Tangu Nicolás Maduro achukue hatamu za uongozi mwaka 2013, Venezuela imepitia misukosuko mikubwa ya kisiasa na kijamii ambayo imesababisha shutuma nzito za ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mashirika ya kimataifa yamekuwa yakiandika ripoti mbalimbali zinazoonyesha mbinu za kimfumo zinazotumiwa na Serikali kudhibiti upinzani na kukandamiza uhuru wa raia.
Baadhi ni kama ifuatavyo:
Mashirika ya kimataifa yamekuwa yakiandika ripoti mbalimbali zinazoonyesha mbinu za kimfumo zinazotumiwa na Serikali kudhibiti upinzani na kukandamiza uhuru wa raia.
Baadhi ni kama ifuatavyo:
1. Uminywaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari
Uhuru wa kujieleza na Vyombo vya Habari umepungua kwa kiasi kikubwa nchini humo kupitia mbinu kadhaa:- Kufungwa kwa Vituo vya Habari: Serikali imekuwa ikitumia Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (CONATEL) kufuta leseni za mamia ya vituo vya redio na televisheni vinavyoonekana kuwa na mrengo wa kuikosoa Serikali. Mamlaka hii haina tofauti na TCRA kwa Tanzania
- Sheria dhidi ya "Chuki": Mnamo mwaka 2017, Serikali ilipitisha sheria ("Ley contra el Odio") ambayo inatumiwa kuwafunga waandishi wa habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaochapisha maoni yanayoikosoa Serikali, kwa madai ya kuchochea chuki. Kumbuka, 2018 Tanzania ilipitisha Online Content Regulations zinazoshabihiana na hizi.
- Udhibiti wa Intaneti: Kuna ripoti za mara kwa mara za Serikali kuzuia upatikanaji wa tovuti za habari za kimataifa, tovuti zenye maudhui yasiyoifurahisha Serikali na mitandao ya kijamii wakati wa maandamano au migogoro ya kisiasa.
2. Mauaji ya Raia na Mauaji ya Holela (Extrajudicial Killings)
Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kutafuta Ukweli (UN Fact-Finding Mission) ilibaini kuwepo kwa ushahidi wa uhakika wa mauaji ya maelfu ya watu yanayofanywa na vikosi vya usalama:- Vikosi vya FAES: Kikosi maalum cha Polisi (FAES) kimetajwa mara nyingi kwa kuhusika na mauaji ya vijana katika maeneo maskini kwa kisingizio cha kupambana na uhalifu, lakini mara nyingi yakiwa ni mauaji ya kisiasa.
- Ukandamizaji wa Waandamanaji: Wakati wa maandamano makubwa ya mwaka 2014, 2017, na hivi karibuni 2024 (baada ya uchaguzi wa rais), vikosi vya usalama vilibainika kutumia nguvu kubwa kupita kiasi, ikiwemo matumizi ya risasi za moto dhidi ya waandamanaji wasio na silaha.
3. Kutekwa na Kupotezwa kwa Wananchi (Enforced Disappearances)
Mbinu ya "kutoweshwa kwa lazima" (watu wasiojulikana) imekuwa ikitumiwa kudhoofisha upinzani:- Operesheni "Tun Tun" (Gonga Gonga): Jina hili linatokana na sauti ya hodi mlangoni, ambapo vikosi vya usalama huvamia nyumba za wapinzani na kuwachukua bila hati ya kukamatwa. Mara nyingi familia hazijulishwi mahali walipo kwa siku au wiki kadhaa.
- Kutekwa kwa Wanaharakati: Wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu na viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakikamatwa na kupelekwa kusikojulikana, jambo ambalo ni kinyume na sheria za kimataifa.
4. Uminywaji wa Demokrasia
Mfumo wa kidemokrasia nchini Venezuela umeingiliwa na Serikali ili kuhakikisha Rais anabaki madarakani:- Udhibiti wa Tume ya Uchaguzi (CNE): Tume ya Uchaguzi inatuhumiwa kuwa na upendeleo kwa chama tawala (PSUV), huku ikizuia wagombea wenye nguvu wa upinzani kushiriki.
- Kuzuia Wagombea: Viongozi wakuu wa upinzani kama María Corina Machado wamewekewa ugumu wa kushika nyadhifa za umma kwa tuhuma zisizo na ushahidi wa kutosha, lengo likiwa ni kuwaondoa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi.
- Kudhibiti Bunge na Mahakama: Mahakama Kuu (TSJ) imekuwa ikitumika kutoa maamuzi yanayofuta mamlaka ya Bunge pindi upinzani unaposhinda viti vingi.
5. Kukamatwa na Kufungwa kwa Wapinzani na Wakosoaji
Venezuela ina mamia ya wafungwa wa kisiasa wanaoishi katika mazingira magumu:- El Helicoide: Jengo hili maarufu huko Caracas linatumika kama gereza la siri la shirika la ujasusi la nchi hiyo (SEBIN), ambapo ripoti za mateso, ikiwemo kupigwa, matumizi ya shoti za umeme, na unyanyasaji wa kijinsia, zimeripotiwa mara kwa mara.
- Mfumo wa "Revolving Door": Serikali imekuwa ikitumia mbinu ya kuwaachia baadhi ya wafungwa wa kisiasa ili kupunguza shinikizo la kimataifa, huku ikikamata wengine wapya siku chache baadaye ili kudumisha hali ya hofu.