Ukiwa Maskini hata siku ya Kufa utakuwa nayo ni Shida tu kwa wengine

Ukiwa Maskini hata siku ya Kufa utakuwa nayo ni Shida tu kwa wengine

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
Yaani unakuta mtu anakaribia kufa unamuuliza "sasa mzee unatuachaje?" Anasema "muishi kwa amani na upendo"

Khaaaa... Amani na upendo hakuna mshiko? Mzee anakufa anawaachia Kauli tu. Maana ndiyo aliyo nayo hana mali.... Anaacha kauli na madeni.unakufa bado unawaachia shida. Si bora ungeishi umalize madeni yako ndo ulale mbele?

Halafu bado unaweka na masharti "nikifa kinazikwe kididimo" we mzeee? Umeacha pesa ya kukusafirishia huko? Mbona inakuwa shida juu ya shida. Sometimes unaona watoto wa marehemu wanalia sana ukijiuliza wanalia nini kumbe wanalia uchungu mkubwa kwa baba yao kuondoka na kuwaachia kauli tu na madeni.

Hapo watoto wa maskini utasikia. "Baba yetu alituachia kauli thabiti" sasa unauliza angeacha nini? Maana hakuwa na kitu....basi ndo anawaachia kauli. Unadhani akifa Bil Gates, akifa Elon Mask. Anahaja ya kuacha kauli thabiti? Anaacha matendo thabiti.

Basi mzee Kigwasu akiwa kitandani amezungukwa na watoto wake akawatizama kwa macho ya upole. Akatizama dirishani...akawa kama anawaza. Watoto wake wakawa wanasubiria neno toka kwake.

Akasema "Acheni ujinga, tafuteni pesa" kisha akashusha pumzi akafa. Wale watoto wakaondoka kwanza kila mtu akiwa kama amechanganyikiwa wakimwacha mzee kitandani. Kisha baada ya dk kama 3 wakaitana tena mle.chumbani. wakagundua mzee wao hakuwa na cha kuwaachia. Kawaachia kauli.
 
Kama huyo mzee angekuwa na mali siangekufa tu???hao watoto wanatakiwa wapambane kivyao ili nao waone maisha yakoje..
 
Back
Top Bottom