Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

WADAU KUNA MAGARI YA UMEME NAYAONA ALIBABA....BEI INAONEKANA SIYO MABAYA...VIP HAPO BANDARINI UTARATIBU UMEKAAJE KWA MAGARI YA CHINA
Usijaribu kununua magari Alibaba. Mengi ni vituko nenda kwenye official website hata kwa Brand za China kama BYD.

Kama unataka kuona hivyo vituko ingia Youtube uone wakionunua EV from Alibaba
 
Usijaribu kununua magari Alibaba. Mengi ni vituko nenda kwenye official website hata kwa Brand za China kama BYD.

Kama unataka kuona hivyo vituko ingia Youtube uone wakionunua EV from Alibaba
Asijaribu aisee. Tulinunua pikipiki ya umeme kwa Tsh Mil 2.5 hivi. Aisee ile hela bora tungenunua Boxer.
 
Nna ka hybrid Kwa mizunguko ya mjini si haba. Ila siwezi kwenda Nako masafa marefu.

Kubwa yake kidogo ( hii ni full mafuta) ukiweka full tank, 240,000/- Kutoka Dar, ukifika Dom taa inawaka inabidi uongeze mwarabu. Uzuri speed ni 140km/h-200km/h.
Sure kaka. Uzuri/ubaya wa hybrids inataka foreni na speed ndogo.

Mfano Aqua iyo na Prius (nadhani ni mtu na mdogo wake hawa) ukiwa na speed ndogo bellow 50kph inaweza kwenda full EV kwa kilometa kadhaa (chini ya 6 kutegemea na battery lako).

Ila ukiwa highway engine muda wote ipo on.
 
Yeah baada ya kilometa atleast 400,000 unatakiwa ubadirishe battery. Itakua imepungua range.
Sasa kilometa 400,000 ni leo? Mimi nimenunua gari 2017 na ninaitumia kila siku kwa mizunguko yangu ya mjini. Niliinunua na km 67,000 leo iko 138,000.

Kilometa 400,000 ni miaka angalau 10 - 15 kwa matumizi ya kawaida.
 
Around lita 70 Mkuu.
Hiyo gari uza... itakutia umaskini.

Inatembea km 6 per liter. Hapo ni HIGHWAY ina maana CITY DRIVE hiyo gari inakupa km 3-4 per liter...

Mie ninayo gari ambayo ni cc2000 nimetoka DSM mpk ARS kwa liter 60. Ina maana kwa kilometers nilizotembea ilikunywa 10.5 - 11 km per ltr. Na kuna sehem nilisimama almost 1 hr bila kuzima gari.
 
Na nimeshaenda safari mbili kupitia Dodoma, zote nilijaza full tank lakini Dodoma taa inawaka kitu empty inabidi uongeze. Hapo ni mwendo wa 140-200km/h. Pia gari inakua haizimi kwakuwa I safari ya masafa marefu.

Wewe ulikua unatembea Kwa speed ya ngapi kiongozi?

Kuna siku tumeenda Moro na wife mwendo wa mahaba, full tank kwenda na kurudi tukabakiwa na ya kuanzia mizunguko ya mjini. Shida yake ukizidi speed ya 100km/h tu. Ukitembea mwendo wa serikali sio mbaya sana.

Mara ya mwisho nimeenda Moshi nilifika Kwa full tank kutoka Dar.
 
Back
Top Bottom