Ukiwa na mapesa unaweza kununua kila kitu, isipokuwa mambo haya

Ukiwa na mapesa unaweza kununua kila kitu, isipokuwa mambo haya

Labda kwa mifano utanielewa. Kwani ukinunua gari Japan si unalipata likiwa perfect? Gari linakuja na user manual. Usipofuata masharti ya jinsi ya kulifanya liendelee kuwa perfect, litahabirika. Adam na Hawa walipewa masharti wasile matunda ya mti uliokuwa katikati ya bustani; Mungu akawaambia wakila watakufa. Walikaidi amri hiyo. Kuanzia wakati huo kifo kikaingia na uovu ukaingia. Ila kwa kuwa Mungu anatupenda ametuandalia tena makazi yasiyokuwa na evils. Ukitubu na kumwamini Yesu utaingia katika mbingu isiyokuwa na evils. Tuko pamoja?
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je HAKUJUA kwamba Adamu na Hawa watakula hilo tunda licha ya kuwakataza?

Mungu mjuzi wa vyote, Alishindwaje kuwadhibiti Adamu na Hawa wasile hilo tunda?

Kwa nini Mungu aliruhusu nyoka kuingia bustanini kumdanganya na kumrubuni Eva wale hilo tunda?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
 
Kwanza huyo Mungu kipindi cha Nuhu(Noah), Si aliangamiza uovu, dhambi na waovu wote kwa gharika kuu la mafuriko?
Hakuangamiza uovu; aliangamiza waovu. Waliozaliwa baada ya Nuhu walikuwa na asili ile ile ya dhambi ya Adam na Hawa. Hawakupenda kumfuata Mungu kama baba yao Nuhu, hatimaye wangaamizwa tena kwa moto katika miji ya Sodoma na Gomora. Waliozaliwa baada ya maangamizi ya Sodoma na Gomora wakapendelea dhambi badala ya kumpenda Mungu. Hukumu inakuja nayo ni moto wa milele
 
"Hata ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu; mtu huyu alimwendea Pilato akauomba mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe. Yusufu akautwaa mwili, akauzonga-zonga katika sanda ya kitani safi, akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake".

Masia mwenyewe alizkwa na tajiri sio mbugila mbugila kama tunavyowaza.
Itafutwe pesa amani itapatikana na makasiriko yasiyo ya lazima yataepukika.
 
Hakuangamiza uovu; aliangamiza waovu. Waliozaliwa baada ya Nuhu walikuwa na asili ile ile ya dhambi ya Adam na Hawa. Hawakupenda kumfuata Mungu kama baba yao Nuhu, hatimaye wangaamizwa tena kwa moto katika miji ya Sodoma na Gomora. Waliozaliwa baada ya maangamizi ya Sodoma na Gomora wakapendelea dhambi badala ya kumpenda Mungu. Hukumu inakuja nayo ni moto wa milele
Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu?

Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii siku zote na wakati wote?

Mungu muweza wa vyote, kwa nini aliumba binadamu wenye uwezo wa kutenda dhambi na mabaya?

Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao tenda mema siku zote na wakati wote?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
 
Bado sijakupata ndo maana nasema unachanganya.. mungu na pesa ni vitu viwili tofauti Na havina uhusiano wowote.
Sikiliza, BLACKTIGER: kuna watu wanatafuta mapesa kwa nguvu zote, wakidhani kwamba wakipata mapesa watapata amani tele, furaha tele, uzima tele; lakini kinyume chake baada ya kupata mapesa wanajikuta bado hawana raha tele wala furaha tele wala amani tele kama walivyotarajia. Hivyo lengo la uzi huu ni kutuasa kwamba pesa peke yake haiwezi kutupa amani ya kweli, furaha ya kweli na uzima wa milele. Pesa tuitafute na Mungu tumtafute. Tukiwa na pesa, tukawa na Mungu pia katika maisha yetu tutapata yote yanayoweza kununuliwa kwa pesa na tutapata yasiyoweza kununuliwa kwa pesa kama vile amani ya kweli, furaha ya kweli na uzima wa milele. Hapo vipi. Tuko pamoja?
 
Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu?
Hili nimeishalijibu. Hakuumba dunia yenye uovu. Dunia ilikuwa perfect. Mwanzoni hakukuwa na magonjwa wala kula kwa jasho wala kifo. Hata mavazi hayakuhitajika. Uovu uliingia baada ya Adam na Hawa kuvunja vigezo na masharti. Lakini bado Yesu anatuandalia makao mengine yasiyokuwa na uovu.

Yohana 14:2-3

Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningewaambia. Naenda kuwaandalia makao. Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo nanyi mpate kuwepo.

Makao yanaandaliwa kwa wote wanaoamini. Wasioamini watatupwa katika moto wa milele
 
Itafutwe pesa amani itapatikana
Sijasema tusiitafute pesa. Tuitafute. Ila pesa peke yake haiwezi kutupatia amani ya kweli. Tukitafuta pesa, tusisahau kumtafuta pia Mungu awezaye kutupatia amani ya kweli na uzima wa milele. Uzima wa milele hatuwezi kuupata kwa mapesa.
 
Sikiliza, BLACKTIGER: kuna watu wanatafuta mapesa kwa nguvu zote, wakidhani kwamba wakipata mapesa watapata amani tele, furaha tele, uzima tele; lakini kinyume chake baada ya kupata mapesa wanajikuta bado hawana raha tele wala furaha tele wala amani tele kama walivyotarajia. Hivyo lengo la uzi huu ni kutuasa kwamba pesa peke yake haiwezi kutupa amani ya kweli, furaha ya kweli na uzima wa milele. Pesa tuitafute na Mungu tumtafute. Tukiwa na pesa, tukawa na Mungu pia katika maisha yetu tutapata yote yanayoweza kununuliwa kwa pesa na tutapata yasiyoweza kununuliwa kwa pesa kama vile amani ya kweli, furaha ya kweli na uzima wa milele. Hapo vipi. Tuko pamoja?
Ok lakini ufaham kwamba sio watu wote wanaamini katika huyo mungu unayemjua wewe
ndo mana nikasema pesa na mungu ni vitu tofauti
pesa tunaiona kila siku ila mungu hajulikani na hapatikani!
 
Hili nimeishalijibu. Hakuumba dunia yenye uovu. Dunia ilikuwa perfect. Mwanzoni hakukuwa na magonjwa wala kula kwa jasho wala kifo. Hata mavazi hayakuhitajika. Uovu uliingia baada ya Adam na Hawa kuvunja vigezo na masharti. Lakini bado Yesu anatuandalia makao mengine yasiyokuwa na uovu.
Nakuuliza hivi..👇

Huyo Mungu aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kuvunja vigezo na masharti?

Huyo Mungu Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii siku zote na wakati wote?

Kwa nini huyo Mungu aumbe binadamu wenye uwezo wa kuvunja vigezo na masharti wakati alikuwa na uwezo wa kuumba binadamu watakao fuata vigezo na masharti siku zote na wakati wote?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?

Yohana 14:2-3

Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningewaambia. Naenda kuwaandalia makao. Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo nanyi mpate kuwepo.

Makao yanaandaliwa kwa wote wanaoamini. Wasioamini watatupwa katika moto wa milele
 
Huyo Mungu aliumbaje binadamu wenye uwezo wa kuvunja vigezo na masharti?
Hili swali pia nimeishakujibu. Mungu alipowaumba Adam na Hawa aliwapa free will; hakuumba marobot. Labda utauliza tena: kwanini aliwapa free will? Huo ni uamuzi wake Yeye Muumbaji.
Warumi 9:20:
"Lakini, ee mwanadamu, u nani wewe umhojiye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kitamwambia yeye aliyekiumba, ‘Mbona umenifanya hivi?’"
 
ila mungu hajulikani na hapatikani!
Mungu hajulikani kwako wewe kwakuwa hujamtafuta kwa moyo wa dhati
Isa 55:6-7
Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.
 
Mungu mjuzi wa vyote, Alishindwaje kuwadhibiti Adamu na Hawa wasile hilo tunda?
Hakuwadhibiti kwa sababu aliwapa uhuru wa kuchagua mema au mabaya. Lakini aliwaonya kabla kwamba wakila tunda walilokatazwa watakufa. Hata leo Mungu bado anaonya kwamba kuna hukumu inakuja. Usitarajie atakudhibiti. Ukiamua kumkataa usimlaumu siku ya hukumu.
 
Hili swali pia nimeishakujibu. Mungu alipowaumba Adam na Hawa aliwapa free will; hakuumba marobot. Labda utauliza tena: kwanini aliwapa free will? Huo ni uamuzi wake Yeye Muumbaji.
Warumi 9:20:
"Lakini, ee mwanadamu, u nani wewe umhojiye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kitamwambia yeye aliyekiumba, ‘Mbona umenifanya hivi?’"
Freewill ambayo baadae inakuja kuingilia uhuru wako wa kufanya mabaya kwa kupewa adhabu kwa mabaya uliofanya, Hiyo sio freewill.

Huo ni mtego.
 
Back
Top Bottom