Lucha
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 14,516
- 50,658
Wakuu katika harakati zangu niliwahi kuwa na mahusiano na dada mmoja ambae ni Nesi huyu nili-plan had kumuoa ili tusaidiane kwenye maisha.
Hatua za mwisho za mahusiano yetu alianza kunidanganya yupo shift za usiku kila siku, lakini hali ilizidi hadi nikahisi hatari nikiwa kama binadamu mwenye moyo nilianza kumchunguza, siku 1 nilienda sehemu anayofanya kazi night lakini wale wafanyakazi wenzake wakaniambia hayupo na siku hiyo alisomeka off duty, ilibidi niondoke tu nikakaa kimya.
Asubuhi nikamuuliza jana ulikuwa kazini? Akaanza kunijibu "kwani sikukwambia kuwa nipo shift ya usiku? Au unaniona malaya? "
Ilibidi nitumie busara za kiume tu nikamwambia samahani nilisahau, siku zilienda mapenzi yakapungua kumbe alikuwa anatembea na mkuu wake wa kazi. Nilijaribu tena kwenda night kwa baadhi ya siku zingine zilizofata na baadae nilichoka.
Siku moja nikamwita nikamueleza ukweli wote na vithibitisho vya kutosha baadae nikamwambia "kama tulivyopendana kwa wema naomba mapenzi yetu nayo yaishe kwa wema, nilikupenda sana lakini kwa sasa mapenzi yamegonga ukuta. Naomba uendelee na maisha yako nami niendelee na maisha yangu"
Aliniomba msamaha lakini nilishindwa kabisa kumsamehe na nilishukuru kwa kuyatambua yale mapema pengne ningekuja kuyatambua wakati tumeoana ingekuwa ni msalaba mzito zaidi kwangu
GunFire