Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Imagine kwa elfu 40 tu unaweza kwenda na kurudi Dodoma ukitokea Dar.

Mfano, ukiwa na Tesla Model 3 yenye battery ndogo kabisa 57.5 kWh (hii ndio battery ndogo ipo kubwa Long Range ila tusiiongelee hapa), inamaana utatumia unit 57.5 tu kuijaza full charge. Na kwa bei ya sasa, unit moja ya umeme ni Tsh 358, so ukizidisha na ukubwa wa battery ni elfu 20!

Na hii model ikiwa full charge inatembea jumla ya kilometa 513. Na distance kutoka Dar hadi Dodoma ni Kilometa 460!

Kwahiyo hapo ushaenda na zinabaki kilometa za kutosha za misele hapo Dom.

So na kurudi hivo hivo, jumla 40.

Mtu, mwenye IST akiiga yeye kwa average fuel consumption ya 20km/L atataka elfu 70 ya mafuta kwenda tu na kurudi ivyo ivyo. Jumla 140,000/=
 
Gharama utazipata kwenye kubadilisha betri baada ya iliyopo kuchoka. Kutumia zaidi ya nusu ya gharama ya gari kununua battery kawaida. Na hayo magari warranty ikiisha utaliogopa.

Na wale wa magari used hapa si kwao utalia na kusaga meno. Mambo ya kuendesha gari la 2006 leo 2024 yataisha. Mambo ya kuendesha gari maili 150,000 almost yataisha.
 
Nna ka hybrid Kwa mizunguko ya mjini si haba. Ila siwezi kwenda Nako masafa marefu.

Kubwa yake kidogo ( hii ni full mafuta) ukiweka full tank, 240,000/- Kutoka Dar, ukifika Dom taa inawaka inabidi uongeze mwarabu. Uzuri speed ni 140km/h-200km/h.
 
Back
Top Bottom