombwe,

Ikiwa unaamini dini lazima uukubali uchawi kwa maana ktk biblia matendo ya mitume inasema,,

Hapo mwanza mtu mmoja alikuwa akifanya mambo ya kichawi, mtu huyo ni muyahudi tena nabii wa uwongo na jina lake ni simioni,

Yesu anamwambia simioni ww ni shetani rudi nyuma yangu,

Msaafu unasema na huuu uchawi haushushwa pamoja na quraan , hapo vitabu vyote vimezungumzia uchawi, tena quraani imeenda mbele zaid imesema , wachawi enzi za farao ,

Ww leo unasema hakuna uchawi,

Au unatuletea mambo ya siasa hapa hakimu amekwenda kwa mganga ili awe imara kwenye kazi yake lkn akiletewa kesi ya uchawi anaitupilia mbaliiiii
 
Sawa. Hapa mjadala umemaliza. Nimejua wewe ni mtu wa namna gani. Kwani wewe unavyo jua, nini maana ya Mungu? Watu wanaposema Mungu huwa wanamaanisha nini?

Ukishaweka ushirikina NA DINI kwenye mambo halisi unakuwa huwezi tafuta solution ya tatizo kwa sababu kila kitu utaona ni Mungu, shetani, uchawi, nyota na kadhalika.
 
Huyu amachanganya mambo, kuna uchawi wa kuloga na uchawi wa mazingaombwe,

Ikiwa unaamini dini lazima uukubali uchawi kwa maana ktk biblia matendo ya mitume inasema,,

Hapo mwanza mtu mmoja alikuwa akifanya mambo ya kichawi, mtu huyo ni muyahudi tena nabii wa uwongo na jina lake ni simioni,

Yesu anamwambia simioni ww ni shetani rudi nyuma yangu,

Msaafu unasema na huuu uchawi haushushwa pamoja na quraan , hapo vitabu vyote vimezungumzia uchawi, tena quraani imeenda mbele zaid imesema , wachawi enzi za farao ,

Ww leo unasema hakuna uchawi,

Au unatuletea mambo ya siasa hapa hakimu amekwenda kwa mganga ili awe imara kwenye kazi yake lkn akiletewa kesi ya uchawi anaitupilia mbaliiiii

Hakuna mtu mwenye akili ambaye anaamini kitabu kilichoandika nyoka anaongea na binadamu.

Hivi kwa akili zako za kawaida unaamini nyoka anaweza kuongea na binadamu ?

Biblia ni kitabu chenye upuuzi na contradictions nyingi tu.

Wenye akili hawawezi kuamini hicho kitabu
 
Mkuu wewe una amini kuwa Mungu yupo au hayupo? Je una amini juu ya nguvu za asili ambazo zinaendesha kila kitu hapa duniani?
Sitaki kuamini, nataka kujua, kuthibitisha. Ukweli. Kuhakiki mambo kimantiki.

Kuamini hata uongo naweza kuamini.

Ni haki ya kikatiba na kibinadamu kuamini unachotaka.

Sasa kwa nini kuamini kiwe kitu muhimu?
 
Mkuu hiyo michezo mbona hata kwa email tu unafanya, kuna uchawi gani hapo?

Fanya uchawi mtu apae na ungo tuone.

Kesho itoke kwenye TV kila mtu kaona.

Halafu tuje tujadili hapa.
hujajibu swali nlokuuliza
 
Unaenda chunguza uchawi kwenye GOOGLE badala ya kufanya tafiti kwenye mazingira hali unayoishi...!!

Tafuta vijiji kadhaa vinavyosifika kwa ushirikina, then nenda kaendeshe utafiti wako huko...
 
Usichojua ni kuwa kuna factors nyingi sana zinazopelekea mtu arogwe au afanyiwe ushirikina. Kutokurogwa inategemea pia mazingira uliyo kulia, ukoo, utamaduni wa ukoo wenu nk. Ila usiseme uchawi haupo. Pia kurogwa kutategemeana na unafanya nini na una nini. Siyo kila mtu anaweza kurogwa.
Visingizio vingi ni ishara mojawapo kuwa uchawi haupo.

Ungekuwepo kweli wala msingeleta tararira!
 
Ndugu Mleta Uzi, naimani hayajakukuta na nakushauri omba yasikukute (nukta)
 
Habari wadau

Binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

Ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi kuhusu Anthropology, elimu ya Human psychology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

Watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.

Kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu.

Mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu kwa kutumia Placebo effects na magic tricks. yaani ukizijua hizo hakuna mganga ataeweza kukudanganya hasa ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.

Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

Jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.

Ndugu unayo mengi mno ya kujifunza katika ulimwengu huu. Hiyo internet ndio inafichua uchawi kwa namna ya ajabu kuwahi kufikiriwa. Fuatilia mikasa ya Davista Mata kwenye YouTube utaona mwenyewe ukweli ulivyo.
 
Back
Top Bottom