Ukiwa na miaka 45 bila nyumba jitafakari

Ukiwa na miaka 45 bila nyumba jitafakari

Naam kila mtu anastahili kuwa na sehemu ya kujihifadhi..., zamani nyumba ilikuwa asset ukimaliza, unasahau sasa hivi nyumba inaweza ikawa inakufilisi (maintanance n.k.) na kama sio mzee haujastaafu kuna tozo za kodi na sasa hivi mijini itafika wakati bila kuanzia ghorofa au aina fulani ya nyumba hupewi permit ya kujenga kwahio unaenda kujenga hukoooo in the middle of nowhere...

In short mfumo ninaouna unakuja ni mfumo wa mortgage (developers wanajenga nyumba za viwango sehemu nyingine hata ghorofa alafu watu mnapewa mortgage ya kununua hizo nyumba..., siku mkizeeka au vipi mnaziuza sababu hata kumuachia ndugu yako itabidi alipie inheritance tax na kama hajastaafu inabidi alipia kodi ya jengo (hapo kama hapangishi unakuwa haujamiachia asset bali liability)

In short mambo yanakwenda kwa kasi sana....
Nyumba gani hio mkuu inayokufilisi? Binafsi nimenunua magari aina mbali mbali na kujenga pia. Kamwe sijawahi kujuta kujenga. Na huwezi linganisha nyumba na magari hata magumu kama land cruisers ambayo maintenance yake ni ya juu sana na ya gharama. Is the best investment hata kama ni kijijini. Sasa sijui ww unaona investment gani ni nzuri zaidi mkuu.
 
Kujenga nyumba ni moja kati ya uwoga wa maisha, sana sana labda kwa wafanyakazi, wafanyakazi ndio wanao jenga, wafanyabiashara wanajenga ili iwaje? Uwekeze zaidi ya 50M kwenye ujenzi badala ya kuizungusha?
 
Location..., Location..., Location

Tunakoelekea lazima ulipie yafuatayo katika nyumba husika
  • Cleaning / Upkeep (hivyo kama eneo ni kubwa kuliko uwezo wako wa kufanya mwenyewe lazima uweke mfanyakazi na usipoweka mfanyakazi ufanye mwenyewe bado utalipia gharama ya muda.
  • Kodi ya Jengo; Kama hupangishi hivyo hauingizi ni kwamba unazitoa.
  • Maintanance; Nyumba inahitaji maintenance..
Kwahio utaona kwamba kuna cultural changes nyumba badala ya kukuingia inaweza ikakugharimu hususan huku Bongo ambapo wapangaji sio wastaarabu (rent kulipa shida na wakiondoka uharibifu ni mkubwa) na wakikupa pesa nzuri ni usumbufu wa kurekebisha hiki au kile..., unaweza ukaamua kufukuza wote ili hata uweke mifugo....
 
Hata baba yako alikuwa anajitahidi familia yenu muwe na maisha mazuri na mlale sehemu nzuri sidhani kama mtu kuwaza kujenga ni vibaya au ni kufanya mashindano!!!

Unless uwe umemuelewa vibaya mleta mada au mimi ndiye sijakuelewa.
Kuwaza kujenga na kujenga is one thing which is well and good....

Kufikia umri fulani na kuanza kujitafakari / na kupata msongo wa mawazo sababu haujajenga is quite another; One is good another inaweza ikakufanya uishie kwenye matatizo
 
Ni mfumo tuu mbona wenzetu ( huko tunakosema wana good life) wana rent mpaka wa wanaondoka duniani
 
Mwanaume akifikisha miaka 45 hadi 50 hapo kibongo bongo walio wengi ndo angalau huwa yuko vizur kimaisha na hii ni kutokana na changamoto za maisha tunazokutana nazo kwenye maisha katika kujipanga na kujiweka sawa kimaisha...

Ila kama hauna hata haka na uko na miaka 45 hadi 50 hapo inabidi kujitafakari upyaa ni wakati wa kuamka toka usingizini.....
Asikuambie mtu kuwa mwanaume sio jambo dogo na jepesi hata kidogo[emoji848][emoji848]
View attachment 2078457View attachment 2078458View attachment 2078459View attachment 2078455
GENTAMYCINE, ujumbe wako huo
 
Kujenga nyumba ni moja kati ya uwoga wa maisha, sana sana labda kwa wafanyakazi, wafanyakazi ndio wanao jenga, wafanyabiashara wanajenga ili iwaje? Uwekeze zaidi ya 50M kwenye ujenzi badala ya kuizungusha?
[emoji848][emoji848]kumbe wafanyabiashara hawajengagi nyumba sikujia
 
Back
Top Bottom