Kwisha habari yake. Vingi vishstupwa. Battery takataka. Most were used.
Naweka mrejesho kama mmojawapo wa wamiliki wa pikipiki za umeme.
Kwanza nikweli katika magari na pikipiki za umeme gharama kubwa huangukia kwenye battery.
Nirudi kwenye feedback.
Zimeingizwa pikipiki nyingi sana zikiwa branded majina tofauti, kuna Linkall, Nuru, zactec, Yadea na nyinginezo sizikumbuki, katika hizo zote Yadea tu ndio mzalishaji mkubwa wa pikipiki za miguu miwili na mitatu za umeme duniani
kwa hiyo kwa yeyote anaetaka pikipiki ya umeme anunue yadea tu na sio hizo nyingine.
Kwenye upande wa battery pikipiki nyingi zinakuja na battery aina ya Lead Acid hizi bei zake ni rahisi na pia huwai kufa makadirio ni miezi 12 kama zitatunzwa vizuri, baada ya muda huo zinakua zinahitaji kubadilishwa.
Aina zingine za battery ni Graphene na Lithium ion kundi hili la pili battery zake ni ghali na pia zina maisha marefu ukilinganisha na lead acid, hivyo pikipiki yoyote iliyofungwa hizi battery huwa na bei ya juu.
Kwa Brand ya yadea wanafunga battery za Graphene ni reliable kwakweli, pia unaweza upgrade battery kama unahitaji kuongeza range.
Kwa kifupi na uchache hayo ni machache naweza kusema.
Maintenance cost kwa hizi pikipiki ni kama hamna ila battery ikifa ndio lazima mfuko utoboke.
Gharama za battery inategemea na ukubwa wa motor pamoja na controller zimekua rated vipi za pikipiki husika.
Kuna 36V, 48V, 60V na 72V
Na zile battery huwa ni za 12V hivyo kwa mwenye 36V atahitaji battery 3
wa 48v atahitaji battery 4
wa 60V atahitaji battery 5
wa 72V atahitaji battery 6
Hizo Voltage zinatofautiana kulingana power rating ya motor husika, kadri voltage inakua kubwa ni nguvu kubwa ya motor na ndio speed huweza kuwa kubwa pia.
Kuhusu Range inategemea na capacity ya battery na speed utakayoendesha.
kwa mfano 72V38Ah ukitembea na eco mode unaweza kwenda 100km
72V23Ah in eco mode unaweza kwenda 70km
Kwa hivyo 38Ah na 23Ah ni capacity za battery husika na pia huathiri bei.
Nilichokuja kubaini watu wengi wananua hizi pikipiki bila kuwa na taarifa sahihi na muhimu, mtu ataangalia rangi na mwonekano kumbe kuna taarifa muhimu sana kuliko hizo urembo za nje, kingine wauzaji karibu wote hawana taarifa sahihi za vitu wanauza, unamuuliza muuzaji yeye amekariri bei tu, ukimbana sana unaitiwa fundi 😂😂 ambae nae hamna anachojua zaidi wanajua ku assemble zile pikipiki kutoka kwenye mabox nazungumzia zile za mafuta, ila technical specs hawajui kabisa na hawaelewi chochote ila majibu utapewa wabongo hawakosagi majibu hata kwa wasichokijua.