Ukiukwaji wa maadili (unethical conduct) na professionalism kati ya DCI Boaz na Luteni Urio kwenye kesi ya Mbowe na wenzake

Ukiukwaji wa maadili (unethical conduct) na professionalism kati ya DCI Boaz na Luteni Urio kwenye kesi ya Mbowe na wenzake

Nilichoelewa ni kwamba bwn Urio naye ameunganishwa tu kwenye huu ushahidi ila naye alikuwa kwenye mateso sawasawa na wakina Ling'wenya ila hawa wakina Kingai wamem-coach ili awe shahidi upande wa serikali ili awe salama.Hapo ni kwamba anataka kujinasua yeye mwenyewe.
Moses Lijenje hajulikana alipo mpaka sasa, huyu kijana nini kilimpata?....mbona haonekani mahakamani pamoja na wenzake?

Hii kesi ina maswali mengi kuhusu utendaji kazi wa polisi.
 
Waliosema mwanzo kuwa kesi hii ifutwe walitaka kutukosesha kujua mambo mengi.

Sioni kama Denis Urio anayo namna ya kulipa madhira aliyosababisha kwa rafiki zake hawa kwa kuwauza.
 
Umeandika vizuri sana... mpaka mtu uwe Great Thinker ndo unaweza kuelewa umeandika nini hapa. Haiwezekani mtu uwatoe watu kwenye shughuli zao halali, uwaingize kwenye matatizo makubwa, waanze kupigwa, kuteswa, kukaa jela, kushtakiwa kwa ugaidi.. wakati watu walikuwa busy na mambo yao tu. Huyu Urio ni mtu muovu sana ambae anastahili apigwe mawe hadharani! Wake na watoto wao wanateseka kwaajili ya huyu Urio.. Kesi ikiisha inatakiwa ashtakiwe na awalipe fidia hawa makomandoo kwa kuwaingiza kwenye matatizo
Wewe hamnazo kabisa! Kama kweli Urio na DCI walikuwa na utu hao kina Bwire walitakiwa wawe upande wa polisi kuwa waende kufanya hiyo issue ila hata wakikamatwa itakuwa bosheni tu! Mwisho wamewatesa watu wa watu bila hata kosa.
 
Urio alikuwa afisa wa JWTZ wakati anapodai Mbowe alimtaka awatafute hao vijana waliotakiwa kufanya ugaidi; kwanini Urio aliona ni busara kwanda kwa DCI na kuripoti tuhuma hizo badala ya kutoa ripoti kwa mkuu wake huko JWTZ anayehusika na military intelligence?
 
Wewe hamnazo kabisa! Kama kweli Urio na DCI walikuwa na utu hao kina Bwire walitakiwa wawe upande wa polisi kuwa waende kufanya hiyo issue ila hata wakikamatwa itakuwa bosheni tu! Mwisho wamewatesa watu wa watu bila hata kosa.

Sasa mimi nimeandika nini na wewe unasema nini...we maandazi nini?
 
Urio ndiyo anamfungisha Mbowe yaani kaanika ukweli mtupu Mbowe angeiharibu nchi alikuwa na nia ovu haswaaa Mbowe anakwenda kufungwa hamna namna
Utasubiri sana! Kingai unaumia moyoni lkn ujweli ndo huo. Movi uliosotea muda mrefu haitakupa jina.
 
Kama ni mtego mbowe kajaa.
Mtego utoke wapi? Kwanza maajabu ni kwamba, kama leo Mbowe anakutana na Urio Casa, kesho yake Urio anaenda kwa DCI kutoa taarifa hapo hapo anaingia Kingai ambaye by then alikuwa Ars kama RCO! Real? Nini kilimwotesha Boaz kwamba hii kesi inayokuja mpelelezi awe RCO Wa Arusha ingawa itafungukiwa DDM. Aisee?! RCO wa DSM wala mikoa iliyokaribu na DSM wameenda wapi?. Yaani hii connection ya Kingai, Urio na Boaz inakujaje wakati Mbowe alikuwa anaratibu haya mambo akiwa DSM? Something very fishy here
 
Urio ndiyo anamfungisha Mbowe yaani kaanika ukweli mtupu Mbowe angeiharibu nchi alikuwa na nia ovu haswaaa Mbowe anakwenda kufungwa hamna namna
Wafuasi wa Cdm hawakuwepo kusaidia huo Ugaidi? Vijana 4 wanaweza Fanya Ugaidi Nchi nzima? Vilipuzi viko wapi? Mimi nilifikiri alikuwa anaombwa Connection ya Mabomu kumbe Walinzi!!
 
Mtego utoke wapi? Kwanza maajabu ni kwamba, kama leo Mbowe anakutana na Urio Casa, kesho yake Urio anaenda kwa DCI kutoa taarifa hapo hapo anaingia Kingai ambaye by then alikuwa Ars kama RCO! Real? Nini kilimwotesha Boaz kwamba hii kesi inayokuja mpelelezi awe RCO Wa Arusha ingawa itafungukiwa DDM. Aisee?! RCO wa DSM wala mikoa iliyokaribu na DSM wameenda wapi?. Yaani hii connection ya Kingai, Urio na Boaz inakujaje wakati Mbowe alikuwa anaratibu haya mambo akiwa DSM? Something very fishy here
MBOWE angekuwa Gaidi angeomba Connection ya Mabomu kwa Komandoo Urio. Hapo tungeogopa. Mbowe alimkosea Nini Urio hadi amsaliti hivi?
 
Katika ushaidi wa jana Urio alieleza kwamba Mbowe alimuomba amtafutie askari waliofukuzwa ili awatumie kufanya vitendo vya kuvuruga amani ya nchi, kama kukata miti mikubwa kuchoma masoko na vituo vya mafuta na kudhuru viongozi. Kwa maelezo yake LT Urio alisema kwa uzalendo wake kwa nchi aliamua kwenda kuripoti suala ili kwa DCI Boaz. DCI Robert baada ya kupata taarifa za URio alimwambia aendelee na kazi hiyo ya kutafuta watu hao. Na awe anatoa taarifa kwake na kwa Kingai.

Urio alienda kuwatafuta vijana Raia wema waliofukuzwa Jeshini waliokuwa kwenye shughuli zao nyingine halali na kuwaambia kwamba kuna kazi ya ulinzi binafsi (bodyuard) anayoitaji Mbowe, na hakuwaambia ukweli vijana wale kwamba kuna kazi ya kufanya ugaidi. (kuvuruga amani ya nchi, kama kukata miti mikubwa kuchoma masoko na vituo vya mafuta na kudhuru viongozi)

Ukiukwaji wa maadili na unproffesionalism unaanzia hapo
Kwa sisi ambao tunafanya research kunakitu kinaitwa implied consent (ridhaa) lazima iwepo, hata unapofanya suala la kijasusi lazima mtu akubali ndio mambo mengine yaendelee. DCI inabidi naye aitwe mahakamani aeleze alipomkubalia Urio awatafute hao watu ilikuwa ili wawe upande wa serikali au waangushiwe jumba bovu? Tena bila ridhaa yao. Na Urio aulizwe ni nani alimuelekeza awatafute vijana awadanganye kwamba mbowe anataka walinzi wakati mbowe alimwambia anataka vijana wa kufanya ugaidi na hata kwa maelezo yake DCI alimkubalia Lt Urio aende akatafute vijana wa kwenda kufanya huo ugaidi na sio kazi ya ulinzi aliyowaambia

Hivi kweli tufikirie kwa kina na wewe Urio kama unasoma hapa unawezaje kama kweli wewe ni raia mwema wa nchi kumtafuta raia mwema mwenzako na kumdanganya kwamba kuna kazi ya ulinzi wakati kweli unajua kuna kazi ya ugaidi na ukamuingiza bila yeye mwenyewe kufaamu na bila ridhaa yake, halafu kwa macho makavu kabisa unakuja kumtolea ushahidi mahakamani kwamba walikuwa wanapanga uaidi ambao wewe ulikuwa uanujua tokea mwanzo lakini ukawaambia ni kazi ya ulinzi (Bodyuard). Wewe Urio unatakiwa upiwe mawe hadharani hadi ufe kwa aina ya ushaidi ulioutoa mahakamani jana.

Unprofesionalism ya DCI ipo hapa
Alipopokea taarifa ya Urio angetakiwa awasiliane na makachero wake waadilifu au awasiliane na IGP amuombe CDF ampatie vijana wake wa millitary intellience waitwe wakalishwe chini waambiwe kwamba wamepata taarifa mbowe anataka kufanya vitendo vya kigaidi na anahitaji watu wa kufanya hiyo kazi na wao kama vijana waadilifu na wazalendo wa nchi wameteuliwa kwenda kumchunguza jupata ukweli wa taarifa hiyo na watawasiliana na mtu wa kuwaunganisha na Mbowe.

Vijana hao wangeambiwa watakuwa undercover na watajulikana kama vijana waliofukuzwa jeshini na wangeambiwa baada ya kazi kumalizika watalipwa honorary na wafanye kazi na kuhifadhi ushahidi pamoja na uthibitisho usio na shaka ambapo utakapopolekwa mahakamani utakuwa hauna shaka yeyote. Na mwisho hawatachukuliwa hatua.

Kinachoelezwa mahakamani kwa sasa ni upuuzi na upumbavu uliopitiliza vitu vimetengenezwa kipumbafu hadi vinaleta kinyaa

WEWE URIO UMETOA USHAIDI WA HOVYO SANA
Basic question,huyo urio ni intelijensia oficcer?ana ujuzi wa intelijensia?
 
MBOWE angekuwa Gaidi angeomba Connection ya Mabomu kwa Komandoo Urio. Hapo tungeogopa. Mbowe alimkosea Nini Urio hadi amsaliti hivi?
Urio ni shetani, alitafutwa na kutumiwa na akina Sabaya kummaliza Mbowe chini ya uratibu wa mwendazake. Bahati mbaya Jamaa katangulia mbele za haki kabla udhalimu haujakamilima. Hii ndo maana Sabaya na Makonda walilia kama watoto wadogo against kifo kile. Makonda akiwa na Boaz Dar wanapika sumu against Mbowe; Arusha, Sabaya na Kingai wanasaga sumu against Mbowe. Kote huku nia ni moja; Mbowe
Sijawahi kuona watu wenye roho mbaya kama Hawa. Wakati Urio akitamba kwamba kwenye screen server ya techno yake Kuna picha ya familia yake lkn wakati huohuo anaagamiza familia ya Mbowe na familia za wale washitakiwa wengine Kwa maslahi ya watawala. Very sad.
Lutein Denis Urio is just form four leaver. Akili ndogo, upeo mdogo na uelewa mdogo. Wanasiasa Wa chama tawala waliamua kutumia ujinga wake kumdhalilisha bila yeye kupima impact yake kwake. Jeshi imedhalilika pia.
 
Hakuna officer wa jeshi ambaye ni from four leaver take it from me.
 
Nionavyo;
Nikweli Uri aliombwa na boe kutafuta walinzi toka wajeda walostopishwa.

Uri alimtafutia kweli na kumkabidhi dili likaisha.

Boe alishtukiwa ametafuta wajeda kumlinda na kupambana na yeyote atayemdhuru!

Ikafatiliwa Uri akashtukiwa,kujitetea akafundishwa vya kuongea ili kina damoo wawe magaidi

Kesi inatengenezwa ili Uri aonekane hanashida Bali kina Boe,damoo et al.

Uri amelazimishwa kuongea anavyoongea kwakuongeza vituflani ili abaki salama.

Tumuombe Mungu awafarakanishe na kuwaumbua wooote wanaoapa hadharani nakuishia kuongea uongi
 
Hii kesi itawaacha midomo wazi watanzania wengi sana....

Watajua serikali na majeshi yetu wanafanya mambo gani nyuma ya pazia....

Haijalishi matokeo yatakuwaje.... Ila nadhani kuna siku hii kesi itatumika kama reference... Na kuna viongozi wengi kuanzia sasa watakuwa makini sana
 
Urio ndiyo anamfungisha Mbowe yaani kaanika ukweli mtupu Mbowe angeiharibu nchi alikuwa na nia ovu haswaaa Mbowe anakwenda kufungwa hamna namna
Nyie ndo tunasema kila siku mmelishwa ugali tu tangu utoton bila hata mboga za majan hadi mkawa hivi. Usiharib uzi wa mtoa mada mwenye akili timam. Kuna majukwaa yako humu mengine! Huku kigezo ni uwe na akili timam
 
Back
Top Bottom